Masshele Swahili
Tamathali za semi ninani?
Hii ni Msemo ambayo hutumiwa kutoka maana tofauti na maana za maneno yake.
Zifuatazo ni baadhi ya tamathali za semi
i) Tashibiha, Huu ni ulinganishi wa vitu au halipo mbili tofauti kwa kutumia maneno kama vile, kama, mithili ya, Sawa na, utadhani ni, Sawa na
Kwa mfano, anaimba vizuri kama Ally kiba
ii) Sitiari, Huu ni ulinganishaji wa vitu au halipo mbili, na ulinganishaji huu huwa ni wa moja kwa moja
Mfano Juma ni simba
iii) Mubalagha
Huu ni uelezaji wa jambo kwa kutia mno chumvi kuliko uhalisia.
Mfano
Manyama ana tumbo kama gunia.
iv) Tashihisi, hii ni hali ya kuvipa vitu visivyo binadamu sifa za ubinadamu.
Mfano, Jua likasema siwezi kuendelea na safari
V) Taashira, Hii ni njian ya kutaja kitu Fulani kwa lengo la kuwakilisha kitu au jambo jingingine.
vi) Taniaba, hii ni njian ya kutumia jina Fulani kwa namna ya ulinganisho ili kumaanisha kitu kingine. Ambavyo huwa na tabia Fulani linganifu. Mfano kiongozi Huyu ni Idi amin wa kizazi hiki.
Tamathali nyingine ni kama
majazi,
Tafsida
Dhihaka
na Ritifaa
www.masshele.blogspot.com