Thamani ya hisa zake zimeshuka kwa asilimia 0.86 na kuwafanya wawekezaji wake wapoteze Sh10 kwa kila hisa moja.- Kampuni nyingine iliyopoteza leo ni ya habari ya NMG ambayo thamani ya hisa zake imeshuka kwa asilimia 2.25.
Dar es Salaam. Wawekezaji wa kampuni mbili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwemo benki ya KCB leo watalala na maumivu baada ya thamani ya hisa za kampuni hizo kushuka kwa viwango tofauti ikilinganishwa na ijumaa ya Desemba 6, 2019.
Wiki za DSE hujumuisha siku za kazi pekee yaani Jumatatu hadi Ijumaa.
Ripoti ya soko ya siku ya DSE ya Desemba 10 inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa jioni ya leo kampuni ya habari ya NMG ndiyo iliyofanya vibaya zaidi baada ya thamani ya hisa zake kushuka kwa asilimia 2.25 ambapo wawekezaji wake wamepoteza Sh20 kwa kila hisa moja.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa thamani ya hisa moja ya NMG ilikuwa Sh870 kutoka Sh890 iliyorekodiwa ijumaa.
Kampuni nyingine ambayo thamani ya hisa zake imeshuka ni benki ya KCB ambayo thamani ya hisa zake zimeshuka kwa asilimia 0.86 na kuwafanya wawekezaji wake wapoteze Sh10 kwa kila hisa moja.