Filamu hiyo ni Ad Astra iliyogharimu Sh229.8bilioni itaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema wiki nzima kuanzia leo.- Ikiongozwa na James Gray, kijana Roy McBride (Brad Pitt) anatakiwa kwenda angani kutatua changamoto za mradi wa kielektroniki.
- McBride ataweza kupingana na baba yake kuokoa dunia?, safari yake ni kama kujitoa kafara. Ataweza kuiacha familia yake?
Dar es Salaam. Unasababu nyingi za kukaa kwenye kiti cha kumbi ya sinema, kuweka mkono wako kwenye pembe moja ya kiti chako huku mkono mwingine ukitafuta bisi kwenye mfuko wa kilaji hicho ili kuburudika na filamu mpya iliyoingia sokoni wiki hii.
Filamu hiyo ni Ad Astra iliyogharimu Sh229.8bilioni itaonyeshwa katika kumbi mbalimbali za sinema wiki nzima kuanzia leo.
Ikiongozwa na James Gray, mkasa tungwa “fictional” wa kijana Roy McBride (Brad Pitt) anatakiwa kwenda angani kutatua changamoto za mradi wa “Power surge” ulioanzishwa na baba yake kwa ajili ya kufanya tafiti ya masuala ya angani.
Akiwa na waigizaji wenzake Ruth Negga na Tonny Lee, McBride ameishi miaka mingi akijua baba yake (Tonny Lee) amefariki lakini anabaki mdomo wazi pale anapopata taarifa ya kuwa huenda baba yake yupo hai.
Akiwa hajapona baada ya kupata ajali, McBride anatakiwa kuzuia mradi wa “Power Surge” kwani unahatarisha usalama wa ulimwengu mzima.
- Safari ya kuzuia mradi huo ni ngumu kwani sio rahisi kukabiriana na baba yake ambaye mbali ya kuwa mzazi wake ni motisha kwenye utendaji wa kazi zake.
Je McBride ataweza kupingana na baba yake kuokoa dunia?, safari yake ni kama kujitoa kafara. Ataweza kuiacha familia yake?
Maswali hayo utayajibu baada ya kulipia Sh10,000 siku yoyote ila Alhamisi ambayo utalipia Sh5000 kuitazama filamu hiyo kwenye kumbi uipendayo Jijini Dar es Salaam
.
.