Sunday

NADHARIA YA UDHANAISHI NA UHAKIKI WA DUNIA UWANJA 2A FUJO

0 comments

 


NADHARIA YA UDHANAISHI/UTAMAUSHI (EXISTENTIALISM)

  • DHANA YA UDHANAISHI

Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali una maana ya ;

Kimani Njogu na Rocha Chimera (1999) wanasema  kwamba udhanaishi ni nadharia inayoshughulikia zaidi na “dhana ya maisha “.Swali la kimsingi katika nadharia hii ni maisha ni nini? Wadhanaishi   huchunguza kwa undani nafasi ya mwanadamu ulimwenguni, .pia  wanajishughulisha na uchunguzi kuhusu uhusiano uliopo kati ya binadamu na mungu.

Wamitila K.W (2003)katika kamusi ya fasihi na nadharia amefanunua udhanaishi kama   dhana inayotumia kuelezea maono au mtazamo inayohusiana na hali ya maisha ya binadamu ,nafasi na jukumu la binadamu ulimwenguni ,na uhusiano wake na mungu au kutokuwepo nauhusiano na mungu.

Wanjala Simiyu (2012) katika kitabu kitovu cha fasihi simulizi  udhainishi ni falsafa au mtazamo wa maisha ulio na kitovu chake katika swala kuwa, maisha ni nini na yana maana gani kwa binadamu? Ni kwa njia gani mwanadamu anaweza kuyabadilisha maisha yake yaliyojaa na dhiki, mashaka na huzuni.. 

Kimani Njogu na Wafula L M  katika nadharia za uhakiki wa fasihi (2007) wanasema udhanaishi ni falsafa kuhusu dhana ya maisha. Ni falsafa inayo husiana na utamaushi kutokana na neno “kutamauka”. Kutamauka ni kutokuwa na furaha au kutokuwa na tamaa kwa kuhisi kutokuwa na matumaini katika maisha.

Naye Camus (1984) udhanaishi ni falsafa inayoshugulikia maswala kuhusu maisha; ni mtazamo unaokagua kwa upembuzi hali ya nafasi ya mtu katika ulimwengu anamoishi na pia ni falsafa inayo zungumzia uhusianao uliomo kati ya mtu na mungu na iwapo mtu anapaswa kuamini kuwepo kwa mungu.

Nadharia hii inatusaidia kuhakiki maisha ya mwanadamu  anayeishi katika ulimwengu uliojaa shinda na matatizo mengi ambayo yanayosambambishwa na binadamu mwenyewe. Matatizo anayoyapitia ni kama vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya kidini, jaa na uchumi kuharibika, kukosa kazi, ajali barabarani. Matatizo haya yanafanya mwanadamu kukata tamaa na kushuku iwapo kweli mungu yuko. 

  • WAASISI WA NADHARIA YA UDHANAISHI

Wamekwa kwenye vitengo vitatu

Wanaoamini kuwepo kwa mungu

Soren Kierkegerd ni mwanathiolojia wa kidenimaki aliyekuwapo kati ya mwaka wa 1813 hadi 1855.aliweza kuandika makala mbali mbali hasa;

The concept of dread 

Fear and trembling

The sickness unto death

Wafula R.M na Kimani Njogu (2007) naWamitila. W(2003)

Wasiomini kuwepo kwa mungu

Wanafalsafa wakijerumani wakiongozwa na FRIDRICK NIETZSCHE,MARTIN HEIDEGGER,  GABRIEL MARCEL na KARL JASPERS walitokea katika karne ya ishirini.(Wamitila K.W 2003)

Wasio na uhakika wa kuwepo kwa mungu.

JEAN PAUL SATRE aliyetokea baada ya vita vikuu vya dunia na alikuwa mwanafalsafa wa kifaransa .Kimani Njogu  na Rocha chimera (1999)

HISTORIA FUPI

Udhanaishi unaouhusishwa kwa kiasi kikubwa na mwanathiololojia wa ki-denimaki kwa jina Soren Kierkegaard (1813-1855).katika maandishi yake mbalimbali 

Soren kieregaard (1844)The concept of dread                                                                                                                        Soren kieregaard (1843)Fear and trembling

Soren kieregaard (1849)The sickness unto death

Kieregaard anaeleza kuwa mtu haishi kwa nguvu zake mwenyewe kuna nguvu zinazomtawala ambozo ni za mungu.Binadamu anapoishi hutenda dhambi  na ili apate utulivu wa kiroho inambidi atubu dhambi hizo.Wanaamini kuwepo kwa mungu kwa binadamu wote.Anaeleza kuwa binadamu ni kikaragosi cha nguvu zilizomuumba ni katika kuzicha mtu huyu hupata utulivu wa kiroho .Anaendelea kusema kwamba udhanaishi ni dhana ya hofu pale ambapo binadamu huogopa adhabu kutoka kwa mungukwa hivyo amefunikwana wasiwasi hataki kumkosea mungu.Anasisitiza binadamu ni mtu binafsi (hali ya kujijali).

Binadamu hupata kimbilio kutoka kwa mivutano ya maisha kupitia kwa mungu.Imani hii ilishika nguvu sana kwenye ukristo ,huu ukawa mwanzo wa udhanaishiwa ukristo.(christian existentialism)

Kwa mujibu wa Wamitila .K.W(2003)kamusi ya fasihi ,istilahi na nadharia ,asema kuwa  katika karne ya ishirini ,udhanaishi ulipata msukumo mpya kutoka kwa mwanafalsafa wa kijerumani Friedrich Nietzsche na wengine kama Martin Heidegger ,Gabriel  Marcel na Karl Jaspers.

Nietzche(1927)”joyful wisdom” anadai kuwa mungu amekufa .Tamko hili lake pamoja na misimamo ya wenzake vinakuwa misingi muhimu ya kuzuka kwa udhanaishi wa ukanaji mungu(atheistic existenialism)

Kwa mujibu wa tovuti ,Martin Heidegger,mwanafalsafa wa kijerumani na mwanafunzi wa Husserl aliamini kuwa neno ‘nitakufa’si katika dunia ya ukweli.

Kwa mujibu wa kimani Njogu na Rocha Chimera(1999)wanaelezea kuhusu mwanafalsafa wa kifaransa Jean Paul Satreambaye ndiye mwasisi mkuu wa udhanaishi .Baada ya vita vikuu vya dunia anadai kuwa mtu huzaliwa au hujipata ametumbukia katika ombwe la aina fulani.

Vilevile mtu yuko huru kuishi tu na kukabiliana vilivyo na ulimwengu unaomzunguka .Isitoshe kwa vile binadamu hana uwezo kwa yale anayoyapitia maimivu na mateso anaweza kukata tamaa.Katika mhadhara alioutoaJean Paul Satre, (1946)“Existentialism and Humanilism”alisisitiza kuwa “kuzimu ni za watu wengine”.Hii ni ishara kuwa ana uwezo wa kuchagua na uhuru wa kila mtu anaweza athiri wa watu wengine .alisisitiza pia dini haiwezi kutatua shinda za binadamu .isitoshe ,aliegemea katika suaia la ubinafsiwa mtu.

  • MIHIMILI YA UDHANAISHI

Waandishi mbalimbali wameweza kutoa mihimili ya udhanaishi ,kwa kuwarejelea Wafula .R.M na Kimani Njogu (2007) wao wameainisha mihimili hiyo kama ifuatavyo;

wanatilia mkazo matatizo halisi yanayomsimbu mwanadamu na kwanakwepa imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi.

Hawaamini uwepo wa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu.

Juhudi za mtu binafsi kujisaka au kupambana na maisha huishia katika mauti.

maudhui yanayotajwa na wadhanaishi ni kama vile uhuru wa mtu binafsi ,uwezo wake wa kujifikilia na kujiamlia.

Hujadili hali kaka vile mashaka na uchovu wa mambo mbalimbali yanayotutatiza maishani na jinsi yanavyoathili maisha  ya binadamu.

hujadili maudhui ya ukengeushi (hali ya kukata tamaa aukutokuwa na uhakika)

Mtindo wanaotumia wadhanaishi ni taswira wanaochorea msomaji picha mbalimbali za maisha ya kuteseka anayopitia mwanadamu ulimwenguni.

HITIMISHO

Ufaafu

Nadharia ya udhanaishi inaweza kuhakiki wahusika katika kazi ya fasihi mfano wahusika waliokata tamaa ,walio na matatizo ,walijawa na uchovu.

kuhakiki maudhui katika kazi za fasihi kama vile ukengeushi,ubinafsi,kukata tamaa.

Udhaifu

Nadharia hii haiwezi kuhakiki vitabu ambavyo havijatumiwa nadharia ya udhanaishi.

  • UHAKIKI WANADHARIA YA UDHANAISHI KWA KUZINGATIA RIWAYA YA DUNIA UWANJA WA FUJO-E. KEZILAHABI.

Mwandishi euphace kezilahabi ni miongoni mwa wadhanaishi wa fasihi ya kiswahili .

Kwa kutumia  riwaya ya dunia uwanja wa fujo tunapata Nadharia ya udhanaishi.Ili kuweza kuihakiki tunazingatia mihimili ya nadharia hii ya udhanaishi ;

wadhanaishi wanatilia mkazo matatizo halisi yanayomsubumwanadamu na kukwepa imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi:wahusika katika kitabu hikiwanapitia matatizo mengimfano mamake Kasala anapatikana akijishughulisha na uchawi anafukuzwa kijijini na kupelekwakwenye kisiwa cha wachawi.wanakijiji hawako tayari kuishi na mchawi miongoni mwao.(uk 31-32)


Hawaamini uwepo wa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu.Nyumbani mwa mulele wazee wanajadili imani ya wakristu kuhusu kupokea mwili wa Yesuwanasema waumini hupewa vijidudufulani mdomoni ambazo siku moja walichoma na zikaungua wanashindwa mungu yuko wapi.Pia wanazungumzia waislamu ambao kulingana na imani yao hawali nyamafu wanasema wao hula na wana nguvu kuwashinda.(uk 37).baada ya tumaini kuvamiwa anakosan matumaini na kutamani kufa anajiuliza alichomkosea mungu kwani kama angekuwa hangepitia mateso hayo.(uk.97). 

Juhudi za mtu kujisaka au kupambana na maisha katika maisha huishia katika mauti:Misango aliyefanya kazi kwa Kapinga kama mpishi baada ya kujitahidi na ilisemekana alikufa kwa sababu ya kuchota kisimani alizoea kusomba madebe matano ya maji ili bwana waoge.(uk.12).Babake tumaini alikufa tumaini alipokuwa darasa la tisa ,ilisemekana alikufa kwa sababu ya mawazo mengi;mke wangu alifanya nini alipoenda kuwasalimu wazazi wake nyumbani?au mtoto wangu atarithi nini?hayo ndiyo maswali yaliyokuwa yakimsumbua moyoni badala ya kufikiri afanye nini ili apate kuwa raia mwema.(uk.12).Tumaini anapobadilisha mienendo yake na kufanya kazi kwa bidii,anapambana na utawala wa ujamaa ukiongozwa na mkuuwa wilaya waliotaka kuchukua mashamba ili waweze kujenga kijiji cha ujamaa.Walimshawishi Tumaini ajiunge nao lakini alitaka alipwe walikataa hili na kudai kuwa ardi ni mali ya taifa.Aliapa kuwafunza somo kuwa ujamaa ulikuwa ndoto.Katika mkutano wa pili ,mkuu wa wilaya ya shinyanga alipoamka kuwahutubia watutumaini alimfyatulia risasi na kufa .jambo hili lilimpelekea Tumainikupelekwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata baada ya kuchapwa na mwishowe akapelekwa jela.Baada ya mwaka mmoja kesi ilifanywa ;kesi iliyokuwa fupi,kwani Tumaini alikiri makosa yake akahukumiwa kunyongwa juhudi zake zote ziliishia katika mauti.

maudhui yanayotanjwa na udhanaishi ni kama uhuru wa mtu binafsi,uwezo wake wa kujifikilia na kujiamulia.Anastasia bintiye Mulele anafanya uamuzi wa kibinafsi wa kutoolewa na mzee Tembo.Wanapanga njama wakiwa na Tumainina kuweza kutoroka naye wakati wa ngoma huko Lutare anaolewa na Tumaini (uk.43).Baada ya mkutano kati ya maam Resi,Makoroboi,mwenye baa na Kristina kumalizika bila suluhisho mwafaka ,mama Resi aliamua kumuua Tumaini kwa mikono yake mwenyewe.Alitaka kutimiza hili alipomkuta Tumaini kwake na kujaribu kumndunga kwa kisu.(uk.107).Tumaini anaamua kubadilisha maisha yake anamua kuacha ushenzi wote wa zamani na maisha ya kitoto.anaamua kuishi na Anastasia na kutoingia tena kwenye baa kwa ajili ya pombe na wanawake.pia Tumaini anaamua kufanya kazi yenye uchovuili ale jasho lake aliamua kulima pamba(uk.100).Hadija aliyekuwa mpenziwe Tumaini anamua kuishi maisha ya starehe huku akiwategemea wanaume bila kujali wake wao(uk.83).John ,rafikiye Tumainianamua kuishi maisha ya raha; pombe na wanawake huku akimtegemea Tumaini kwa kila jambo baada ya wawili hawa kutengana kimawazo,walifarakana na Tumaini akamfukuza kwake baada ya kumpata akijaribu kumshawishi bibi yake(uk.105).Baada ya Dennis kugundua uovu wa bibi yakekwamba alihusika na Tumaini alipovamiwa na wanaume wanne wakati walipokuwa na Kristina,alichapwa na akaumizwa vibayahuku akikanywa kazi ya upelelezi  alizirai  na baadaye akatupwa karibu na hospitali ya shingaya.Kutokana na maumivu aliyohisi alitamani kufa”niacheni nife peke yangu”hii ni ishara ya ukengeushi(uk.97).

Hujadili hali kama vile mashaka,uchovu wa mambo mbalimbali yanayotutatiza maishani.Kasala anatatizwa na mamake Mugala ambaye anashiliki uchawi unaomfanya afukuzwe kijijini na kupelekwa kisiwa cha wachawi(uk.32).Leniora anapachikwa mimba na Tumaini jambo linalomtatiza babake.Kapinga alishindwa kutimiza wajibu wake wa ndoa na anatatizika mwanzoni jambo lilowafanya watu  kumdharau kijini kote(uk.10.)Alipofanya kazi yake ya ualimu,alifikili kuhusu mkewe na mambo aliyoyastenda anapoenda kwa wazazi wake na urithi atakaouachia Tumaini. Tumaini alichoshwa na maisha yake ya awali na kubadilisha mienendo yake.


MAREJEREO.

a.Kimani,N na Chimera,R.(1999).Ufundishaji wa fasihi,Nadharia na mbinu .Nairobi ,Jomo kenyatta foundation.

b.Wafula ,R na Kimani,N (2007) Nadharia za uhakiki wa fasihi .Nairobi.Jomo Kenyatta Foundation.

c.Wamitila, K.N (2002)Uhakiki wa fasihi ,misingi na vipengele vyake ,Nairobi :Phoenix publishers ltd.

d.Wamitila,K.N (2003):Kamusi ya fasihi,Istilahi na Nadharia,Nairobi:Focus publications ltd.

No comments:

Post a Comment