Masshele kiswahili
-Aina za msimu
-Sifa za msimu
-Umuhimu wa kutumia msimu
-Changamoto za kutumia msimu
°Misimu au simo ni maneno ambayo kwa kawaida huwa siyo sanifu, yanayozushwa na watumiaji walugha na baada ya muda mfupi huweza kutoweka ingawa kunamisimu inayodumu kwa muda mrefu na kisha kusanifishwa.
Aina za misimu, tunaweza kuigawa kutokana na aina za uundwaji wake
a, misimu inayotokana na kubuni maneno mapya kabisa, mfano
Nyomi- kujaa watu
Nguna- Ugali
b, misimu inayotokana na kuunda nahau
Mfano
Piga pamba
Piga mbonji
Misimu inayotokana na kuchukua maneno ya lugha nyingine mfano
Menyu- chakula
Kumaindi- kuchukizwa
Laivu- Bila kificho
Misimu inayotokana na kuyapa maneno ya kawaida maana mpya
Pochi- fedha
Kitimoto- nguruwe
Kumlalia- kudhulumu
Misimu inayotokana na kuoanisha sifa
Mfano
Mguu wa kuku- bastola
Sifa za misimu
-Haidumu
-Inachumvi nyingi
-Ni maneno yasiyosanifu
-Hueleweka na watumiaji wa lugha hiyo
-Huchukuliwa kama lugha isiyona heshima.
Umuhimu wa misimu
-Kukuza lugha
-Kupamba lugha
-tafsida
-Huhifadhi historia
www.masshele.blogspot.com