MOTO wa Amazon umeanza kusababisha matatizo ya kupumua kwa wananchi wa Brazil, huku Shirika la Kulinda mazingira Greenpeace likionya kwamba moto huo pia unaharibu msitu wa Bonde la Kongo Barani Afrika.
Shirika la Kimataifa la Ulinzi wa Mazingira Greenpeace limezitaka Serikali za mataifa yaliyo katika Bonde la Kongo kuchukua hatua zaidi kupambana na moto wa msitu wa Afrika ya Kati, katika wakati ambapo ulimwengu umeelekeza macho yake katika moto unaoteketeza msitu wa mvua wa Amazon huko Brazil.
Msitu ya Bonde la Kongo sehemu inayofunika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon, Kongo-Brazzaville na Cameroon, msitu unaoshika nafasi ya pili duniani baada ya msitu wa Amazon.
Kama ilivyo kwa msitu wa Amazon, msitu wa bonde la Kongo unachangia kusafisha hewa chafu ya kaboni kwa kiasi kikubwa na ni njia muhimu kwa mujibu wa wataalamu ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.