Wednesday

Lipuli wamtahadhalisha kwa barua Asante Kwasi

0 comments

 
Klabu ya Lipuli FC 'Wanapaluhengo' yenye maskani yake mkoani Iringa imesema imemuandikia barua mchezaji wake Mghana Asante Kwasi kuripoti mapema kazini Kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yake.
Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa klabu ya Lipuli FC Ramadhan Mahano amesema Kwasi alitakiwa kuwa awe ameripoti tangu Disemba 17 lakini mpaka sasa siku mbili zikiwa zimepita Bado hajaripoti kazini jambo ambalo ni utovu wa nidhamu.
Amesema walimpatia ruhusa ya kwenda kwao nchini Ghana kwa ajili ya kuhani msiba wa baba yake, na ruhusa yake ilikuwa inafikia tamati Disemba 16 lakini wakijua wazi kuwa tayari ameshawasili nchini Lakini wanashindwa kuelewa kwa nini bado hajafika kambini.
-Tumemuandika barua (Kwasi) kumtahadhalisha kuhusu kitendo chake cha kutofika kazini, alitakiwa awe amefika kambini toka Jumapili lakini hadi sasa hivi hatujamuona, ajue tu kuwa bado ni mchezaji wetu na anatakiwa kuheshimu taratibu za klabu," Mahano amesema.
Hatujaongea na Simba.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema anashangaa kusikia taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa wao kama Lipuli tayari wameshakubaliana na Simba SC kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo ambaye amekuwa na kiwango cha hali ya juu.
-Niseme wazi Simba bado hawajatufuata kuzungumza na sisi, imepita wiki sasa toka huu mjadala uanze lakini niseme wazi Simba hawajatufuata na hatujakubaliana chochote, hivyo Asante Kwasi ni mchezaji wetu bado," Mahano alisema. asante kwa kusoma masshele blog
Kumekuwa na sintofahamu kwa takribani juma moja sasa kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo ambaye awali taarifa zilisema tayari ameshasajili kuitumikia Simba kwa mkataba wa miaka miwili, huku Lipuli wakidai kuwa bado hawajafuatwa kwa utaratibu wowote wa kumsajili mchezaji huyo.