Wamiliki wa shule binafsi Mkoa wa Dar es salaam wameiomba serikali kutupia jicho la tatu suala la wanafunzi wanaohitimu masomo kwenye Shule binafsi ili na wao waweze kupata Mikopo kama wengine kwakuwa baadhi yao wanashindwa kuendelea na Elimu ya juu Kwa kukosa fedha
Ujumbe huo umetolewa na viongozi wa ubimiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano Maalum utakaokutanisha wamili wa shule 709 na vyuo 41 pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili kwa kina mambo muhim kuhusu sekta ya Elimu na kuweka mikakati ya pamoja ya Kuboresha zaidi elimu nchini
Katika Mkutano huo utakaofanyika jumatano hii utajadili Masuala muhimu kwenye sekta ya Elimu ikiwemo kuanzisha sakosi ya Wamiliki wa shule binafsi,kuhusu wanafunzi wanaohitimu kwenye Shule binafsi kukosa mikopo ya Elimu ya juu pamoja na kujadil Kwa kina gharama zinazotozwa na Shule binafsi
Pamoja na mambo mengine katika Mkutano huo utachagua viongozi wa wilaya tano za Mkoa wa Dar es salaam ambao watasimakiavmaendeleo ya shule binafsi kwenye wilaya hizo