Thursday

Changanua muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina, huku ukionesha mora.

0 comments

 SWALI: Changanua muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina, onesha mora.


 

Muundo wa Ndani wa Silabi za Kiswahili kwa Kutumia Mkabala wa Mgawanyo wa Kiuwili Unaozingatia Mwanzo na Kina, kwa kuonesha Mora.

Utangulizi

Swali hili limegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo ni utangulizi, kiini, hitimisho na marejeleo. Sehemu ya utangulizi ni maelezo kuhusiana na mgawanyiko wa kazi, fasili ya silabi na muundo wa ndani wa silabi. Sehemu ya kiini ni uchanganuzi wa muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili kwa kuzingatia mwanzo na kina pamoja na kuonesha mora. Sehemu ya hitimisho ni maoni ya jumla kuhusiana na kazi kisha vyanzo mbalimbali vilivyosheheneza kazi hii vimewekwa katika sehemu ya nne.

Dhana ya Silabi

Dhana ya silabi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitofautiana na kufanana katika fasili zao. Mathalani, Crystal (2004) anaeleza kwamba silabi ni sauti moja au zaidi inayowakilisha kifungu kimoja cha sauti katika lugha, sawasawa na Massamba na wenzake (2004) ambapo wao wanaona silabi ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Tofauti na Crystal na Massamba, Feng (2003) anaona kwamba silabi ni mpangilio wa fungu la sauti za kutamkwa. Pamoja na ubora wa fasili hii, bado haijitoshelezi kwani si wakati wote silabi lazima iundwe na fungu la sauti (konsonanti+irabu) bali silabi huweza pia kuundwa na irabu peke yake, kwa mfano; neno ‘anaimba’ ($a$$na$$i$$mba$) lina irabu a na i ambazo zimesimama kama silabi.

Aidha, maelezo ya Pike (1943) yanaoesha kwamba vipo vigezo mbalimbali vilivyotumika katika kuifasili dhana ya silabi kama vile; fonimu kuwa na nguvu zaidi, msikiko n.k, inaelekea wataalamu hapo juu wameifasili dhana ya silabi kwa kujikita zaidi katika kigezo cha nguvu msikiko kwani ili kuweza kubaini silabi katika maneno ni sharti uzingatie nguvu msikiko wa sauti katika neno hilo.




Hata hivyo, Togeby (1973) katika kuelezea silabi anatoa muhtasari wa fasili zilizotolewa na wanazuoni mbalimbali kuhusiana na silabi katika aina kuu tatu kama ifuatavyo;

Fasili ya kiutendaji 

Ni fasili ambayo kwayo silabi inabainishwa kwa mujibu wa kazi zinazofanywa nayo. Sentensi zinagawanywa katika mafungu ya silabi na mafungu ya silabi yanagawanywa katika silabi zake (silabi ni kijenzi cha neno). 

Mfano; a.     Mtoto anaimba 

$m$$to$$to$  $a$$na$$i$$mba$

Katika mfano (a) hapo juu, sentensi imeundwa na mafungu mawili ya silabi kisha mafungu hayo ya silabi yamegawanywa katika silabi zake kama ilivyooneshwa katika (b). Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kwamba silabi ni kijenzi cha neno ambacho kikiondolewa katika neno hilo huondoa maana ya awali ya neno hilo. 

Fasili ya kiuchanganuzi

Ni ile inayochukulia silabi kuwa darajia ya mwisho ya kanuni za mjengosauti za lugha. Hivyo, silabi ni kipengele kidogo kabisa kinachoweza kujenga sentensi. Ubora wa fasili hii, ni kwamba silabi za lugha nyingi huchanganuliwa kiundani. Mathalani pamoja na zile ambazo maneno yake huundwa na silabi pasi na kubainishwa mkazo mkazo wake. Kwa mfano lugha ya Kifaransa neno ‘eux’ (wao)

Fasili ya kisanisi

Katika fasili hii, silabi huweza kufasiliwa kwa kuzingatia viambajengo vyake ambavyo ni mkazo na kiini cha silabi. Hivyo, silabi huweza kugawanywa katika makundi ya konsonanti na irabu, yaani silabi huweza kuundwa na konsonanti na irabu au na irabu peke yake.

Baada ya kutalii dhana ya silabi na jinsi ilivyofasiliwa na wataalamu mbalimbali,  tutatumia fasili ya kiuchanganuzi katika kushughulikia  muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa sababu fasili hii inaonekana ni mwafaka kwa lugha zenye mkazo na zile zisizo na mkazo. Aidha, kabla ya uchanganuzi wa muundo wa ndani wa silabi sehemu ifuatayo inaeleza kwa ufupi dhana ya muundo wa ndani wa silabi.

 Dhana ya Muundo wa Ndani wa Silabi 

Muundo wa ndani wa silabi ni sifa za silabi zisizobainika waziwazi katika uchanganuzi. Muundo wa ndani wa silabi unaweza kutuonesha baadhi ya viambajengo ambavyo huwa havidhihiriki katika maandishi bali hudhihrika katika matamshi. Kwa mfano uwepo wa wakaa ama mfupi au mrefu ndani ya silabi.

2.0 Uchanganuzi wa Muundo wa Ndani wa Silabi za Kiswahili kwa Kutumia Mkabala wa Mgawanyo wa Kiuwili Unaozingatia Mwanzo na Kina, kwa Kuonesha Mora.

Katika kuchanganua muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina kwa kuonesha mora, tutaanza kuchanganua muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa kimora ili kujenga msingi wa uchanganuzi wa mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina. Aidha, katika uchanganuzi tutatumia mifano mbalimbali kutoka katika lugha ya Kiswahili.

2.1 Uchanganuzi wa Ndani wa Silabi kwa Mkabala wa Kimora (µ)

Mora ni kipimo cha wakaa ambacho urefu wake ni sawa na silabi fupi. Silabi fupi ni zile ambazo zina wakaa mfupi na huwa na thamani ya mora moja ilhali silabi ndefu zinabainika kwa wakaa wake kuwa mrefu na mora hugawanyika katika matawi mawili kiupimaji. Kanuni ya mora katika lugha ya Kiswahili ni;

    σ (K20  µ(µ) K0  (silabi inaweza ama kutokuundwa na konsonanti yoyote au kuundwa na konsonanti zisizozidi mbili zikifuatiwa na irabu ambazo haziwezi kuishia na konsonati)

Hivyo, mifano ifuatayo inadhihirisha maelezelo haya

Nyooka - / ɳͻͻka/  (kitendo cha kukaka katika hali inayofaa)

    σ  σ       σ 

          K µ  µ   K µ 

           ɳ ͻ  ͻ    k  a

Katika data (a), neno “nyooka” lina silabi 3 yaani $ɳͻ$$ͻ$$ka$, kila silabi zote zina kiwango sawa cha wakaa. Hivyo zina mora sawa. Kinachotutufanya kuona kwamba silabi hizi zina kiwango sawa ni ile nguvu msikiko ya silabi hizi pamoja na utamkaji wake.

Nyoka - /ɳͻ:ka/  (mnyama anayetambaa chini na hana miguu)

      σ         σ 

          K µ  µ   K µ 

          ɳ    ͻ      k a

katika data (b), neno “nyoka” lina silabi 2 yaani $ɳ$$ͻ$$ka$, kila silabi imeoneshwa urefu wake wa wakaa kwa mora, ambapo wakaa wa silabi ya kwanza $ɳͻ$ ni mrefu kuliko silabi ya pili $ka$. Kutokana na sababu hiyo kipimo cha mora kimegawanyika mara mbili kuelekea silabi hiyo. Hii inatokana na nguvu msikiko yake kuwa juu kuzidi silabi ya pili.

Hivyo, ni dhahiri kwamba katika mkabala huu (wa kimora) silabi zenye wakaa mfupi zinawakilishwa kwa mora moja inayojitegemea ilhali silabi zenye wakaa mrefu hukigawanya kipimo cha mora kama ilivyooneshwa katika mifano hapo juu. Hivyo, katika mkabala huu silabi huchanganuliwa kwa kuangalia wakaa katika utamkaji wake na hii ina maana kwamba muundo wa silabi hutegemea wakaa katika silabi hizo.

Baada ya kuchanganua silabi kwa mkabala wa kimora, sehemu ifuatayo ni uchanganuzi wa muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina, kwa kuonesha mora. Aidha, katika uchanganuzi tutatumia mifano mbalimbali ya lugha ya Kiswahili ili kuweza kuonesha namna muundo wa ndani wa silabi unavyochanganuliwa kama ifuatavyo.





Kanuni ya mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina ni,

(σ(mwanzo na kina)

Kina(kiini + koda

Kaka /ka:ka/ (ndugu wa kiume)


                                                            

                                               ∑                                      

                               σ                 σ

             mwanzo           kina      mwanzo                kina

                            kiini         koda                   kiini           koda

                       µ            µ                                µ  

                  k           a              0      k               a               0

Katika data (i) neno “kaka” imeundwa na silabi 2 yaani $ka$$ka$, silabi ya kwanza ina wakaa mrefu zaidi ya silabi ya pili. Hivyo, silabi yenye wakaa mrefu imewakilishwa na mora inayogawanyika katika sehemu mbili kuelekea irabu ya silabi husika ilhali silabi ya pili imewakilishwa kwa moja moja isiyogawanyika. 





mana( /mana/ (chakula)



                                              ∑                                      

                               σ                 σ

             mwanzo           kina      mwanzo                kina

                            kiini         koda                   kiini           koda

                               µ                                      µ  

                  m          a              0      n               a                0

Katika data (ii) neno “mana” limeundwa na silabi 2 yaani $ma$$na$, silabi ya kwanza na ya pili zote zina wakaa unaolingana. Jambo linalofanya kuziona silabi hizi ziko sawa ni nguvumsikiko katika utamkaji. Hivyo, kipimo chake cha mora kinalingana. 

cheka( /ʦɜ:ka/ (kitendo cha kufurahi)

                                     

                                               ∑                                      

                               σ                 σ

             mwanzo           kina      mwanzo                kina

                             kiini         koda                   kiini           koda

                       µ            µ                                µ  

                  ʦ          ɛ               0       k              a               0

Katika data (iii) neno “cheka” limeundwa na silabi 2 yaani $che$$ka$, silabi ya kwanza ina wakaa mrefu zaidi ya ile ya pili kwa sababu zinatofautiana katika nguvumsikiko yake, hivyo, uchanganuzi wa silabi ya kwanza umewakilishwa kwa mora ambayo inagawanyika mara mbili kuelekea kwenye silabi. 

mbuzi (mnyama) (/ᶆbu:zi/

                                     

                                               ∑                                      

                               σ                 σ

             mwanzo           kina      mwanzo                kina

                            kiini         koda                   kiini           koda

                       µ            µ                                µ  

        m           b       u              0     z                i                0

Katika data (iv) neno “mbuzi” limeundwa na silabi 2 yaani $mbu$$zi$, silabi ya kwanza ina wakaa mrefu zaidi ya ile ya pili kwa sababu zinatofautiana katika nguvumsikiko na katika utamkaji wake. Hivyo, uchanganuzi wa silabi ya kwanza umewakilishwa kwa mora ambayo inagawanyika mara mbili kuelekea kwenye irabu ilihali silabi ya pili imewakilishwa kwa kipimo cha kawaida cha mora.






anakula /anaku:la/

                                       

                       ∑                                                ∑                                  

       σ                           σ                  σ                                   σ               

mwanzo    kina      mwanzo         kina   mwanzo    kina      mwanzo   kina  

          kiini      koda             kiini        koda         kiini      koda       kiini     koda

            µ                                 µ                    µ        µ                     µ

    φ   a            0         n         a          0     k     u            0    l        a        0

Katika data (v) neno “anakula” limeundwa na silabi 4 yaani $a$$na$$ku$$la$, silabi ya pili kutoka mwisho yaani $ku$ ina wakaa mrefu zaidi kuliko silabi zingingine kwa sababu ina nguvumsikiko yake ni kubwa zaidi katika utamkaji wake. Hivyo, uchanganuzi wa silabi ya pili kutoka mwisho umewakilishwa kwa mora ambayo inagawanyika mara mbili kuelekea kwenye irabu ilihali silabi nyingine zimewakilishwa kwa kipimo cha kawaida cha mora.

4.0 Hitimisho

Uchanganuzi wa muundo wa ndani wa silabi za Kiswahili kwa kutumia mkabala wa mgawanyo wa kiuwili unaozingatia mwanzo na kina, unaonekana ni bora zaidi kulinganisha na mikabala mingine kwani unatupa picha ya ndani zaidi ya silabi kulinganisha mikabala mingine mathalani ule wa bapa ambapo wenyewe umejikita katika madai kwamba katika uchanganuzi wa silabi hakuna viambajengo vidogo bali kinachofuata ni vipandesauti vyenyewe, jambo ambalo linafanya kutokuutambua muundo wa ndani wa silabi.

 




MAREJELEO

Masamba, D. P. B. (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu: FOKISA. Dar es  

                    Salaam: TUKI.

_______________ (2010) Phonological Theory; history and Development. Dar es 

Salaam:TUKI.

Pike, K. (1948) Tone Languages, Ann Arbor: University of Michigan Press.

Shengli, F. (2003). A Prosodic Grammar of Chinese: University of Kansas.

Togeby, k.(1951) “Structure Imanente de Langue Francise” in Travauxdu la

 Linguiistique de Copenhague.  

No comments:

Post a Comment