Monday

Muhimbili imetoa kauli hii, kuhusiana na mgonjwa anayedaiwa kujigeuza ndege hospitalini hapo

0 comments

Hospitali ya Taifa Muhimbili imekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii, moja ikiwa ni video na nyingine ni sauti ikieleza kuhusu video hiyo kuwa ni mama mchawi amelazwa ‘Hospitali ya Muhimbili’

Imesema video hiyo sio hospitali ya Muhimbili kwa sababu, kwanza hakuna mgonjwa huyo wala hakuna wodi inayofanana hivyo katika hospitali hizo (Upanga na Mloganzila) na sare zilizovaliwa na wauguzi sio za hospitali hizo

Aidha, imebainisha kuwa wanafanyia kazi tarifa hiyo kwa ushirikiano na mamlaka husika ili kibaini aliyesambaza taarifa hiyo ya upotoshaji na udhalilishaji kwa mgonjwa yule na hatua stahiki zitachukuliwa akibainika

Video inayosambaa inamuonesha mwanamke huyo akiwa amezungukwa na Wagonjwa, Waangalizi wa wagonjwa na Wauguzi kwenye wodi ya hospitali akikemewa na kutakiwa aondoke baada ya kudaiwa kuwa anajigeuza kuwa ndege usiku na kuwa binadamu asubuhi

b2d01b28-5c67-4e11-bf82-cfc193269930-jpeg.1173101Reactions:

No comments:

Post a Comment