Duniani kote, yapo matbaa ambayo yamekuwepo kwa miaka ayami na kwa hilo, yamefikia kiwango ambacho huenda tukadhani hatuna uwezo wa kufika wala kufikia yaliko. Jinsi matbaa ya humu Nchini Kenya yalivyo kwa sasa, ni dhihirisho tosha kuwa twasonga mbele kila kuchao. Baadhi ya Matbaa maarufu katika uchapishaji wa vitabu ni:

  1. Oxford University Press East Africa Ltd. [OUP EA]
Oxford University Press Ltd ni shirika linalo ongoza kwenye uwanda huu wa  uchapishaji kote katika kanda hii ya Afrika Mashariki. Tawi la kwanza lilianzishwa mwaka wa 1954 Nairobi, Kenya; Likiwa chini ya mwavuli wa Idara ya Kimataifa ya Oxford University Press. Huu nd’o ulokuwa mzizi wa matawi mengine yaliofuatia katika miji ya Dar es Salaam, Tanzania na Kampala, Uganda.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu
Kamusi ya Kiswahili Sanifu
Kwa miaka ayami sasa, matbaa hii imechangia pakubwa ukuzi wa lugha na waandishi pia. Mwanzo, zipo bewa na vipera tofouti vinavyo hakikisha kuwa kila mwanaelimu ana natijika vilivyo. Kuanzia shule za chekechekea, za msingi, za upili na vyuo vikuu. Toleo la kwanza lilikuwa laKamusi ya Kiswahili Sanifu mwaka wa 1981 kisha Kamusi ya Semi za Kiswahili mwaka uo huo.
Afisi kuu za OUP EA zipo katika eneo lenye mandhari na taswira ya kuvutia: Upper Hill, Nairobi katika barabara ya Elgon mkabala na Hospital Road.
  1. Matbaa ya Focus
Hili ndilo shirika la uchapishaji linalokua kwa kasi zaidi nchini Kenya. Tangu jadi, limepokea takirima si haba na lingali latakirimiwa. Kwanzia riwaya kama vile The River and The Source na vingine ambavyo vimo kwenye kapu la utunzi na ubunifu. Yapo maswala mengi yanayoipa matbaa hii sababu ya kuvishwa koja kila mwaka iwapo si kila mwezi. Mfano wayo ni inavyojitosa katika uandishi wa vitabu ambao hauzingatii tu maadili ya binadamu, bali pia kanuni za utafiti na kitabibu.
Vitabu vyao ni mvuto mkubwa kwa wasomi wote tena wa Nyanja na vidato tofouti. Waandishi wavyo nao ni wa kutajika na walo kolea vilivyo. Kwa maana hii, waandishi ibuka wametiwa ilihamu ya kujitosa pia kwenye ulingo huu… Bila shaka yapo mengi yakutarajiwa ‘toka kwa matbaa hii ya Focus. Afisi zake zapatikana McGeorge Centre, Factory Street, barabara ya Bunyala.
  1. Matbaa ya Vide-Muwa
Unaitwa Nani?
Unaitwa Nani?
Iwapo pana shirika la uchapishaji vitabu ambalo kweli limepiga hatua ya kuwapa fursa waandishi ibuka kati ya mashirika mengine nchini, ni vide-muwapublishers. Licha ya kuwa nd’o matbaa changa zaidi, uendelevu wake ni wa kupigiwa mfano. Kwa hakika, lengo lao la kuwa shirika lenye ufanisi, uaminifu na lenye mfano aula kwa wengi, tayari limepiga hatua kubwa.
Musaleo
Musaleo
Kufikia sasa, Vide-Muwapublishers [Kogo Star Plaza, Nairobi West, barabara ya Langata] imeshinda tuzo ya Jomo Kenyatta Prize katika Fasihi kupitia vitabu vya Musaleo! (2005), Msimu wa Vipepeo (2007), Unaitwa Nani? (2009) na kupitia msururu wa machapisho ya ushairi.
Shirika la East african Publishers lilizinduliwa mwaka wa 1965 [Wakati huo ikitambulika kama Heinnemann Educational Books (EA) Limited] wakati wachapishaji wawili ‘toka Uingereza Heinemann na Cassell, walitia msingi kwa lengo la uchapishaji jijini Nairobi. Nyakati hizo ndizo vitabu kutoka Uropa vilikuwa vyauzwa Afrika kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wana Afrika. Mwaka wa 1972, mwenyekiti wa sasa, Dkt Henry Chakava aliteuliwa kuwa mhariri wa kwanza mkuu kwenye Taasisi ya Heinemann. Kwanzia wakati huo, shirika hili limepiga hatua nyingi za ufanisi hadi leo.
Kill me Quick
Kill me Quick
Yajapo maswala kuhusu tuzo za shirika hili, yafaa kuwa kimya tu maana’ke hata hazihesabiki. Kwanzia mwaka wa 1974, matbaa hii haijapewa kisogo na nyingine yeyote. Katika vitengo vyayo vyote, haijakosa kutakirimiwa… Ukweli ni kuwa limejizatiti kubadilisha maadili yenye doa katika jamii zote Duniani. Lengo kuu ni kuchapisha kazi yenye thamani ya kudumu, kukata katika wigo wa kijamii, kitamaduni, kisiasa, kiuchumi na wakati uo huo, kuwa mtawala mkuu biasharani licha ya vigezo na changamoto katika uga huu.
Baadhi ya vitabu vilivyochapishwa na matbaa hii ni kama vile; Kill Me Quick- Meja Mwangi, Emmanuel Mbogo- Vipuli vya Figo, Ngugi wa Thiongo- Gaitaani Mutharaha-ini, Yusuf Dawood- Eye of the Storm n.v
  1. Matbaa ya Longhorn / Sasa sema
Longhorn Publishers ni Kampuni ya uchapishaji ambayo kichwa chake ki’ nchini Kenya. Kutokana na ubora wa kazi  na uzingativu wa lengo lake, matbaa hii imezindua matawi mengine katika nchi ya Uganda, Tanzania na Rwanda. Biashara yake kuu ni usambazaji wa maendeleo, uchapishaji na masoko ya vitabu vya elimu kwa ujumla. Hili limedhihirika kote tena na watu wengi.
Chini ya shirika hili, pana tawi la uchapishaji kwa jina Sasa Sema Focus ambalo hujishughulisha na uchapishaji wa aina na fani zote za uandishi. Kwa kiwango kikubwa, Longhorn Publishers imeleta mabadiliko katika muundo na ubora wa bidhaa kupitia Sasa Sema. La mno ni kuwa ukuzaji wa lugha ya Kiswahili umepigiwa upato na shirika hili. Vipo vitabu vingi ambavyo vimewafaidi wanagenzi wengi. Baadhi ya vitabu hivyo ni kama vile; Kamusi ya Karne ya 21, Riwaya ya Utengano [kiswahili], When The Sun Goes Down na The Blue Sweater.
Afisi zake Nchini Kenya zapatikana kwenye barabara ya Funzi, Industrial Area.
Ni vyema kujivunia Matbaa/Mashirika na Kambuni hizi miongoni mwa nyingine ambazo kwa kiwango kikubwa, zimechabgia kuwepo kwa ufanisi, amani, mlahaka mwema, ndoto komavu, ari na zaidi, ukuzi wa lugha na utamaduni wa Waafrika.
(function(d, s, id) { var js