Mwanamume mmoja nchini Kenya ambaye jina lake halikufahamika anadaiwa kumuuwa kwa kumpiga na jiwe kichwani mwanaume mwenzake David Maina (35), wakati wakimgombania mwanamke aitwae Miriam Njeri mwenye umri wa miaka 27.
Katika kisa hicho, Miriam akiwa ameandamana na Maina walikuwa wakirudi nyumbani kwake majira ya saa 1:00 asubuhi wakati wakitokea kwenye maeneo ya burudani, ambapo mara baada ya kufika nyumbani walimkuta mwanaume mwingine akimngoja Miriam na ndipo ugomvi ulipoanza kati ya wanaume hao wawili.
Afisa Mpelelezi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI) Kasarani, Vincent Kipkorir, alisema mtuhumiwa alikimbia baada ya kugundua kama amesababisha kifo cha mwanaume mwenzake na Miriam anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kasarani ili kusaidia katika uchunguzi na zoezi la kumtafuta muuaji linaendelea.