Ulimi kushikwa ni hali inayotambuliwa kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii hupelekea ulimi wa mtoto kuwa na uhuru kidogo wa miendo inayotakiwa kama binadamu wa kawaida
Mtoto mwenye Ulimi ulioshikwa huwa na utando ama ukuta mpana ulio chini ya ulimi na unashikamanisha ulimi kwenye sakafu ya kinywa. Mtu mwenye tatiazo la ulimu kifungoni huwa na tatizo la kutoweza kutoa ulimi nje yam domo, pia huathiri ulaji wa mtoto.
Wakati mwingine tatizo la ulimi kushikwa halisababishi tatizo llote lile, tatizo hili huhitaji matibabu ya upasuaji ili kuuweka ulimu kuwa huru
Dalili
Dalili za ulimi kifungoni ni kama vile
- Ugumu katika tendo la kuinua ulimi kutoka katika sakafu ya kinywa
- Kushindwa kutoa ulimi nje ya kinywa
- Ulimi kuonekana una umbo la moyo ama umegawanyika kama ukitolewa nje
Wakati gani umwone daktari
Mwone daktari endapo;
- Mtoto anadalili za ulimi kushikwa na anapata matatizo kama, kushindwa kunyonya vema
- Kama mtoto anaonekana kuathiliwa uongeaji wake
- Mtoto wako mkubwa analalamika ulimi wake umeshikwa na anashindwa kula, kuongea
- Mtoto anakereka na tatizo hilo
Visababishi
Kwa kawaida utando unaoshika ulimi hukatika kabla ya kuzaliwa, na kuruhusu ulimi uwe na uhuru wa kujongea miendo yote. Ulimi ukiwa umeshikwa inamaana utando uitwao lingual frenulum umebaki bila kukatika na hivo huunga ulimi na sakafu ya kinywa. Kwanini hali hii hutokea? Hazijulikani sababu moaka sasa ingawa baadhi ya mambo yanayoambatana na ulimi kushikwa yanajulikana kama vile sababu za kijeni
Vihatarishi
Ingawa ulimi kushikwa unaweza kuathiliwa mtu yeyote Yule, hutokea sana kwa wanaume kulika kwa wanawake.
Wakati mwingine tatizo hili hutembea kwenye familia Fulani tu.
Madhara ya ulimi kushikwa
Ulimi kushikwa huweza kuathiri ukuaji wa kinywa cha mtoto pamoja na kuchangia katika matatizo ya kula, kuongea na kumeza
Mfano huweza kusababisha
- Matatizo ya kunyonya. Mtoto akiwa ananyonya hutakiwa kutuliza ulimi chini ya sakafu yam domoakishindwa kufanya hivi huweza kusababisha kutafuna badala ya kunyonya na hivo kusababisha maumivu kwenye ziwa/chuchu za mama. Hili hupelekea mama kushindwa kumnyonyesha mtoto na kuacha unyonyeshaji. Madhara ya kuacha unyonyeshaji husababisha mtoto kutokua vema.
- Kushindwa kuongea. Huweza kuathiri kuongea sauti kadhaa kama "t," "d," "z," "s," "th" and "l." huweza kupata tatizo la kuongea r pia
- Hali duni ya usafi wa kinywa. Mtoto aliyekuwa, ulimi kushikwa unaweza kusababisha ulimi kutoosha mabaki ya chakula haswa yale yaliyo kwenye meno. Hili huweza kusababisha magonjwa ya meno na kinywa, ama meno kuoza
- Kutofanya kazi zingine za ulimi. Hushindwa kunyonya barafu, kulamba midomo, kubusu, ama kupuliza kifaa cha mziki kama fluti
Vitambuzi na vipimo
- Ulimi kushikwa hutambuliwa wakati wa uchunguzi wa kinywa cha mtoto.
Matibabu
- Matibabu ya ulimi kushikwa kwa watoto hutegemea sehemu moja na nyingine. Baadhi ya wataalamu wanashauri kutibiwa mara baada ya kuzaliwa ama tatizo linapoonekana hata kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbanii baada ya kujifungua. Hawa ni wataalamu wa kunyonyesha na madaktari.
- Utando unaoshika ulimi unaweza kulegea mda unavyokwenda na kusababisha tatizo kuisha. Na wakati mwingine tatizo linaweza lisiishe na hivyo kufanya matibabu mengine yafanyike
- Matibabu ya upasuaji huhusisha upasuaji wa kukata ute ama kukata ute(frenotomy ) na kuunga ulimi endapo tatizo lilikuwa kubwa yaani frenuloplasty
Wakati gani Mtoto atibiwe tatizo la ulimi Kushikwa-Tongue tie?
Ulimi kushikwa ni hali inayotambuliwa kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii hupelekea ulimi wa mtoto kuwa na uhuru kidogo wa miendo inayotakiwa kama binadamu wa kawaida
Mtoto mwenye Ulimi ulioshikwa huwa na utando ama ukuta mpana ulio chini ya ulimi na unashikamanisha ulimi kwenye sakafu ya kinywa. Mtu mwenye tatiazo la ulimu kifungoni huwa na tatizo la kutoweza kutoa ulimi nje yam domo, pia huathiri ulaji wa mtoto.
Wakati mwingine tatizo la ulimi kushikwa halisababishi tatizo llote lile, tatizo hili huhitaji matibabu ya upasuaji ili kuuweka ulimu kuwa huru
Wakati gani wa matibabu?
Matibabu ya ulimi kushikwa kwa watoto hutegemea na wataalamu uliokutana nao. Baadhi ya wataalamu wanashauri kutibiwa mara baada ya kuzaliwa ama tatizo linapoonekana hata kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbanii, na wengine wanashauri kukaa kwa mda Fulani kabla ya matibabu. Hawa ni wataalamu wa kunyonyesha na madaktari.
Utando unaoshika ulimi unaweza kulegea mda unavyokwenda na kusababisha tatizo kuisha. Na wakati mwingine tatizo linaweza lisiishe na hivyo kufanya matibabu mengine yafanyike
Kwa maana nyingine uiona dalili hizi mwone daktari:
- Mtoto anadalili za ulimi kushikwa na anapata matatizo kama, kushindwa kunyonya vema
- Kama mtoto anaonekana kuathiliwa uongeaji wake
- Mtoto wako mkubwa analalamika ulimi wake umeshikwa na anashindwa kula, kuongea
- Mtoto anakereka na tatizo hilo.