Saturday

HISTORIA YA WASUKUMA HII HAPA

0 comments

Duu..! kumbe kihistoria kabila la wasukuma chimbuko lake ni Ethiopia.! tembelea kijiji cha wasukuma bujora utajua mengi.

Dada Maria Nyanjige akinionesha na kunielezea zana za jadi zilizokuwa zikitumika na kabila la kisukuma katika kujilinda katika mambo mbalimbali ikiwemo na kupambana na maadui
Pichani nikiwa nimepozi na Dada Maria Nyanjige ikiwa ni kama picha ya ukumbusho na shukurani tele kwake kwa ukarimu mkubwa aliotuonyesha,tangu tunafika kijijini hapo na mpaka tunamaliza kubarizi maeneo mbalimbali ya kumbukumbu ya kabila la Wasukuma.
Nyumba illiyokuwa ikihifadhi vifaa mbalimbali vilivyotumika kwa ajili ya michezo ya kabila la Kisukuma Bagika na Bagala, yaani utamaduni uliokuwa na ushindani mkubwa kama vile wa Simba na Yanga.
Hii ni nyumba maalum ambayo ilitumika kuhifadhia madawa, na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kufanyia tiba ya kiasili.kwa kawaida hujengwa kwa nyasi,lakini hii ionekayo pichani ilifanyiwa ukarabati kama uonavyo ili kuongeza uimara zaidi wa dawa zilizokuwa zikihifadhiwa kwenye ghala hilo.

Huu ni mfano wa eneo lililotumika kwa kufanyia maombi ya kimila na kufanya toba (sehemu ya tambiko) kwa kabila la Kisukuma,kabla ya wazungu na waarabu kuleta dini zao.
Pichani ni mawe matatu yayolikuwa na kazi muhimu katika eneo la nyumba ya msukuma,jiwe la kwanza kulia lilitumika kusagia dawa mbichi,jiwe la pili lilitumika kuogeshea watoto wachanga pamoja na kusagia chakula cha mbwa,na jiwe la mwisho lilitumika kusagia dawa kavu.
Hili ndilo kanisa lililoanzishwa ndani ya kijiji cha makumbusho cha Bujora na Padri Daud Fumbuka.
Pichani ni nyumba iliyohifadhi ngoma hizo zinazopigwa wakati Chifu wa Kisukuma anapokuwa na matukio muhimu, lakini pia imejengwa katika mfano wa kiti alichokuwa anakalia chifu wa kisukuma kama uonavyo kwa chini.
Pichani ni sehemu ambayo Kabila la kisukuma walitumia kufundishia kuhesabu kwa lugha ya kabila hilo,hata kama watoto/watu walikuwa hawajui kuandika na kusoma lakini walifanikiwa kufundishwa kuhesabu kwa njia ya kipekee kabisa kwa kutumia lugha ya kisukuma.
Ramani inayoonyesha majina ya majimbo yaliyokuwa yakitawaliwa na machifu mbalimbali wa kabila la Kisuma.
Ni nyumba ambayo ilikuwa ikitumiwa na kabila la Kisukuma kwa ajili ya kujihifadhi,lakini pia ilitumika kuhifadhi vifaa mbalimbali vya uhunzi.
Sehemu ambayo walikuwa wakifanyia uhunzi wa zana mbalimbali wa kabila la Kisukuma.
Pichani Dada Maria Nyanjige akiielezea mfano wa ngoma iliyokuwa ikitumika wakati Chifu wa Kisukuma anaoa ama anasimikwa kuwa chifu au akiwa amefariki Dunia, ngoma hii ilitumika kupigwa katika matukio hayo matatu.

Maria Nyanjige akifafanua jambo huku akiweka msisitizo mkubwa.Maria alisema kuwa kihistoria asili ya kabila la Msukuma ni nchini Ethiopia,na akaongeza kuwa kabila la wasukuma limegawanyika katika sehemu tatu,kwamba kuna wasukuma wa Mwanza,kuna wasukuma Tabora pamoja na Wasukuma wa Shinyanga,akaeleza kuwa pamoja kugawanyika kwa makabila hayo lakini bado yana lafudhi inayotofautiana kwa namna moja ama nyingine.
Bango kubwa la utaratibu ndani ya sehemu ya mapokezi.
Pichani ni Mpiganaji mwenzangu wa Blog ya Fullshangwe,Bwa.John Bukuku akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mhifadhi msaidizi wa kijiji cha makumbusho ya Bujora ,Dada Maria Nyanjige kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo kijiji hicho.

===== ===== ===== ==== ===== ===== .
Historia kwa ufupi ya makumbusho ya kijiji cha Bujorwa,Kisesa jijini Mwanza.

Mapema leo mchana tulifanya ziara fupi ndani ya kijiji cha makumbusho cha kabila la Wasukuma kiitwacho Bujora,kilichopo maeneo ya Kisesa,ni kama umbali wa km 20 hivi kutoka Mwanza mjini na kufika kwenye kijiji hicho,ambacho kimewekwa/jengwa maalum kwa ajili ya kuhifdhi vitu mbalimbali vilivyotumika na kabila la Wasukuma enzi za ukoloni.

Kwa mujibu wa mwenyeji wetu Dada Maria Nyanjige anasema mahali hapo palianzishwa mwaka 1954 na Padri Daud Clement Fumbuka wa kanisa katoliki jimbo la Mwanza, anasema na kuongeza kuwa Padri huyo hakuwa na nia ya kuanzisha kanisa mahali hapo ,bali alipenda kujua mila na desturi za kabila la Wasukuma, Wakati huo alipokuwa rafiki mkubwa wa Askofu Joseph Blomjons wa jimbo kuu la Mwanza wakati huo ikiwa mnamo mwaka 1965.

Baadae Padri Daud Fumbuka alienda huko Sumve zamani kukiitwa (Lumve) ambako alijifunza lugha ya kisukuma kwa miezi sita, baada ya kutoka Sumve ndipo akarejea tena Bujora zamani pakiitwa (Kujorwaningo) kutokana na eneo hilo kuwa la hatari , palikuwa si mahali salama kwa sababu kulikuwapo na wanyama wakali na pia ilikuwa ni sehemu ambayo watu wabaya waliookuwa wakiwanyoga wapita njia na ndio maana pakabatizwa kwa jina la (Kujorwaningo), yaani kwa kisukuma kunyonga shingo.

Mnamo Mwaka 1958 Padri Fumbuka alianzisha rasmi kanisa la katoliki hapo Bujora na kuendelea na huduma ya kuhifadhi mila, desturi na tamaduni zote za kisukuma mpaka mwaka 1968, ambapo ndipo ikarasimishwa kuwa ni makumbusho rasmi ya Bujora na hatimaye kutambuliwa na Serikali.

No comments:

Post a Comment