![]() |
Moja ya picha ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kufariki kwa Mangi Mashelle wa shimbi |
Historia ya ukoo wa Mashelle
Dhana ya ukoo
Ukoo Ni muunganiko wa kimbari ambao huunganisha familia zilizo na chanzo kimoja (Mababu) ukoo huweza kukua na kupelekea kugawanyika kwa vitongoji kadhaa. Vilevile ukoo huweza kugawanyika kwa sababu za kigeografia. Katika makala hii tutazungumzia ukoo wa Mashelle ambao unaasili ya Mkuu, Shimbi.
HISTORIA YA SHIMBI (chimbuko la ukoo wa Mashelle)
Uruka wa Shimbi (nchi ya Shimbi)
Ukoo wa Maria kawishe (Kavishe) Shimbi ndio chanzo hasa Cha Mashelle. Ukoo huu wa Maria kawishe ukianza Shimbi Karne nyingi zimepita na mwanzilishi wa ukoo huu aliitwa M'mamba aliyetokea mamba kwa kirie na wakati akitafuta makazi mapya ardhi yenye rutuba ndipo alipoweka maskani yake katika uruka wa Shimbi (nchi ya Shimbi) na hapo ndipo ukoo wa Maria kawishe ulipoanzia.
Kwa mujibu wa sensa ya wanaukoo mwaka 1993 hivi ndivyo vizazi vya wanaukoo
M'mamba akamza Kitimbiri, Kitimbiri akamzaa Ileti na Makaviha.
A. Ileti akamzaa Mhambo, Latemba, Msheve na Kisinga.
Mahambo akamzaa, Rimbisha, Kiorumu na Kituunga.
Latemba akamzaa Kivese na Sangio.
Msheve akamzaa Mlesani , na Kasimiri
Kisinga akamzaa Mboloso.
B: Makaviha akamzaa Mashaare, katika uzao wa Mashaare akawazaa Lamasawe, Mashelle na Mkave Pia Mshakai , Masaule, mwashile & Kyauka , Mshau & Mriaumbe.
Sasa tutahamia Kizazi Cha Mashelle ambalo ndio lengo hasa la makala hii
N.B. vizazi vitakavyowekewa mabano wamezaliwa kwa mama mmoja. Tutakumbuka kuwa Mashelle alikuwa na wanawake wengi (mitara)
1. Mashelle akamzaa (Leina & Stambuli ) , (Karufu &Stamesa) , Marikoso na Kastabu
Marikoso akamzaa Ameli , Ameli akawazaa Juma, Revokati, (policarp & Francis) Juma akamzaa Narsis, Revokati akamzaa Rustus
2: Mashelle akawazaa Tena Rabdiel na Daudi.
Rabdiel akamzaa Michael na (Felisian, baltazari, na Reginald) Michael akamzaa Edgar
Daudi Akawazaa Joseph , Gasper, na (Leonard , Rogasian, Adelin, Just, Joachim, na Evodi)
Joseph Akawazaa (Florian, Beda, Priscus) Gasper Akawazaa (Edward na Bruno)
3: Mashelle Akawazaa tena
Salia , Baiseli, Samuel na Mtafanye(selasin).
Salia akamzaa (Joseph , Sabas, Policarp na silvest)
Baisel akamzaa Machakos Na (Gasper Joseph na Nolascos)
Samuel akamzaa (Dominic &Severing)
Mtafanye akamzaa Mark
Machakos Akamzaa Tablei
Mark akamzaa (Alexander Living & Cosmas)
4: Mashelle Akawazaa Tena
Sabini, Fulani, na Faradi
Sabini Akawazaa Didas, Roman na Saturnine
Didasi akamzaa Evodi,
Romani akamzaa (Felician & Frederick
Fulani Akawazaa (Simon , Elia & Victus)
Faradi akawazaa Joseph & Gasper
5: Mashelle Akawazaa Tena
Leseri, Tilisho, Rajabu, Sausiku
Leseri kamzaa Aloise
Tilisho Akawazaa(Peter &John
Rajabu Akawazaa (Pauli, Damas, Alexander na Peter)
6. Mashelle Akawazaa Tena
Abeid na Afnail
Abeid Akawazaa
Armogast, Tarimo na Antipas
Afnail Akawazaa, Bonifas, Adelin, na Peter
Armogast Akawazaa Oscar , Emmanuel, na Osmund
Tarimo akamzaa Vinus
Bonifas akamzaa Beatuce,
Adelin akamzaa Donacian na Fidelis
Peter Akawazaa(John , Thad3i, Fulgence, Frederk
7: Mashelle Akawazaa Tena
Hamisi na Kashili
Hamisi akamzaa Roki, Akwilin, Michael, iddi
Roki akamzaa Venance, Makarius, Liberati, Luka
Akwilin akamzaa Edward na Josephat
Michael akamzaa Christopher
Iddi akamzaa Abas na Hemed
Kashili akamzaa, (Michael Ferdinand, Clemence , Gabriel na Aristark)
8: Mashelle Akawazaa Tena
Ndesaika , Kashomba (cosma) na Kisawani
Ndesaika Akawazaa Faustin na prosper
Kashomba Akawazaa Roman na Edward
Kisawani Akawazaa wilbard , Adams, Orest, Paul, Thomas na Gasper (baba yangu)
Faustin Akawazaa Morgan , Innocent, Daudi, Lasco, na novatus.
Roman Akawazaa Cosmas, Jamhuri, na Alois,
![]() |
Picha ya mzee ndesaika Mashelle |
9. Mashelle akamzaa Tena Leina
Leina Akawazaa Masumbuka, William, Francis, na afrika
Masumbuko Akawazaa Prosper na chrispn
William Akawazaa Joseph , Policarp, Ludovic nestory na Mathias
Francis akamzaa John , Afrika akamzaa Didas na John
John akamzaa Alfred , Didas akamzaa Joseph
Leina Akawazaa tena
Stephen na (Joseph, Roman, Damas, Adolf, na inyasi
Stambuli Akawazaa Shauri, baltazari, na Gasper
Baltazari Akawazaa (bonifasi, Beati, Daniel na Bazili
Karufu akamzaa Satoti na Fasili
Satoti akamzaa Pauso Gabriel na Policarp
Pauso akamzaa Mosoi, Joseph, Paul, Ludovic na Colman
Gabriel akamzaa living na Vicente
Fasil akamzaa Yohan Na Dismas
Yohani akamzaa Andrea na Maroni
Dismas akzaa Karoli
Karufu akamzaa pia Thadei na Francis
Thadei akamzaa Justi, Wilhelm , Ulirk, na Innocent.
Francis akamzaa Joseph , Romani, Avelin na Modest.
STAMEZA
Akawazaa Kalist , Winston Damas, na Michael
Kalist akamzaa Hermeti, Perfect, na Regoberto
Winston akamzaa Deograsias na Valentin
Damas akamzaa, Revokati, Christopher, Deonis, Victoria, na Frimin,
Michael akamzaa, Eliuter na Isdor
STAMEZA Akawazaa Tena
Shilven , Eugen, Salvator, Policarp
shilven akamzaa Ladislaus, na Edmund
Eugen akamzaa, Gido na Novati,
Salvator akamzaa Abauku, nocholaus na Geming,
Policarp akamzaa , Gasper, Silvest Thadei na Priscus
KIZAZI KILICHOHAMIA SHIMBI TOLA USERINA KUKAA KWA MANGI MASHELLENA KUSHIRIKI MAMBO YOTE YA UKOO KATIKA KITONGOJI CHA KARUFU
Kimoruru akamzaa Issa, isaa akawazaa Wilbard na Pascal
Wilbad Akawazaa Ulirk , Leonard, Edward na Francis, Pascal akamzaa Silvest
Vipi vizazi vingine vya Ndugu wa Mashelle ambavyo havitaoredheshwa hapa.
Napenda kuomba Radhi kwa mababu niliotaja majina Yao hapa. (Ngsameheni hai Kavishe)
HISTORIA YA SHIMBI
UTAWALA WA MANGI MASHELLE SHIMBI
Kunako Karne ya 16 na 17 katika nchi ya wachagga kulikuwa na utawala wake na viongozi wakuu waliitwa Mangi. Katika nchi ya Shimbi nako walikuwa na Mangi wake. Historia ya umangi Shimbi ilianza kwa mzee Makaviha mwana wa pili wa mzee Kitimbiri, na mjukuu wa mzee, M'mamba. Ilikuwa Ni deaturi kurithishana umangi hivyo mzee Makaviha alimrithisha umangi ndugu yake Latemba. Latemba akamwachia umangi mzee Mashaare, Mashaare avivyozeeka akamrithisha umangi mwanae mkubwa Lamasawe, baadaye Lamasawe akamrithisha umangi kwa mwanae mkubwa Matolo, muda mfupi baadaye Lamasawe aliuliwa kwa viata vya kuvizia "kisooki" ambapo wakati huo Mangi Matolo alikuwa katika nchi ya Usseri karibu na Kenya baada ya kupata habari za kuuliwa kwa baba yake alifuka Shimbi Haraka kwa kuwa wauwaji walikuwa bado hawajaondoka wakamuua Mangi Matolo Ni Nia ovu ya kuuamgamiza utawala wa shimbi. Baada ya matukio hayo wananchi wa shimbi wakikubaliana wamwito ndugu wa Lamasawe , mzee Mashelle aliyekuwa uhamishoni huko uruka wa masharti ili aje awe Mangi Shimbi. Mashelle alikubali na akaiongoza Shimbi kwa mafanikio makubwa. Baada ya mzee Mashelle kuzeeka akamchagua mwanae mkubwa Mzee Leina kuwa Mangi wa Shimbi.
Mzee Leina Aondolewa Umangi , Mzee Mashelle arudia Umangi Shimbi.
Ilivyokuwa, Mangi Leina alikuwa na makarani wawili ambao walikuwa Ni Ali masharo na na victory kishindwa ambao walimwibia Mangi Leina shilingi 30 wakala njama na Mangi Selengia wa mkuu. Hata Mangi Leina alivyoenda kukopa fedha misheni mkuu , Mangi Selengia wa uruka wa mkuu alimshawishi padri asimkopeshe Mangi Leina TSH 30. siku ya kukusanya mapato kwa dc wa Moshi fedha ya Mangi Leina ilikuwa pungufu na hivyo kufukuzwa Umangi , Mangi wa uruka wa Usseri Mangi Sengua alipendekeza baba yake Leina mzee Mashelle arudishwe kuwa Mangi wa Shimbi mpaka alipofariki 1893.
Wasaidizi wa Mangi MASHELLE
1. Mashami, mzee Tamira ibara
2. Masho, mzee mwasu, na baadaye marema Moshivira
3. Issia mzee kitara matere
4. Kitirima mzee Manguo mashombo
5. Uua. Mzee ngumia Teng'ute
Shimbi Yatawaliwa na Mangi Selengia wa Mkuu: Baada ya Mangi Mashelle kufariki 25.12.1823 , mwanaye aliyekuwa Mangi, Leina alienda Moshi kudai umangi lakini alikataliwa na hivyo Mangi Selengia wa uruka wa mkuu aliambiwa kutawala Shimbi na hivyo Shimbi ukapoteza hesma ya Umangi rasmi mpaka utawala wa kimangi ulivyokoma baada ya Uhuru. Pamoja na kuwepo kwa Wana wengine wa Mzee Mashelle waliokuwa na uwezo wa kutawala Kama mzee stameza na Karufu njama ilifanywa ili kulinganisha uruka wa Shimbi na Mkuu(kirya)
SHIMBI NDANI YA UTAWALA WA MABAVU
Baada ya Mangi Selengia kupewa utawala wa shimbi alichagua wasaidizi ambao waliitwa wachili. Alimteua Alli ambaye ndiye aliye laghai pesa za Kodi kwa Mangi Leina Hadi kufukuzwa Umangi, Ali lichukiwa na wananchi wa shimbi kutokana na utawala mbaya.
Katika utawala wa Alli alihakikisha hapati upinzani kwa watoto na wajukuu wa mzee Mashelle kwa kuwaandikisha kujiunga na jeshi la mkoloni miongoni mwao Ni Cosma (Kashomba ) ngalu (Stamesa) William Leina n.k
SHIMBI YABADILISHWA JINA
Mchili Ali alibafili jina la Shimbi katika uongozi wake na kuiita Mwateni , Ali aliendelea kutawa Shimbi mpaka macho yake yalipo koma kuona Tena na baadaye wananchi wa shimbi walimchagua mzee Baiseli Marenga kiwango ambaye alitawala vizuri na heshima ya Shimbi ilianza kufufuka Tena kwa Sasa Shimbi inatawaliwa na uongozi wa kawaida wa nchi nzima ya Tanzania chini ya maaafisa watendaji wa kata na vijiji.
![]() |
Uchomaji wa nyama katika kumbukizi ya miaka 100 tangu kufariki kwa Mangi Mashelle iliyofanyika mwaka 2024 |
Umeandikiwa na kudondolewa na
Emanuel Gasper Kisawani Mashelle
0766605392
Rejeleo A.Abeid&J.W.L. Mashelle (1997) Historia Mila na utamaduni. Head secretarial services. Barabara ya sokoine . Arusha-Tanzania