Vitu hivyo ni muhimu sana katika kuhakikisha afya yako inakuwa salama hata baada ya kutumia maji hayo.
Makapuni yanayotengenezwa vinywaji yanalazimika kuchapisha viambatanisho vilivyowekwa kwenye bidhaa hizo. Chupa nyingi za plastiki huwa na maneno kama PP, HDPE au HDP kwa chini yaliyozungukwa na kama alama ya pembe tatu. Chupa hizi huwa ni salama kwa sababu huwa hizitoi sumu kwenye maji.
Katika makala hii tutakueleza hatua chache unazotakiwa kuzipitia kuweza kupata aina bora ya maji. Hivi ndivyo vitu anavyotakiwa kuviangalia kwa makini unaponunua maji.

Hii hutoa kemikali na chuma (metals) ambavyo huathiri uzalishaji wa homoni katika mwili wa binadamu.
HDPE or HDP
Alama hizi ni salama. Maji kwenye chupa zenye alama hizi unaweza kuyanunua sababu inamaanisha ni bidhaa bora. Chupa zenye alama hizi huwa hazitoi kemikali na sumu kwenye maji.
PVC or 3V
Alama hizi huwakilisha aina mbili za sumu ambazo huathiri ukuaji wa homoni katika mwili. Si salama kwa matumizi ya binadamu.
LDPE
Chupa hizi hazina na wala hazitoi kemikali, lakini si salama kwa ajili ya utengenezaji wa chupa za plastiki. Hii huwekwa kwenye mifuko ya plastiki.
PP
Hii huwa na angavu (transparent) mara nyingi hutumiwa kwenye kuwekea mtindi au maji matamu.
PS
Alama hii huonekana mara nyingi kwenye makasha ya kuwekea vyakula (fast food) na vikombe vya kahawa. PS inamaanisha kuwa plastiki hutoa gesi aina ya carcinogens kwenye kilichomo ndani. Tembelea masshele blog kila mara pia nitumie comment yako wasapp +255766605392 pia click picha za juu endelea hapo chini
Non-labelled plastic or PC
Hii ni plastiki hatari sana. Japokuwa hutoa BPA, baadhi ya watengenezaji huitumia kutengenezea makasha ya kubebea chakula na chupa za michezo za kuwekea maji ya kunywa.
Muhimu: Kila unaponunua kinywaji au kitu kilichohifadhiwa ndani ya plastiki angalia chini ya chombo hicho kujua ni aina gani ya plastiki