Sunday

Wanafunzi 485,866 wa Kidato cha Nne kuanza mitihani kesho

0 comments


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la

Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles  Msonde amesema jumla watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 kati yao wa shule ni 433, 052 na 52, 814 wa kujitegemea.
Dk Msonde ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 wakati akizungumza kuhusu kuanza kwa mitihani hiyo kesho  katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema kati ya watahiniwa 433,052 waliosajiliwa wanaume ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wanawake 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842.
“Mwaka 2018 idadi ya watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 427,181.Kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 5,871 kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana,” amesema Dk Msonde.
Dk Msonde amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote za muhimu zinazohusu mchakato huo katika mikoa ya yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani, wamiliki wa shule, walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani huu. Hatutasita kumchukulia hatua  mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha aidha Mtandao Huu Mashele Swahili unawatakia mtihani mwema watahiniwa wote

No comments:

Post a Comment