Timu ya soka ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam imevuliwa Ubingwa wa Azam Sports Federation Cup na kuwa timu ya kwanza ya ligi kuu kuondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa kwa penati 3-4 na timu ya daraja la pili Green Warriors.
Simba ambao walicheza kandanda safi toka Mwanzo wa mchezo lakini walishindwa kuhimili nidhamu na Hali ya kujituma waliyoonesha Green Warriors katika mchezo huo.
Mpaka dakika 90 zinakamilika Matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1 huku Green Warriors wakiwa wakwanza kupata bao kupitia kwa Hussein Bunu kabla ya Simba kusawazisha kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Nahodha John Bocco Raphael.
Mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo akaamuru ipigwe mikwaju ya penati kuamua timu itakayopita hatua ya ndipo Green Warriors wanaibuka washindi kwa kupata penati 4 huku Simba wakipata penati 3.
Waliokosa penati.
Waliokosa penati kwa upande wa Simba ni Mzamiru Yassin, Mohammed Hussein pamoja na Jonas Mkude wakati waliopata walikuwa ni Erasto Nyoni, Shizya Kichuya na John Bocco.
Hii ina maana kwamba Kama Simba watahitaji kushiriki michuano ya kimataifa Kwani msimu wa 2018/19 watapaswa kunyakua taji la Ligi kuu soka Tanzania Bara asante msomaji Wa masshele blog , happy new year ,