Shingo ya kizazi ni mlango wa kuingilia kwenye kizazi, sehemu hii ni sehemu ya chini kwenye mlango wa kuingilia mfuko wa uzazi. Kama ilivyo kibuyu, sehemu ambapo mdomo wa kibuyu ulipo ndivyo shindo ya kizazi inavyotaka kufanana.
Saratani ya shingo ya kizazi ni ya tatu kutokea kwa wingi kwa wanawake Duniani na inaongoza katika kusababisha vifo.
Saratani hii imepungua huko Marekani kwa sababu ya vipimo vya awali vinavyofanywa kugundua mabadiliko ya kisaratani katika shingo ya kizazi katika hatua za awali sana pamoja na kugunduliwa na kutumika kwa chanjo ya kinga juu ya kirusi anayesababisha saratani hii.
Ingawa wagonjwa wa saratani hii wamepungua huko marekani bado ugonjwa huu unaongezeka katika nchi zinazoendelea ambapo upimaji wa awali wa kugundua saratani hii na matibabu bado ni changamoto.
Saratani ya shingo ya kizazi mara nyingi hukua taratibu. Kabla ya saratani hii kuonekana kwenye shingo ya kizazi kuna mabadiliko hutokea,mabadiliko hayo ni kuonekana kwa chembe zisizo za kawaida zilizofanyika katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya kwa kitaalamu huitwa dysplasia(chembe zinazotokea zinaitwa dysplastic cells).Chembe hizi zinaweza kutoweka kwa baadhi ya watu bila au pasipo matibabu.
Chembe hizi (dysplastic cell ) zisipotibiwa zinaweza kubadilika kuwa saratani baada ya miaka fulani kupita, inaweza kuchukua miaka mingi kwa chembe hizi kubadilika kuwa saratani
Dalili zipi za mtu mwenye saratani ya shingo ya kizazi?
Dalili za mtu mwenye saratani ya shingo ya kizazi huanza kujitokeza pale ambapo chembe hizi zinapo badilika tabia kuzaliana kwa kiasi kikubwa na kuleta madhara. Hivo awali kabisa saratani hii huwa haina dalili na ikiwa dalili zinaanza kuonekana huwa ni hizi/kati ya zifuatazo;
- Maumivu makali ukeni wakati wa tendo la ndoa
- Kutokwa na majimaji ukeni yanayonuka
- Kutokwa na damu ukeni, baada au kabla ya damu ya mwezi
- kwa mara ya kwanza mwanamke anaweza kutokwa na damu anapokuwa anajisafisha kwa mkono au anaposhiriki tendo la ndoa na baadae tatizo likiwa kubwa damu huweza kutoka bila hata ya kujisafisha au kushiriki tendo la ndoa na humaanisha hari ya mtu ni mbaya zidi
Mambo gani yanamuweka mwanamke kupata saratani hii?
- Kwa sababu saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na kirusi aina ya human papilloma basi ni vema kujua nini kinatokea kupata kirusi huyu. Kirusi aina ya human papilloma huambukizwa kwa njia ya ngono zembe yaani kufanya mapenzi na mtu mwenye kirusi huyu pasipo kutumia kinga. Hatari ya kupata kirusi huyu huongezeka kama mwanamke atafanya mapenzi na wanaume wanaotembea na wanamke zaidi ya mmoja kwani hao huweza hubeba kirusi huyu kutoka kwa mtu mmoja na kusambaza kwa mtu mwingine. Vile vile mwanamke akitembea na zaidi ya mwanaume mmoja ni rahisi kupata kirusi huyu
- Imeonekana kwamba kuanza mapenzi mapema (kwenye umri chini ya miaka 15) huwa ni kihatarishi cha kupata saratani hii kwa sababu mtu anayeanza mapenzi mapema huwa ni nadra sana kubaki na mpenzi yule yule maishani mwake na hivo huweza kuwa na mtu mwingine ambaye anavirusi hawa, lakini jambo la msingi ni kuwa na wapenzi wengi kunamweka hatarini mtu kupata kirusi huyo na saratani baada ya muda flani
Kumbuka: Baada ya kuambukizwa kirusi huyu mtu huchukua miaka 10 au zaidi kupata saratani hii na asilimia 5 ya wanawake walioathiriwa na kirusi huyu hupata saratani hii.
Mambo gani yanaongeza hatari ya kupata saratani hii endapo mtu ameathilika na kirusi cha human papilloma?
- Aina ya kirusi cha human papilloma HPV (wapo virusi aina tofauti, walio hatari kusababisha saratani ni HPV 16, 18, 31, 33, 35, 45, 52, 58. Aina ya 16, 18 na 45 husababisha kwa asilimia 94 ya saratani hii na kirusi aina ya 6 na 11 wameonekana kuwa na mahusiano kidogo sana kusababisha saratani hii ila husabaisha ugonjwa mwingine wa mioteo ukeni(genital warts)
- Kinga ya mwili ya mtu- ikiwa mwanamke anamagonjwa/madawa yanayoshusha kinga ya mwili kama virusi vya ukimwi (VVU), lishe duni na kinga ya mwili kushushwa na dawa fulani anaztumia basi humweka hatarini kupata saratani hii na ndani ya mda mfupi zaidi kuliko mwanamke asiye na matatizo hayo
- Sababu za kimazingira
- Uvutaji wa sigara pia unahusika kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia kadhaa, sigara imeonekana kuwa na kemikali zinazobadili tabia ya chembe hai za maeneo ya shingo ya kizazi na pia huhusika kusababisha saratani zingine mwilini
- Upungufu wa vitamini/viinirishi mwilini
- Pamoja na hayo kuwana wapenzi wengi au kuanza mapenzi kwenye umri mdogo huchangia kupata saratani hii
- Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango zimeonekana kuhusiana, kwa wanawake wanaotumia dawa hizi kwa zaidi ya miaka mi5 lakini uhusiano huu unaonekana kusababishwa na maambukizi ya HPV, kwa sababu wanawake hawa huwa wanajiamini kutopata mimba na wanashiriki ngono isiyo salama. Pia tafiti hazijaonyesha kwamba matumizi ya dawa hizi yanaweza kusababisha salatani moja kwa moja
Nini husababisha mabadiliko ya chembe hizi za shingo ya kizazi na kuwa na tabia ya saratani?
Tafiti zimefanyika kwa miaka mingi kugundua nini husababisha mabadiliko ya chembe hizi katika shingo ya kizazi na kuwa na tabia ya saratani na ikaonekana kuwa kirusi aina ya Human papilloma huhusika kwa kubadilisha tabia ya chembe hizi za shingo ya kizazi, kwa kiasi kingine imeonekana kwamba kemikali zilizo kwenye sigara huhusika na kubadilisha chembe hizi pia kisha kusababisha saratani.
Vipimo na matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi kama ikigundulika mapema huweza kutibiwa ipasavyo na mwathirika kupona kabisa, inashauriwa wanawake kuanza zoezi hili la kufanyiwa uchunguzi mapema zaidi kuanzia miaka 21
Vipimo vya utambuzi ni kama;
Kipimo cha PAP
Chembe chembe hai kutoka kwenye Shingo ya kizazi hukwanguliwa na kuchunguzwa maabara kama chembe hizo zina tatizo lolote
Kipimo hiki huweza kuonyesha chembe zenye saratani na chembe chembe zinazoelekea kuwa saratani
Kipimo kingine ni kupima DNA ya Kirusu HPV
Chembe chembe zilizokusanywa kutoka kwenye ukuta wa shingo ya kizazi hupimwa ili kuona kama kirusi huyu yupo kwenye maeneo hayo. Na inajulikana kuwa kirusi huyu husababisha saratani na wapo wa aina tofauti. Kipimo hiki hufanyika kwa wanawake ambao kipimo cha PAP kimesoma chanya na pia huwa ni uchaguzi kufanyika kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 30
Vipimo vya kuhakiki saratani
Kama daktari amehisi una saratani basi atakuchunguza kuanzia sehemu za siri na sehemu zingine za mwili. Kipimo kinachokuza mwonekano wa chembe kiitwacho colposcope hutumika kuangalia chembe zenye sifa za saratani. Wakati ukifanyiwa kipimo hiki chembe chembe hutolewa kwa kutumia kifaa hiki na kufanyiwa kipimo cha biopsy
Punch biopsy- kukatwa kwa kinyama kidogo kwenye shingo ya kizazi kwa ajili ya uchunguzi wa mabadiliko kwenye chembe chembe
Kukwangua ndani ya kizazi- kifaa kama kidogo kilicho na umbo la kijiko huingiza ndani ya mfuko wa kizazi na kuchukua baadhi ya chembe katika kuta hizo kwa ajili ya kipimo ili kuangalia kama saratani imefika huko.
Endapo vipimo viwili hapo juu wasiwsi daktari basi atafanya vipimo vingine kama
Kukata nyama kwa umeme
Hutmumia waya wenye umeme kidogo kukata kinyama nah ii hufanyika wakati umepewa kaputi
Cone biopsy-hukata umbo la koni ambapo huweza kuonyesha saratani imezama kwenye shingo ya kizazi kwa kiasi gani.
Vipimo vya kutambua Hatua ugonjwa
Hatua ya ugonjwa inaweza kutambuliwa kwa kufanya vipimo mbalimbali, ni lazima daktari akuambie hatua ya ugonjwa kwani matibabu hutegemea umefika hatua ipi. Vipimo vinavyoweza kumsaidia daktari kutambua hatua ya ugonjwa ni kama vile
Vipimo mionzi
Kama X-ray na CT scans, MRI na PET
Hivi humsaidia daktari kuona kama saratani imesambaa, na imesambaa kwa kiasi gani kutoka kwenye shingo ya kizazi.
Kipimo cha kuangalia kibofu na ndani ya njia ya haja kubwa
Kipimo kamera kinaweza muonyesha daktari maeneo hayo na kutambua saratani imesambaa kwa kaisi gani
Kipimo cha mikono ya daktari
Daktari atatumia mikono yake kuangalia sehemu mbalimbali za mwili na kwenye sehemu za siri ili kuona saratani imesambaa kwa kaisi gani
Historia ya mgonjwa
Kutoka kwenye historia ya mgonjwa namna anavyoumwa na dalili anazopata daktari ataweza kujua ni hatua gani ugonjwa umefika. Mfano mgonjwa anashindwa kukojoa basi hii inafahamika ni hatua ya tatu
Hatua za ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazizipo hatua nne
- Hatua ya kwanza-saratani imekaa kwenye singo ya kizazi tu
- Hatua ya pili- saratani ipo kwenye shingo ya kizazi na sehemu ya juu ya uke
- Hatua ya tatu- saratani ipo imefika sehemu ya nje ya tundu la uke au imesambaa kwenye kuta za oembeni ya kizazi, mirija ya mikojo huweza ziba hapa
- Hatua ya nne-saratani imesambaa kwenye viungo vingine vya mwili kama kibofu cha mkojo, ndani ya njia ya haja kubwa, mapafu mifupa ama ini
Matibabu
Matibabu ta saratani ya shingo ya kizazi hutegemea mambo mengi kama, hatua ya ugonjwa ilipofikia, m atatizo mengine ya kiafya uliyonayo. Upasuaji, mionzi na dawa za saratani au yote matatu huweza tumika katika matibabu ya saratani
Upasuaji
Hatua za kwanza za saratani hutibiwa kwa kuondoa mfuko wa kizazi . upasuaji huu huponya saratani ya kizazi endapo ipo kwenye hatua za kwanza na hupunguza uwezo wa saratani kujirudia. Unaweza kufanyiwa upasuaji wa
- Kuondoa kizazi tu
- Ama kuondolewa kizazi na sehemu ya uke na mitoki iliyo na saratani
Mionzi
Mionzi hutoa miali yenye nguvu kubwa kama X-ray ambayo huua chembe za saratani. Matibabu haya huweza kutumika yenyewe ama pamoja na dawa za kutibu saratani ili kuua chembe zinazobaki.
Tiba mionzi huweza kuwa
- Mionzi ya kupigwa nje ya mwili
- Mionzi ya kuwekwa ndani ya mwili- kifaa kinachotoa mionzi huwekwa ndani ya mwlili ili kuua chembe hizo
- Aina zote mbili
Wanawake wanaoelekea koma hedhi husimama kuona siku zao(hezi kukoma), kama matokea ya matiabu ya mionzi. Kama unataka mayai yako(kupata mimba baadae) yawe sarama basi ongea na daktari wako njia za kutunza mayai yako wakati wa matibabu.
Matibabu ya dawa za saratani(chemotherapy)
Matibau dawaza kuchoma kwenye mishipa hutumika na kuua chembe saratani. Dozi ndogo ya dawa za kuua chembe saratani na mionzi hutumiwa kwa pamoja, ili kuzuia madhara ya mionzi . Mionzi ya dozi kubwa hutumika kupambana na saratani iliyosambaa sana kwenye mwili