Pyongyang imesema Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) linapanga njama ya kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwa kushirikiana na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini.
Wizara ya Usalama wa Ndani ya Korea Kaskazini imesema ina taarifa za kiintelijensia kuwa Washington inapanga njama na Seoul ya kumuua Kim Jong-un kwa kutumia silaha za kibiolojia katika mojawapo ya sherehe za umma mjini Pyongyang.
Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa na Pyongyang imesema kuwa, CIA na Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia kemikali ya sumu ya nano na kwamba njama hizo ni sawa na Marekani kuitangazia vita Korea Kaskazini.
Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu kilomita elfu sita na 760.
Hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani katika kile wadadisi wa mambo wanasema ni kujaribu kupotosha fikra za walio wengi, alisema yupo tayari kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ikiwa kutaandaliwa mazingira ya kufanyika mazungumzo hayo. TANGAZO, KWA KUWA MASSHELE BLOG INA KUJALI WEWE MSOMAJI WETU INGEPENDA KUKUSHIRIKISHA KATIKA FURSA MUHIMU , WASILIANA +255766605392 KWA MAELEZO ZAIDI