Tuesday

VAN DIJK APAMBANISHWA NA MESSI NA RONALDO KUWANIA BALLON D'OR

0 comments


NYOTA Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Mohamed Salah, Sadio Mane NA Virgil van Dijk wameingia kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or iliyotangazwa Ufaransa jana.  
Mane na Van Dijk ni miongoni mwa wachezaji saba wa Liverpool katika orodha hiyo ambao wanaungana na nyota wengine wa Ligi Kuu ya England, Sergio Aguero, Bernardo Silva na Pierre-Emerick Aubameyang. 
Wachezaji wengine wa Liverpool ni Salah, Roberto Firmino, Alisson, Georginio Wijnaldum na Trent Alexander-Arnold ambao wote walikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotwaa taji la saba la Ligi ya Mabingwa. 
Ronaldo na Messi wote watakuwa wakiwania tuzo ya sita ya Ballon d'Or, wawili hao wakitarajiwa kuchuana tena msimu huu, huku mshindi wa tuzo hiyo mwaka jana,  Luka Modric akikosekana kwenye orodha hiyo ya watu 30.
Beki Virgil van Dijk wa Liverpool na Uholanzi ameteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu 

NYOTA 30 WANAOWANIA BALLON D'OR

Sadio Mane - Liverpool
Sergio Aguero - Manchester City 
Frenkie de Jong - Ajax/ Barcelona 
Hugo Lloris - Tottenham 
Dusan Tadic - Ajax
Kylian Mbappe - PSG
Trent Alexander-Arnold - Liverpool
Donny van de Beek - Ajax
Pierre-Emerick Aubameyang - Arsenal
Marc-Andre Ter-Stegen - Barcelona 
Cristiano Ronaldo - Juventus
Alisson - Liverpool
Matthijs de Ligt - Juventus
Karim Benzema - Real Madrid
Georginio Wijnaldum - Liverpool


























Raheem Sterling - Man City

Virgil van Dijk - Liverpool
Bernardo Silva - Manchester City
Heung-min Son - Tottenham Hotspur
Robert Lewandowski - Bayern Munich
Roberto Firmino - Liverpool
Lionel Messi - Barcelona
Kevin de Bruyne - Manchester City
Kalidou Koulibaly - Napoli
Riyad Mahrez - Manchester City
Antoine Griezmann - Barcelona 
Mohamed Salah - Liverpool
Joao Felix - Atletico Madrid
Eden Hazard - Real Madrid
Marquinhos - PSG

No comments:

Post a Comment