Sunday

Simba ni mwendo wamakombora tu sasa

0 comments


Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi yao ya leo dhidi ya Mbeya City lakini Kocha Joseph Omog ameonekana kusisitiza mashuti langoni mwa wapinzani wao.

Mazoezi hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana.

Omog alionekana kusimamia mazoezi ya wachezaji wake hasa viungo na washambulizi kuhakikisha wanapiga mashuti kila wanapopata nafasi.

Kocha huyo Mcameroon, alikuwa akiwasisitiza kulenga lango na waliokosea walirejea tena kuhakikisha wanafanya vizuri.

Mazoezi ya Simba chini ya Kocha Omog yamefanyika kwenye Uwanja wa Sokoine ambao mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kesho, itapigwa hapo.