Kocha aliyekabidhiwa majukumu mazito ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club, Mrundi Masoud Djuma amesema mipango yake baada ya kupewa kikosi hicho ni kurudisha heshima na morali.
Amesema atafanya hivyo kwa wachezaji mashabiki na wanachama wa timu hiyo ambao kwa kuanzia ni lazima aifunge Ndanda FC kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mjini Mtwara.
-Nafahamu mashabiki na wanachama wamepoteza imani na timu yao, lakini nitahakikisha imani yao inarejea na hiyo ni kushinda mechi zijazo, tunachopaswa kukifanya sasa ni kusahau yaliyopita na kuangalia yaliyopo mbele yetu, Bado timu ni nzuri na kikosi ni kipana,” amesema.
Djuma alisema katika mazoezi ya Jumapili asubuhi alitumia muda wake kuzungumza na wachezaji ili kila mmoja kujua jukumu lake ndani ya timu, Nataka kila mchezaji aelewe jukumu lake uwanjani, kwani tunachohitaji sasa ni ushindi pekee na si kitu kingine, hivyo Wana Simba wategemee baadhi ya mabadiliko yenye mafanikio katika timu yao,” aliongeza.
Djuma alisema mipango yake ni kurejesha Simba katika kiwango bora kwani anafahamu kiu ya Wanasimba wote ni mafanikio na kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Suala la nidhamu.
-Kuhusu suala la nidhamu Simba ni jambo la ndani sana si kulitoa nje, ila binafsi napenda mchezaji afahamu majukumu yake, pamoja na mambo mengine nidhamu ni kitu cha msingi sana katika timu,” alisema Djuma.
Kumuhusu Kocha Joseph Omog aliyetimuliwa Jumamosi Djuma amesema anamuheshimu na anaheshimu kila kitu ambacho amekiweka kwenye timu ila itamlazimu kubadilisha baadhi ya mambo.
-Omog alikuwa ni bosi wangu na nilimkuta, ana mfumo wake japo wakati mwingine tulijadiliana, ila mimi nina mfumo wangu huo ambao mara nyingi napenda kuutumia, “alisema akizungumza na Mwanaspoti.
Djuma Baada ya Simba kutolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup nafasi pekee ambayo timu hiyo imebakisha ili kushiriki michuano ya kimataifa ni kushinda taji la ligi kuu, na wataanza kampeni yao Disemba 31 kwa kucheza na Ndanda FC mkoani Mtwara.