Friday

Jocker: Filamu itakayokupa sababu za wachekeshaji kukosa furaha inayodumu

0 comments


Kuonewa na kutengwa na jamii inayomzunguka, kunafanya filamu hii iliyogharimu Sh126 bilioni kuwasilisha kisa cha Fleck ambaye anakuwa kiongozi wa wahalifu wengi wanaojificha nyuma ya kifunika uso (mask) kwenye jiji la Gotham. Picha|Mtandao.

  • Inasimulia maisha ya Arthur Fleck (Joaquin Phoenix) baada ya kutengwa na jamii
  • Jifunze madhara ya upweke na umuhimu wa marafiki.
  • Kwa Sh126 bilioni, mkasa wa Jokeri aliyepoteza mwelekeo unasimamiwa na Todd phillips.

Dar es Salaam. Mazoea ya mfuatilia vichekesho (Comedy) ni kumuona jokeri akichekesha. 
Lakini mambo siyo mambo kwenye filamu ya “Joker” ambayo imeingia kwenye kumbi za sinema leo (Oktoba 4, 2019) kwani filamu hiyo siyo tu inabadilisha taswira ya jokeri (Joker) inakufanya ufikiri mara mbili kila umuonapo mchekeshaji yeyote.
Wengi husema kati ya watu wasio na furaha duniani ni wale wanaowapa furaha wenzao. Msemo huu umetia nanga kwenye filamu hii kwani Arthur Fleck (Joaquin Phoenix) ambaye ni mchekeshaji aliyeshindwa kuendeleza malengo yake anageuka kuwa mhalifu.
Kuonewa na kutengwa na jamii inayomzunguka, kunafanya filamu hii iliyogharimu Sh126 bilioni kuwasilisha kisa cha Fleck ambaye anakuwa kiongozi wa wahalifu wengi wanaojificha nyuma ya kifunika uso (mask) kwenye jiji la Gotham.
Jifunze jinsi upweke na kutengwa kunaweza kukusababishia uendawazimu na hata kufanya “U turn” katika maisha yako.

Kama umewahi sikia msemo wa “good guy gone bad”, tembelea Mlimani City, Mkuki House, Aura Mall na kumbi yeyote ya filamu kuwaona Zazie Beetz (Dead pool, Atlanta na Geostorm), Robert De Niro ( The Irish man na Good Fellas), Frances Conroy (Cat woman) na wengine wengi  wakikuonyesha nini maana halisi ya msemo huo.
Unakosaje filamu iliyoongozwa na kiongozi Todd Phillips aliyekonga nyoyo za mashabiki wake katika filamu za A star is bornThe Hangover  (Sehemu ya1, 2 &3), na hata War Dogs.

No comments:

Post a Comment