Mashindano ya mpira wa miguu ya Mkenda Cup yamezinduliwa rasmi wilaya Rombo,kwa mara ya kwanza yakishirikisha timu 91 kutoka kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Mashindano
hayo ambayo yamezinduliwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro
Patrick Boisafi katika uwanja wa Sabasaba na yamedhaminiwa na Mbunge wa
jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia
Prof.Adolf Mkenda na Wadau.
Kwa
mujibu wa Prof.Mkenda mshindi wa kwanza wa michuano hiyo ataibuka na
kitita cha shilingi milioni tatu pamoja na ziara ya kutembelea Makao
Makuu ya nchi,mshindi wa pili atapata shilingi milioni 2 na wa tatu
atapata milioni moja.
Katika
mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya Rongai Fc
waliwafunga Motamburu Kitendeni Fc kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare
ya nao 1-1 katika muda wa dakika tisini na kufanikiwa kupata zawadi ya
mbuzi mnyama.