Sunday

FAIDA KULA MACHUNGWA KIAFYA

0 comments

 


Utangulizi


Chungwa ni tunda la mchungwa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Jina la kisayansi ni Citrus aurantium L. var. sinensis L. au Citrus sinensis (L.) Osbeck. Ni jamii ya matunda aina ya citrus. Jamii hii ya matunda inajumuisha machungwa, machenza, tangerine, clementine n.k.

Tunda lenyewe ni kijani na rangi inabadilika kuelekea njano ikiiva. Pamoja na limau, danzi, balungi na ndimu ni mojawapo kati ya matunda chungwa. na yanapatikana kwa wingi na urahisi sehemu mbalimbali hapa nchini. Machungwa ni matunda maarufu sana sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Asili yake ni katika Asia ya Kusini-Mashariki ambako lilioteshwa na wakulima. Kuna aina mbili yanayotofautiana kwa ladha ama chungu au tamu.

Aina yenye ladha chungu iliwahi kusambaa duniani hivyo jina la Kiswahili limetunza ladha hii hata kama matunda mengi yanayopandwa siku hizi ni aina tamu.

Chungwa tamu lilisambaa kote duniani baada ya Wareno kuchukua machipuko yake na kuyapanda kwanza Ureno baadaye hata Amerika na Afrika kuanzia karne ya 15.

Virutubisho Vinavyoaptikana Katika Machungwa

Machungwa yana mkusanyiko wa virutubisho vingi; Wanga, Protini kwa kiasi kidogo, Vitamini (A, B1, B2, B3, B5, B6, B9, C, E) madini (Kalsiam, Chuma, Zinki, Potasiam) na kambakamba (roughage/fibers).

Machungwa ni chanzo kikubwa na kizuri cha Vitamini C katika mlo. Chungwa la ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke. Hivyo chungwa moja au mawili kwa siku yanaweza kutosheleza mahitaji hayo.

Machungwa yanaweza kuliwa kama tunda zima au kwa kunywa juisi ya machungwa. Juisi ya machungwa huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi mtu napokula chungwa zima.

Kiwango cha asidi
Kama ilivyo kwa jamii ya matunda ya citrus, machungwa nayo huwa na hali ya aside, yenye kiwango cha pH karibu na 2.5 -3, kulingana na umri wake, ukubwa na aina ya chungwa. Japo si kama ilivyo kwa limao, bado machungwa huwa na kiwango cha asidi cha kutosha.

Je Ninapaswa Kula Machungwa Mangapi kwa siku?

Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii hutosheleza mahitaji ya Vitamin C na madini mengine mwilini. Ulaji wa machungwa mengi sana(zaidi ya 50) kwa siku unaweza kusababisha kujaa Vitamini C (hypervitaminosis) ambako ni hatari kwa afya.

Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

FAIDA ZA MACHUNGWA


Huimarisha Kinga ya Mwili
Vitamini C pamoja na madini mengine ikiwemo Zinki, yanatumika kwenye ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga ya mwili.

Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo na Saratani
Machungwa yana kampaundi ziitwazo phytochemicals kama hesperedin, ambazo hulinda mishipa ya damu na kupunguza lehemu (cholesterol) kwenye damu.Vitamini C pia iliyopo kwenye machungwa huondoa sumu za mwili (free radicals), ambazo huchangia kutokea kwa saratani na magonjwa ya moyo zinapokuwa zimelundikana mwilini.

Huimarisha afya ya fizi na mdomo
Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni, hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za kutosha.

Hupunguza lehemu(cholesterol) mwilini
Machungwa yana kambakamba laini (soluble fibers) ambazo huyeyuka kwenye chakula. Hizi husaidia kunyonya mafuta ya lehemu(cholesterol) yaliyo kwenye chakula na kutolewa nje ya mwili kama choo. Hii hupunguza mafuta ya lehemu(cholesterol) kwenye mwili wa mtu.

Kuona vizuri
Machungwa yana Vitamini A ambayao inasaidia kuhakikisha macho yanaona vizuri, pamoja na kamapundi nyingine ambazo hulinda tishu za macho zisiharibiwe na mwanga.

Hupunguza hatari ya kukosa choo/kupata choo kigumu (constipation)
Machungwa hasa pale mtu anapokula chungwa zima, humpatia kambakamba ambazo husaidia kulainisha chakula kwenye utumbo na kukifanya choo kuwa laini.

Huimarisha afya ya ngozi
Madini yaliyopo kwenye machungwa pamoja na Vitamini A na C husaidia kujenga na kuondoa seli za ngozi zilizokufa.

MARADHI 13 YANAYOWEZA KUEPUKIKA KWA ULAJI WA MACHUNGWA

1. UKOSEFU WA CHOO

Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

2. UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya flavonoids, phytonutrients vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na hesperidin vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.

5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

6. AFYA YA NGOZI
Anti oxidants iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi isizeeke.

7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya folic acid inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.

9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.

11. VIDONDA VYA TUMBO
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.

12. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.

13. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.

No comments:

Post a Comment