UHAKIKI WA DIWANI YA DHIFA
Dhifa ni ushairi ulioandikwa na Euphrase Kezilahabi unaoweka bayana uchafu na maovu
yanayofanywa na watawala (viongozi) dhidi ya tabaka la chini ambao ni wananchi
(watawaliwa). Ambapo huonekana wakiishi katika maisha duni katika nyanja zote za
maisha ilihali viongozi wao wakiishi katika maisha ya starehe.
Kwa mjibu wa TET (1996), mtindo katika kazi ya fasihi ni ile tabia pekee ya mtunzi au
uandishi ambayo yaweza kumtofautisha mtunzi huyo na mwingine.
(T.Y) Mtindo ni ile tabia ya mtunzi ambayo inamtofutisha na mtunzi mwingine katika kazi
ya fasihi hata kama kinachotungwa ni kimoja.
Kwa mjibu wa Mayoka (1984), Ushairi ni mtungo wa kisanaa ulio na mpangilio maalum
na lugha ya mkato ambayo ndani yake ina vina, urari wa mizani na muwala maalum
ambavyo kwa pamoja huwa na fani na maudhui yahusuyo hisi fulani au tukio juu ya
maisha ya mtu au watu wa mazingira na wakati maalum.
Kwa mujibu wa Mlokozi na Kahigi (1979), ushairi ni sanaa inayo pambanuliwa kwa
mpangilio maalum wa maneno fasaha yenye muwala, lugha ya mkato, picha au sitiara au
ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuelekeza wazo au mawazo,
kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia
inayogusa moyo.
(T.Y) Ushairi ni utungo wenye upangilio maalumu w silabi na lugha ya mkato, ukiwa na
urari wa vina na mizani (kimapokeo) au kutokuwa na urari wa vina na mizani (kisasa).
Hivyo basi mtindo uliotumika katika ushairi wa Dhifa unaweza kubainishwa kwa
kuangalia vigezo vifuatavyo:-
Aina ya Ushairi;
Mwandishi amejikita zaidi katika ushairi wa kisasa kwa sababu katika kitabu kizima
kuanzia mwanzo hadi mwisho mwandishi hakuzingatia urari wa vina na, mizani. Hivyo
basi hii inaweza kubainishwa katika shairi la “kwa walimu wote” katika ubeti wa kwanza
kama ifuatavyo. Mfano;
Sikilizeni wimbo huu,
Nilipokuwa mtoto nilitwa Chacha
Kwa matamshi yangu ya sasa
Nilipokuwa kijana niliitwa Chaupele
Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele
Nilipokuwa mwalimu nikaitwa Bure. Uk- 1.
Kigezo cha idadi ya mistari;
Katika kigezo cha mistari iliyotumika, mwandishi ametumia mitindi tofauti tofauti ya idadi
ya mistari katika ushairi mzima. Hivyo ametumia idadi ya mistari isiyolingana hata kama
beti zilizotumika ni za shairi moja. Mfano, katika shairi la “Dhifa” linabainisha dhahiri
kwamba idadi ya mistari katika beti zake hailingani katika ubeti wa nne na ubeti wa tano
kama ifuatavyo:-
Mpambe masikini nyuma amekaa
Wacheza ngoma wakulima
Warukaruka jukwaani
Na
Palepale bila papara
Nzi akunja kiunoche
Kwa shibe anya kabisa.
Ni dhifa.
Hivyo basi kutokana na mifano hapo juu kwa kigezo cha idadi ya mistari iliyotumika, ubeti
wa nne una mishororo mitatu kwa kuitwa tathlitha na ubeti wa tano unamichoro minne
mbao unaitwa tarbia.
Kigezo cha mofolojia;
Mofolojia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia namna maumbo mbalimbali ya maneno
yalivyo katika lugha. Kwa ujumla mwandishi hakuzingatia kigezo cha mofolojia katika
ushairi wake kwani amekiuka utaratibu huu kwa sababu kuna baadhi ya maneno
yamefupishwa. Mfano,
Katika shairi la “Dhifa”, ubeti wa tano (5), katika katika mchoro wa pili ametumia
neno kiunoche badala ya kiuno chake. Uk- 27.
Vile vile, katika shairi la “Mlokole” ubeti wa tano (5) mshororo wa pili amefupisha
neno kwa kuliita mdomowe badala ya mdomo wake. Uk- 48.
Kigezo cha matumizi ya lugha;
Katika kigezo hiki mwandishi ametumia lugha rahisi yenye kueleweka kwa msomaji,
misamiati iliyotumika ni ya kawaida isiyo na ugumu wowote. Lakini pia ametumia lugha
ya picha kwa kiasi kikubwa. Mfano, Katika shairi la “kwa walimu wote” uk- 1, ametumia
lugha ya picha ambayo huonyesha wazi maisha halisi ya mwalimu akiwa kazini na pindi
anapostaafu.
Kigezo cha kisintaksia;
Sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia mpangilio wa maneno katika sentensi. Kwa
mfano, katika mfumo mzuri wa mazingira ya kisintaksia unaokubalika tunaanza na
nomino, kivumishi, na mwisho kitenzi. Mfano, “mtoto mzuri anacheza.” Hivyo basi
mtindo aliotumia mwandishi haukuweza kufuta kigezo hiki kama inavyotakiwa. Mfano,
katika shairi la “Mlokole” ubeti wa pili, mshororo wa pili unabainisha wazi kuwa
mpangilio wa kisintaksia haukufuatwa. Mfano;
Mdomowe ukigusa wangu mguu. Uk 48.
Kwa ujumla mwandishi amefaulu kufikisha ujumbe kwa sababu lugha iliyotumika
inaeleweka kwa wasomaji na vilevile mashairi aliyotumia yana zungumzia mfumo mzima
wa maisha ambayo jamii ya sasa inaishi kwani inajibainisha dhahiri kwamba kuna tofauti
kubwa kati ya tabaka la juu hukandamiza au kunyonya tabaka la chini.
MAREJELEO:
Kazilahabi F. (2008). Dhifa, Daisy Printers (K) Ltd Nairobi.
Mayoka Jumanne, M (1984), Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, Tanzania
Publishing House, Dar es salaam.
Mlokozi M.M na Kahigi K.K, (1979), Kunga za Ushairi na diwani yetu, Tanzania
Publishing House, Dar es salaam.
TET (1996), Kiswahili Kidato cha kwanza, Oxford University press, Dar es salaam.