Monday

UTANGULIZI WA UCHAPISHAJI KWA KISWAHILI

0 comments
-Historia ya uchapishaji
-Michakato ya uchapishaji
-Wadau wa uchapishaji
-Uchapishaji na tehama
-Uchapishaji katika karne ya 21
-Uchapishaji Afrika mashariki.
Dhana ya uchapishaji
Kwa mujibu wa M.M.Mulokozi (2014)
Ni mchakato wa utoaji na usambazaji/uenezaji wa taarifa kwa watu wengi katika umbo mahususi.

Uchapishaji lenye kisawe publishing katika kingereza litokanalo na neno Public lenye kisawe hadharani katika kiswahili hivyo publishing/ uchapishaji ni mfumo mzima kuweka maandishi hadharani kwa watu wengi katika umbo fulani.

Uchapishaji ni matokeo ya mwingiliano wa maendeleo na mabadiliko ya kijamii na kiufundi, hasa uandishi na kisomo, ugunduzi wa karatasi, na ugunduzi wa uchapaji, dhima ya dini, siasa na biashara.

Uchapishaji ulianza kwenye ueneaji, kisha uandishi na hatimaye uchapaji.


Uchapishaji simulizi, ulihusu ngoma, ngomezi, ala mbalimbali za sauti n.kk

Uandishi: ulichochewa na umuhimu wa kuweka rekodi zabiashara, utawala, nasaba, kodi, vita na dini,
- michoro ya mapangoni Afrika na ulaya kuanzia kama karne 50,000 KK
-Kati ya karne ya 3400-3200 KK uandishi ulivumbuliwa huko Sumeria(Mesopotamia)
Na misri. Wasumeria walitumia Cuneiform na wamisri walitumiavmichoro ya picha(Hiemographic)  ambayo baadaye ilichanganywa na ishara za kifonetiki.

-Kama 1200KK huko China nako walianza kuandika kwa michoro ya dhana ya Ideografia aina ya maandishi iliyoenea mashariki ya mbali kama Japani na Korea.

-India nako walikuwa na aina yao ya maandishi ya michoro tangy 3200KK
-America hasa mexico, maandishi ya picha kuanzia kama 3000KK

-Africa hasa Ethiopia (Abbyessian) nao walikuwa na maandishi katika karne nyingi zilizopita kabala ya kristo.

itaendelea
www.massheleswahili.blogspot.com


No comments:

Post a Comment