![]() |
fasihi ya kiswahili |
Kumekuwepo na mijadala juu ya niipi iitwe fasihi ya kiswahili miongoni mwa kazi mbalimbali za kifasihi zinazotokna na uswahili na waswahili. Kabla ya kujadili jambo hili embu tutalii kidogo kuhusu waswahili, uswahili na kiswahili, Unapojadili kuhusu uswahili na kiswahili unaingia pia katika mjadala mrefu wa chimbuko na asili ya lugha ya kiswahili, lakini kwa mujibu wa andiko hili nisingependa kukuingiza katika mjadala huo. ila cha muhimu unachopaswa kufahamu nikuwa zipo nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko na asili ya lugha ya kiswahili. Sii vyema kutalii sana katika asili ya kiswahili lakini ujue pia sio rahisi kusema mswahili ni nani? je ni wale wanaozungumza lugha ya kiswahili? hata wachina wanazungumza kiswahili nao ni waswahili? je wazungumzaji wanaojifunza lugha ya kiswahili kama lugha yao ya pili/ watu wa bara nao ni waswahili? kama sivyo tutumie kigezo cha utamaduni, je wale wanaofuata mila na dasturi za kiswahili ndio waswahili? hata ikiwa hawajui kiswahili? kama sivyo basi tutumie kigezo cha Kigeografia
Je waswahili ni watu wa pwani ya Afrika mashariki? je wanaozungumza kiswahili walio katika maeneo mengine sio waswahili hata ikiwa wanafuata mila na desturi za kiswahili? vipi kuhusu wazungumzaji wa lahaja za kiswahili waliuopo congo na kilugwana cha kule Madagaska? mpaka hapa nadhani umepata picha utata ulipo katika kueleza mswahili ni nani haswa ndivyo ilivyo katika kueleza dhana ya
Fasihi ya kiswahili.
Maswali ya kujiuliza
je kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lugha ya kiswahili ndio fasihi ya kiswahili? vipi kuhusu riwaya na tamtiliya zilizoandikwa kwa lugha za kigeni kisha kufasiliwa kwa lugha ya kiswahili?
Je nizile zilizoandikwa na waswahili? vipi kuhusu waswahili wanaoandika kazi zao kwa lugha za kigeni au makabila mengine lakini zenye maudhui ya kiswahili? je tuziweke katika kundi lipi?
Nadhani nimuhimu tuweke sifa katika kuiainisha fasihi ya kiswahili kama ifuatavyo
- Ni lazima iwahusu waswahili yani iwe imeandikwa kwaajili yao
- Yenye maudhui ya mila na desturi za waswahili
- iandikwe kwa kiswahili