Wednesday

Rais Samia Ataja Mikoa Yenye Wagonjwa wa Corona

0 comments



RAIS Samia Suluhu Hassan amesema wimbi la tatu la ugonjwa wa corona limeshaingia nchini na tayari kuna wagonjwa katika mikoa kadhaa mikubwa huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huo ili usiangamize maisha yao.

 

Rais Samia amesema hayo leo Julai 7, 2021 wakati aliposimama Kibaigwa kuzungumza na wananchi wa eneo hilo akiwa safarini kuelekea Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.

 

“Nimelipokea suala la maegesho ya malori hapa Kibaigwa, tutakaa Serikali na halmashauri kuona namna ya kulitatua ili malori yapaki pembeni, magari yapite na biashara ziweze kuendelea.

 

“Naelewa kwamba umeme wa Kibaigwa ni ule unaotoka Morogoro, kwa hiyo unafika hapa ukiwa umepoa, cha kufanya ni kujenga kituo cha kupozea umeme hapa Kibaigwa ili umeme upatikane kwa uhakika. Nitamuomba Waziri mwenye dhamana aje alifanyie kazi na linawezekana.”

“Ninaowaona wameziba midomo na pua ni kidogo sana, tuchukue tahadhari zote dhidi ya maradhi ya corona, wimbi la tatu la ugonjwa huu tayari lipo nchini wala si jambo la kuficha na tunao wagonjwa Dar, Mwanza, Arusha na kwingine hata Dodoma.

 

“Tuchukue tahadhari kuhusu janga la corona lisije likatupukutisha kama nchi nyingine huko, kwa sababu likianza kuangusha linapukutisha tu halina kusimama.

 

“Niwaombe wafanyabiashara wote fuateni sheria na kanuni zinazowekwa na halmashauri, sisi Serikali tunajitahidi sana kuwabeba, sisi ni marafiki sana wa wafanyabiashara, tunafanya kila tunaloweza ili maisha yenu yaende vizuri.

 

“Tuweke ulinzi na usalama katika maeneo yetu, kila mmoja awe mlinzi wa wenziwe, aangalie kwenye eneo lake kunatokea nini. Anaeingia na mambo yasiyofaa mumseme mara moja, tuweke sawa, mambo yaendelee.”

 

“Kwenye migogoro ya ardhi tutaleta Waziri mwenye dhamana au naibu wake ili waje wamalize matatizo haya. hatutaki jimbo la Mhe Spika, Job Ndugai kuwe na migogoro ya ardhi,” amesema Rais Samia Suluh akiwa Kibaigwa.

 

No comments:

Post a Comment