Naposema mwanga wa blue wengi watafikiria ule mwanga unaotoka kwenye taa za blue,Ila sio huo naouzungumzia hapa.
Mwanga tunaoona kutokea kwenye jua,taa,simu nk inakuwa ni muunganiko wa mawimbi ya umeme-sumaku (electro magnetic waves). Mawimbi haya yanaposafiri huzalisha nguvu. Mawimbi yakiwa mafupi ndo huzalisha nguvu nyingi zaidi na mwanga wenye mawimbi marefu unakuwa na nguvu kidogo. Kila urefu wa mawimbi unawakilishwa na rangi na hapo ndipo tunapata makundi mbali mbali mfano X ray,gamma rays, ultra violet rays.
Katika aina za mawimbi hayo ya mwanga macho yanaweza kuona baadhi (visible light).
Mwanga wa blue (blue light) mawimbi yake ni mafupi (short wave length) kwa hiyo unazalisha nguvu kubwa. Kuwa katika mwanga wa blue kwa muda mrefu ina madhara kiafya hasa kwenye macho na mfumo wa usingizi (circadian rythm)
VYANZO VYA MWANGA WA BLUE.
mwanga wa blue upo kila sehemu. Mwanga wa jua unakuwa pia na mwanga wa blue ndani yake. Vyanzo vingine ni TV,simu, taa za ndani mfano tube lights nk.
Kwenye mwanga wa jua unakua na mawimbi marefu hivyo kusababisha madhara ni kidogo sana. Kwenye vifaa kama TV na Simu,Computer na Tablets mwanga huu unakuwa na mawimbi mafupi hivyo ni rahisi sana kusababisha madhara.
Katika lens ya macho kunakuwa na seli za kukinga mwanga huu usiharibu macho japo kinga hii haiwezi kustahimili kiwango kikubwa cha mwanga huu.
MWANGA WA BLUE UNAATHIRI VIPI AFYA.
mwanga huu unapokuwa kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu husababisha uharibifu kwenye lens ya jicho na kupelekea matatizo ya macho.
Katika mwili kuna kichocheo kinachoitwa melatonin hii ni hormone inayosaidia kuweka utaratibu wa kusinzia na kuamka (circadian rythm). Hormone hii ndio inatuwezesha kutambua usiku ni muda wa kulal na mchana muda wa kuwa macho. Mwanga wa blue husababisha ubongo kupunguza uzalishaji wa hormone hii hali inayopelekea mtu kupata shida kwenye swala la kusinzia. Kwa ufupi inapelekea tatizo la kutopata usingizi endapo unakua na tabia ya kutumia vitu vyenye mwanga wa blue muda mfupi kabla ya kulala.
Tafiti zinaonesha kuvurugika kwa mpangilio wa kusinzia na kuamka (circadian rythm) inapelekea mwili kuzalisha hormone ya stress (cortisol ) kwa wingi hali ambayo inapelekea kuvurugika kwa hormone nyingine za mwili mfano hormone za uzazi.
NINI CHA KUFANYA.
Ni vyema kupunguza exposure ya mwanga huu wa blue hasa muda wa lisaa kabla ya kulala.epuka kuangalia simu au TV ndani ya nusu saa kabla ya kulala ili kuepuka kuharibu mpangilio wa uzalishwaji wa hormone ya melatonin inayosaidia tupate usingizi. Kwa sasa hivi TV za kisasa na baadhi ya simu zinakuwa na jinsi ya kuzuia mwanga huu (blue light filter). Kama simu yako ina blue light filter basi vyema usiku uweke katika mode hiyo ili kuepuka madhara ya mwanga huu.