Polisi
wa Kaunti ya Murang’a nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mwenye umri
wa miaka 41 kwa kosa la kumuua mtoto wake wa kike (16) anayesoma form
one baada ya kurudi nyumbani kwake na kumkuta mtoto wake huyo akiwa na
mpenzi wake kitandani wakifanya mapenzi ndani ya nyumba ya baba yake.
Polisi
wamesema Baba huyo alimpiga mtoto wake huyo aliyekuwa akisoma katika
Shule ya Sekondari Sabasaba hadi akafariki na kutokana na hofu ya
kukamatwa aliamua kuutupa mwili wa mtoto wake ndani ya karavati
(Culvert) lililopo Barabara ya Kenol – Sabasaba umbali wa mita chache
kutoka nyumbani kwake ambapo mwili huo ulionekana na Wapita njia.
Polisi
wanasema walikuta damu kwenye suruali ya mwanaume huyo wakati wa
upekuzi na walipombana akakiri kumuu mwanae huku akisema mpenzi wa mtoto
wake waliyekuwa kitandani na mtoto wake alifanikiwa kukimbia.