Thursday

U-20 SIMBA KUTETEA UBINGWA WAO KUANZIA JANUARY

0 comments

Michuano hiyo ya ligi kuu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inatarajiwa kuanza rasmi mapema Mwezi ujao kwa kushirikisha timu za vijana kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara, imefahamika.
Kwa mujibu wa afisa habari wa shirikisho la soka nchini ‘TFF’ michuano hiyo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, timu 16 zitapangwa katika makundi mawili ya timu nane nane ambapo zitatafutwa timu mbili kutoka katika kila kundi kucheza hatua ya fainali ili kumpata Bingwa.
-Kutakuwa na makundi mawili, kwa kila kundi kuwa na timu nane, ambazo zitapangiwa kituo then wale watakaofanya vizuri watakutana kwenye fainali, na matarajio yetu ni kuwa michuano hii itaanza mapema mwakani licha ya kwamba bado tarehe rasmi haijapangwa,” Alfred amesema.
Udanganyifu wa umri.
Katika kuhakikisha kuwa msimu huu hakutakuwa na udanganyifu wa umri kwa washiriki TFF imepanga kufanya kila jitihada ili kuhakikisha washiriki wote wanakuwa na umri sahihi wakati wa mashindano hayo.
-Kanuni inasema wale wote wanaoshiriki wanapaswa kuwa vijana, sisi safari hii tulikuwa tunapambana ili tupate mdhamini mwingine ambaye angesaidia kama kunatokea udanganyifu kama ikiwezekana tuwe na vipimo rasmi, hilo bado linaangaliwa lakini likishindikana basi tutatumia mbinu ya kuangalia vyeti vya kuzaliwa,” Amesema.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na Azam TV ni timu ya vijana ya Simba ambao mwaka jana waliifunga Azam katika mcheza wa fainali kwa penati 8-7 baada ya muda wa dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.asante kwakutembelea mashele blog