Saturday

AJALI MOSHI KILIMANJARO , KADHAA WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA

0 comments


Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha usiku huu wa Ijumaa Octoba 18,2024 baada ya Bus dogo la abiria aina ya Costa linalofanya Safari zake kati ya Arusha na Moshi Kilimanjaro kugongana Uso kwa uso na lori la Mafuta.

Ajali hiyo imetokea katika daraja la Kikavu lililopo Kwasadala barabara kuu ya Moshi Arusha majira ya saa tatu usiku kilometa chache kabla ya kufika Moshi Mjini.

Bado tunaendelea kufuatilia taarifa hizi kutoka mamlaka husika, endelea kukaa karibu na Mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa hii kiundani zaidi.

HABARI KAMILI

WATU 14 wamefariki Dunia na wengine kujeruhiwa baada ya gari aina ya Costa walilokuwa wakisafiria kutoka Moshi kwenda Arusha kugongana na lori la mizigo eneo la mto kikavu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, Nurdin Babu alisema kuwa, ajali hiyo imetoa usiku wa kuamkia Oktoba 19 mwaka huu ambapo gari ya abiria aina ya Costa ikitokea Moshi kwenda Arusha iligongana na lori la mizigo. 

Babu alisema kuwa, katika ajali hiyo watu sita walifariki Dunia pale pale na wengine nane walifariki wakiwa njia kukimbizwa hospitali huku majeruhi wengine wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Hai na Hospitali ya Rufaa ya kanda ya KCMC. 

"Serikali ya mkoa tunasikitika sana kupoteza nguvu kazi ya watu 14 ambao walikuwa wanaenda kwenye shughuli zao na nitumie nafasi hii kutoa pole kwa ndugu wote waliopoteza wapendwa wao lakini tunazidi kuwaombea Majeruhi wote wapone haraka na kuendelea na shughuli zao" Alisema Babu.

No comments:

Post a Comment