Maana ya SARUFI
Kulingana na Mdee (1986), sarufi ni jina la tawi la masomo ambalo huchunguza kawaida au dhahania sisa za lugha na sharia ambazo hutawala mchanganyiko wao, marejeleo na ufafanuzi.
Sifa hizi ni kama vile sauiti, mofimu,maneno na sentensi. Mdee (1986) anaendelea kusema kuwa sarufi ni mfumo wa kanunu za lugha zinazoonyesha uwezo wa lugha alionao mzawa wa lugha hiyo.
Vitengo vinavyounda sarufi ya lugha ni:
Fonolojia
Mofolojia
Sintaksia
Semantiki
Japo kwa muhtasari, hebu tuangazie vitengo hivi vya safuri.
Fonolojia.
Wanaisimu wengi wametoa maoni kuhusu fonolojia. Kwa mfano, Richard S Mgullu (1999) anaanza kwa kunukuu maelezo yaliyotolewa na Fudge (1973) ambaye anasema kuwa fonolojia ni kiwango kimojawapo cha lugha kilicho na vipashio vidogo Zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya lugha.vipashio vya kifonolojia ni fonimu na alofoni zake.
Mugullu anaendelea kunukuu maelezo ya TUKI (1990) kuwa fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani.
Kutokana na maelezo haya ni wazi kuwa fonolojia huzichunguza sauti zilizo katika mfumo mmoja yaani lugha mahususi na pili, kuwa fonolojia ya lugha huwa na fonimu na alofoni zake.
Mofolojia.
Kulingana na Mathews (1974) akinukuliwa na Mgullu (1999), anasema kuwa mofolojia ni tawi la taaluma ya isimu ambalo huchunguza maumbo ya maneno na hususani maumbo ya mofimu. Nao TUKI (1990) wanasema mofoloji ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno na aina zake.
Kutokana na maelezo haya basi ni wazi kuwa mofolojia ni tawi la isimu linaloshughulika na maumbo ya ndani ya maneno. Kipengele cha msingi kinachochunguzwa katika mofolojia ni mofimu.
Sintaksia.
Sintaksia nayo ni uchunguzi wa sheria ama kaida na njia ambazo sentensi hutungwa katika lugha mahususi. Huangalia utunzi wa sentensi za lugha fuklani. Sintaksia hushughulika na kchanganya maneno kwa vikundi, vishazi/virai na sentensi.
Semantiki
Semantiki ni kipengele ch sarufi kinachotalii maana za maneno, vishazi na sentensi. Manano na mofimu huwa n maana katika lughu yoyote ile ulimwenguni. Katika uchanganuzi wa maneno, neno huangaliwa lina maana gani lilivyojitokeza bali si vile mzungumzaji akavyo.
Kwa hivyo ili sarufi ya lugha iwe sahihi lazima mzungumzaji azingatie matamshifonolojia , maneno yanavyoundwa(mofojia), mpangilio wa maneno hayo katika sentensi(sintaksia) ili kuleta maana ( semantiki).
Mzizi
Hii ni dhana ambayo imeandikiwa na wanaisimu wengi. Kwanza, Richaed Mgullu (1999) akitao fasili ya Richard na wengine (1985) kuwa mzizi wa neno ni mofu ambayo ni sehemu muhimu zaidi ya neno, na ambayo katika lugha nyingi inaweza kukaa pekee yake kama neno kamili. Mizizi inaweza kuwekwa pamoja kuunda neno.
Anaendelea kutoa fasili ya Hartman (1985) kwa kusema kuwa mzizi ni mofu fulani kaika neno iliyo na taarifa ya kileksia iliyo muhimu zaidi katika neno hilo. Mzizi ni tofauti na viambishi ambavyo hutumiwa kunyambua maneno na wakati wa kuunda neno.
Katika fasili hizi mbili za Richard Mgullu, anajaribu kuwakosoa waandishi hawa ambao awali walitumia neno mofimu mahali pa mofu kurejelea umbo fulani la neno.
TUKI nao wanasema kuwa mzizi ni sehemu ya neno ambayo haibadiliki, kwa mfano, -pig- ni mzizi katia maneno pigana, pigwa,kupigwa, n.k.
Kulingana na maelezo ya Y.M Kihore et al (2004) akimnukuu David Crystal katika kamusi yake ya Dictionary Of Linquistcs And Phonetics(1987:267) anasema “mzizi ni umbo-msingi la neno ambalo haliwezi kuchanganuliwa tena katika sehemu nyingine ndogo bila kupoteza (uamilifu) na utambuzi wake (wa kisemantiki).”
ANA ZA MIZIZI
Y.M Kohore na wengine, anasema kuna aina mbili za mizizi katika lugha nyingi za ulimwengu.
1. miziz funge
Hii ni miziz ambayo haiwezi kujitegemea yenyewe,yaani haiwezi kusimama pekee yke kama neon.
Tazama mifano:
Lala lal +a
Lalia lal ++a
Laliwa lal+i+w+a
Laliana lal+i+an+a
Umbo lililopigwa mstari (mzizi) ndilo umbo la msingi kwa maana kuwa ndilo mofimu iliyo ya kiini cha maana za maneno yote yaliyoorodheswa katika mfano wa kwanza. Maumbo hayo yote yanafanana katika maana yake ya msingi, yaani “kitendo cha kulala.” Kutokana na umuhimu wake kimaana umbo hilo la lal ndilo mzizi wa maneno yote hayo.
Jambo linalijitokeza ni kuwa umbo hili la msingi lina tabia moja kuu, nalo ni ile ya kutobadilika katika maneno yote yanayohusiana nalo.
Pia mzizi huu hauwezi kusimama peke yake kama neon sharti uandamane na mambo mengine.
Mzizi huru
Huu ni mzizi ambao unaweza kusimama peke yake kama neon,lakini kama ilivyo katika mizizi-funge,umbo la huu mzizi nalo haliwezi kuchanganuliwa katika sehemu ndogo bila kuathiri ile maana yake ya msingi.Tazama mifano:
2. jembe godoro kumi gani dogo
Jina genge gamba bega jeusi gereza
Hapa kila neno lililotolewa linaleta maana kamili yaani linaweza kijitegemea lenyewe kimaana.
Viambishi
Viambishi ni mofimu zinazoambatanishwa kwenye mzizi wa neno ili kuwakilisha hali au dhana mbalimbali zinazofungamana na neno pamoja na mofimu hizo.
Katika Kiswahili viambishi hutokea tu mwanzoni na mwishoni mwa mzizi.Huu uambatanishaji wa viambishi kwa mzizi huitwa uambishaji.
Kwa mfano:
Ji-we
m-toto
ch-uma
mi-ti
vi-gogo
UAINISHAJI WA VIAMBISHI
Viambishi huweza kuainishwa kwa njia mbili kuu tofauti. Kwanza kuna uainishaji kwa kufuata maumbo na nafasi vinamotokea. Pili, ni kuainisha kwa kuzingatia uamilifu wake kama vipengele vya kisarufi.
Uainishaji kimaumbo.
Hapa hatujishughulishi sana na dhana zinazowakilishwa navyo. Lamuhimu hapa huwa ni kuona ni vipi viambishi hivyo vilivyojengeka na vinachukua nafasi gani katitka neno.
Viambishi awali
Hivi ni viambishi vinavyotokea mwanzoni mwa mzizi-funge.Neno “awali” maana yake ni 9“mwanzo” au “mwanzoni”. Hivyo viambishi awali maana yake ni “viambishi vya mwanzo”.
Tazama mifano:
M+zee
Mu+ungwan+a
Tu+li+po+wa+on+a
Mw+a+limu
A+ta+kul+a
Viambishi tamati.
Hivi hutokea mwishoni mwa mzizi,yaani viliyoko kulia kwa mzizi ndivyo vijulijanvyo kama viambishi tamati.
Tazama mifano:
Chek-ek-e-a kimbi-li-
Pig-an-ish-a
Uaishaji kiuamilifu
Katika lugha ya Kiswahili kuna viambishi ingi vyenye maumbo mbalimbali ambavyo kila kimoja kina kazi ya kisarufi, kazi hizi hutegemea mahili kiambishi kilipo katika umbo la neno na vilevile aina ya neno kimojitokeza. Baadhi ya kazi ya viambishi ni kama vile upatanisho wa kisaruri, unyambulishaji, uwakilishi njeo,uwakilishi wa hali na ukanushi.
Mtazamo huu wa viambishi huwa unafunagana Zaidi na aina za maneno vinamojitokeza. Kutokana na hali hiyo katika maelezo yafuatayo Kihore na wenzake wanajadili kazi za vipashio hivi kulingana na maneno husika. Aian za maneno nza ni nomino na vitenzi.
Uamilifu wa viambishi katika nomino
Kwa jumla kazi za viambishi katika nomino ni kuwakilisha ngeli, idadi na upatanisho wa kisarufi. Hujitokeza hivi:
Viambishi vya ngeli na idadi.
Ngeli na idadi katika Kiswahili huwakiliswa na viambishi kama inavyoonekana hapa:
Umoja wingi
M+tu wa+tu
Ki+tu vi+tu
Ji+cho ma+cho
N+nguo n+guo
Katika mifano hii, maumbo yaliyo upande wa kushoto yana wakilisha umoja na yaliyo kulia yana wakilisha wingi. Viambishi hivyo vina uamilifu wa aina mbili: vinawakilisha idadi,(umoja na wingi) na makundi ya nomino (yaani ngeli za nomino).
Viambishi vya upatanisho wa kisarufi
Viambishi vya nomino vilivyoonyeshwa katika mfano wa (ai) vinahusiana na vingine vinavyojitokeza katika nafasi za mwanzo katika aina nyingine za maneno katika sentesi. Viambishi hivyo inafanya kazi inyojulikana kama upatanisho wa kisarufi.
Upatanisho wa kisarufi ni kule kukubaliana kunakojitokeza baina ya nomino kiima na kitenzi au kivumishi ambapo kunakuwa na kiwakiishi cha nomino kiima katika kitenzi au kivumishi.
Tazama:
Ki+su ki+moja ki+me+potea vi+su vi+wili vi+me+potea
M+toto m+moja a+li+rudi. Wa+toto wa+wili wa+li+rudi.
Ji+we moja li+me+baki. Ma+we ma+wili ya+me+baki.
Hata hivyo, Joash Johannes Gambarage (2007), anapinga maelezo ya Mohamed kuhusu mzizi na kiini yanayoleta mkanganyiko kuhusu dhana hizi mbili. Kulingana na Mohamed (1963:56), akinukuliwa na Gambarage, mzzizi ni kiini cha kitenzi kinachobeba maana ya kitendo.
Kulingana na maelezo haya, kwa ufafanuzi wake Gambarage, yanahitilifiana na maelezo ya Mohamed ya baadaye ya mwaka wa (1963:57). Wakati huu, Mohamed anataja aina mbili za mizizi: (i) mzizi asilia: huu ni ule unaobaki baada ya viambishi vyotekuwa vimeondolewa. Kwa mfano, som- katika soma na chez- katika cheza: (ii) mzizi wa mnyambuliko ambao unajenwa na mzizi asilia na pamoja na viambishi tamati vijenzi. Kwa mfano, som-a na chez-a. Ukinzani unajitokeza pale Mohamed anaposema kuwa mzizi hubaki baada ya viambishi vyote kuwa vimeondolewana wakati huo huo anasema mzizi una viambishi vya kauli. Gambarage anasema ni vizuri ikumbukwa kuwa dhana ya uambishajihaihusu maneno yote ya lugha kwani kuna baadhi ya mizizi ya maneno huru qkama kuku, mama,lakini nasamaki, huwa haiambishwi.
Ni wazi kutokana na mifano hii hapa juu kuwa mzizi wa neno huru hauwezi kuchanganuliwa Zaidi kwani viambishi vya aina yoyote haviwezi kuwa sehemu ya mzizi huru. Hivyo basi ni muhimu kutaja kuwa Gambarage anasisitiza kuwa mzizi ni tofauti na shina la neno ambalo ni muungano wa mzizi na viambishi kama vile vya kauli au vya irabu tamati.
Kuhusiana na swala la iwapo kuna tofauti yoyote kati ya mzizi na kiini, Gabarage anaeleza kuwa dhana hizi mbili zote ni sawa. Akinukuu maelezo ya Wakuza Mitaala Ya Elimu TE (1996), anatoa mifano hii:
Maneno kiini
Anaezeka ezek
Uongozi ongoz
Piga pig
Kwa upande mwingine Gambarage anatofautisha mzizi (kiini) na shina. Kwa kutumia maelezo ya TE, anatoa mifano inayodhihirisha kuwa shina hujumlisha mzizi na viambishi tamati vya baadhi tu ya kauli bali sio vyote kama vile vya udumishaji na usababishi.
Maneno kiini shina
Shikishana shik shikish
Elekeza eleke elekez
Shikilia shik shikili.
Mipaka baina ya Mzizi na Mashina
Kutokana na maelezo yake Gambarage, sifuatazo ni baadhi ya sifa zinazobainisha mizizi na mashina.
Hajo pambanuzi za mzizi:
Ni sehemu ya neno inayohusika katika uundaji wa neno jipya.
Ni kiini cha neno ambacho hupambanuliwa na mofolojia ya mnyambuliko.
Ni kiini cha neno kinachoishia na konzonanti.
Ni sehemu ya neno isiyobadilika.
Ni sehemu ya neno isiyochanganuliwa Zaidi.
Hoja pambanuzi za mashina:
Ni sehemu ya neno ambayo haiwezi kuunda neno jipya.
Ni umbo la neno ambalo hupambanuliwa na mofolojia ya uambatishi.
Ni kiini cha neno kinachoishia kwa irabu.
Hata hivyo Gambarage anatoa tahadhari kuhusu mtazamo wa hoja ya umbo la mzizi kuwa ni kiini cha neno kinachoishia na konzonanti. Anadai kwamba hoja yenyewe kwa upande mmoja ni sahihi na kwa upande mwingine siyo sahihi. Ni sahihi kwa sababu ni kweli kuwa mizizi mingi ya vitenzi vya Kiswahili huishia na konsonanti. Lakini si kweli kuwa wakati wote mizizi huishia na konsonanti na mashina huishia na irabu. Anatoa thibitisho kwa kauli yake kwa mifano hii:
(i) hubiri (T) wa-hubiri (N)
(ii) sinzi-a (T) u-sin-gi-zi?(N) u-sinzi-a-ji
(iii)tembea (T) ma-tembe-zi
(iv) kimbia (T) m-kimbi-zi/ m-kimbi-a-ji (N)
(v) wewe (W)
(vi) lazima (Ts)
Kupitia mifano hii hapa juu, ni wazi kuwa ipo mizizi mingi katika lugha ya Kiswahili inayoishia kwa irabu. Kwa upande mwingine hoja kuhusu umbo la shina ni wazi kuwa shina linaweza pia kuishia na konsonanti kama anavyoonesha kupitia mifano hii:
(i) shikish - katika shikisha
(ii) pigw - katika pigwa
(iii) kimbiz - katika kimbiza
(iv) kalik - katika kalika
Katika mifano hii hapa juu ni kweli kwambakwamba mashina yanaweza kuundwa na mzizi na kiambishi kimoja cha kauli. Katika mifano hii mizizi ni shik-, pig-, kimbi-, na ka- mtawalia. Kupitia mifano hii Gambarage (2007) amethibitisha kuwa si mashina yote huishia na irabu.
Kuhusiana na sifa ya mizizi kuwa sehemu ya neno isiyobadilika,Gambarage kwa kutumia mifano ifuatayo ana maoni kuwa baadhi ya mizizi hubadilika kwa kuchukua maumbo tofauti ilhali nyingine haibadiliki. Tazama:
i. (a) chez-a chez-e-a chez-esh-a
(b) za-a za-li-a za-lish-a
(c) samba-a samba-z-i-a samba-z-a
ii. (a) pend-am-penz-i
(b) Pand-am-panz-i
(c) lind-a m-linz-i
(d) suk-a m-sus-i
(e) chek-a m-chesh-i
(f) pik-a m -pish-i
Mifano hiiinathibitisha upande mmoja wa hoja kuwa kuna maneno ya Kiswahili ambayo mizizi yake haibadiliki. Lakini mifano katika (ii) inathibitisha hoja kwa upande mwingine kuwa kupitia michakato ya kimofofonolojia mizizi huweza kuathiriwa na kuchukua umbo jingine ambalo ni la nje.
5.0 Hitimisho
Tunaweza kuhitimisha hoja yetu kwa kukubaliana kuwa hoja na 4.1.5 ni sahihi zaidi katika kueleza dhana ya mzizi na shina. Ni ukweli usiopingika kuwa mzizi ni kiini cha neno ambacho hakiwezi kuchanganuliwa zaidi bila kupoteza uamilifu wake kisarufi. Kuhusu fasili ya shina tunaweza kusema kuwa shina ni sehemu ya neno ambayo inaundwa na mzizi na kiambishi angalau kimoja au na muambatano wa mizizi katika maneno ambatani. KISWAHILI JUZ. 74 24
MAREJEO
Bauer, L. (1983). English Word-Formation. Cambridge. Cambridge University Press.
Good, J. (2005) “Reconstructing morpheme order in Bantu: The case of causativization and applicativization”. Katika Diachronic 22.3–57.
Good, J. (2007). “Slouching towards dependency: A family of mismatches in the Bantu verb stem”. Proceedings of the British Academy, Volume 145.
Hartman, R. (1972). Dictionary of Language and Linguistics. London. Applied Science Publishers.
Johannes, J.G. (2007). “The Ki-Nata Noun Structure”. Unpublished M.A Dissertation. University of Dar es Salaam
Kahigi, K. K. (2003). “The Sisumbwa Noun: Its Classes and Derivation”. In Occasional Papers in Linguistics. No.1. pp.1-86. University of Dar Es Salaam: LOT Publications.
Katamba, F. (1993). Morphology. Macmillan Press Limited. London.
Kihore na wenzake (2004) Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. TUKI. Dar es Salaam.
Kiango, J.G. (2000). Bantu Lexicography: a Critical Survey of the Principles and Process of Constructing Dictionary Entries. Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia and AfricaTokyo University of Foreign Studies. Japan.
Lyons, J. (1968). Introduction to Theoretical Linguistics. Cambridge. Cambridge University Press. United Kingdom.
Massamba D.P.B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI, Dar Es Salaam.
-------------------- (1996) Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Meeussen, A.E. (1967). Bantu grammatical reconstructions. Tervuren: Tervuren.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers, Nairobi.
Mohamed, M.A. (1993). Sarufi Mpya. Press and Publicity Centre. Dar es Salaam.
Mwansoko, J.M. (2006). Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu. TUKI. Dar es Salaam.
Polomé. E. C. (1967). Swahili Language Handbook. 1717 Massachusetts Avenue: Centre for Applied Linguistics.
Rugemarila, J. M. (2005). A Grammar of Runyambo. Dar es Salaam: Languages of Tanzania (LOT).
Schadeberg T. C. (1995). “Spirantization and the 7-to-5 Vowel Merger in Bantu” katika Belgian Journal of Linguistics. Vol. 9. pp. 73-84
Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato Cha Pili. Oxford University Press. Tanzania.
TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam