masshele Swahili
Nadharia ya tendo uneni ina matumizi ya kila siku katika mazungumzo yetu. Kwa kutumia mifano ya kutosha jadili nadharia hiyo.
1.0 Utangulizi.
Swali limegawanywa katika sehemu tatu, ambazo ni utangulizi, kiini na hitimisho. Katika utangulizi imetolewa maana ya tendoneni na aina ya tendoneni, hatua, masharti ya tendouneni, katika kiini imelezwa matumizi ya tendoneni, na mwisho ni hitimisho.
1.1 Fasili za Dhana za Msingi katika Swali;
Baktir (2011) anafasili tendouneni is an influential theory on the actual communicative funtion of language and tries to answer to what extent impartial interaction is possible between speakers. Tendouneni ni matendo yafanyikayo baada ya msikilizaji kuitika kauli iliyosemwa na msemaji (tafsiri yetu) fasili hii haitofautiani sana na fasili ya Resani (2014) anaye fasili kuwa ni tendo linalofanywa kulingana na tamko. Kwaujumla tendouneni ni tendo au ule mwitiko ufanywao na msikilizaji baada ya tamko kutoka kwa msemaji.
1.2 Historia ya Nadharia ya Tendoneni
Nadharia hii iliasisiwa na mwanafalsafa John L. Austin (1962) katika kitabu chake cha How do Things with Words, ambapo alidai kuwa kuna mambo mengi tunatenda kwa kunena, akiwa na maana kuwa kwa maneno tunenayo tu, tunatenda. Katika nadharia hii Austin anaeleza kuwa si sentensi zote hufanya kazi ya kuarifu jambo katika lugha pia si sentensi zote tunaweza kupima ukweli wake. Anaendelea kusema kuwa sehemu kubwa ya mawasiliano ya binadamu huhusisha maswali, mishangao, amri, na namna mbalimbali za kueleza hisia au matakwa ya watu. Hivyo baadhi ya sentensi ni vitendo au sehemu ya vitendo ambavyo msemaji anavisema kwa kutenda kwa njia ya kusema mfano katika sentensi zifuatazo,
•Ninakubatiza kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu.
Anayebatiza ni mchungaji/padri.
• Kwa hayo machache natangaza kufunga mkutano.
Anayefunga mkutano ni kiongozi.
•Kwa mamlaka niliyo pewa na jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakuhukumu
adhabu ya kunyongwa mpaka kufa.
Katika sentensi hizi zinaonesha utokeaji wa vitendo vinavyotokana na matamko.
1.3 Aina za matendouneni
Austin (1962) alitaja aina tatu za matendo uneni ambayo ni, kile kisemwacho, lengo la kusema, na matokeo ya kile kisemwacho. Hata hivyo Searle (1975) aliboresha aina za matendo uneni na katika uboreshaji wake anadai kuwa kunaaina nyingi za matendo uneni na pengine hazina ukomo. Hii ni kwasababu aina hizo hujikita katika lengo, muktadha na lugha husika. Kutokana na hayo alipendekeza aina tano za tendouneni ambazo ndizo tutazitalii katika swali hili Kama ifuatavyo:
Kwanza, Kitendoneni cha ahadi, haya ni matendouneni ambayo watu huwekeana ahadi na ahadi hiyo nilazima izingatiwe na itimizwe.
Kwa mfano
• Naahidi nitakuoa
•Naapa mbele ya mahakama hii nitakuwa mwaminifu katika sheria zilizowekwa.
Pili, kitendouneni cha maelekezo; Aina hii hujikita katika uelekezo au kuelezea. Mathalani hutumia vitenzi tendeshi ambay ni sihi, amrisha, omba, onya, shauri, na pendekeza
Kwa mfano,
• Mwanangu, nakusihi soma kwa bidii
• Nakuonya mbele ya umati huu acha tabia zako mbaya.
• Nakushauri ndugu yangu, acha kuvuta sigara.
Halikadhalika kuna matendouneni ya hisia, haya ni matendouneni ambayo hudhihirisha hisia, mtazamo, au mawazo ya msemaji juu ya jambo fulani. Mfano wa vitenzi tendeshi katika aina hii ni shukuru, pongeza, fariji,na samehe.
Kwa mfano
• Nimeamua kukusamehe mpenzi wangu
•Nakushukuru sana mama kwa wema wako kwangu.
Pia kuna matendouneni cha matamko, haya ni matendouneni ambayo kunenwa kwake hubadili ukweli fulani wa maumbo. Vitenzi tendeshi vinavyoweza kutumika katika aina hii ni pamoja na jiuzulu, achisha, fungua na funga. Matendouneni hayo huweza kujidhihirisha katika tungo zifuatazo:
• Nimeamua kujiuzulu.
•Natangaza kuufunga mkutano huu.
Aina ya mwisho ni kitendouneni uwasilisho.
Haya ni matendouneni ambayo hueleza kile ambacho mnenaji huamini kuwa ni kweli au sio kweli. Matendouneni haya hujumuisha maelezo, shadidia au mahitimisho.
Kwa mfano katika tungo zifuatazo:
• Wanawake sio waaminifu katika mahusiano
•Bidhaa za kichina sio imara
•Yanga ni timu mbovu
1.4 Hatua za metendouneni
Kwa mujibu wa Austin (1962) anataja hatua tatu za matendouneni kama ifuatavyo;
Moja, kitendo cha utamkaji, hiki ni kitendo cha kutamka neno au sentensi inayobeba fahiwa au maana fulani katika lugha husika. Tamko linaweza kuwa sauti ya msamiati au sarufi katika lugha husika. Tamko linaweza kuwa katika viwango mbalimbali kama vile neno au sentensi. Kwa mfano:
•Acheni kupiga kelele
• Watu wote ingieni ndani
Matamko haya ndio hatua ya awali ambapo msemaji huyatoa au kuyatamka
Hatua ya pili ni kuonesha nia au dhamira ya tamko. Mara nyingi nia hubebwa na vitenzi tendeshi kama vile kuahidi, kulaumu na kutisha. Kwa mfano katika sentensi zilizotolewa katika Hatua ya kwanza,
• Acheni kupiga kelele, msemaji huweza kuwa na nia ya kutaka watu wanyamaze.
Vilevile katika tungo ya pili, Watu wote ingieni ndani, mzungumzaji huweza kuwa na nia ya kuwataka watu wote wawe ndani
Hatua ya mwisho ni athari ya usemi, hii ni athari ya tamko kwa msikilizaji au hadhira na ndiyo hujibu swali la nini kilifanyika baada ya tendo kutamkwa kwa mfano katika tungo hizo hizo tulizo zitaja ambazo ni, Acheni kupiga kelele, msikilizaji anaweza kuitika kauli kwa kuacha kupiga kelele au kukataa.
1.5 Masharti ya Utokeaji wa matendouneni
Tendouneni halitokei tuu kiholela isipokuwa tuu kuwepo kwa masharti kadhaa yatakayotimizwa ili tendouneni liweze kutokea
Kwa mujibu wa Resani (2014) anataja masharti sita ya utokeaji wa tendouneni
1.5.1 Hadhi na mamlaka ya msemaji
Bartel (2012) akimnukuhu De Pietro (1994) katika utoaji wa tendouneni nilazima utambue mahusiano ya kijamii na hadhi ya kila mtu kwa kuwa tendoneni huhusisha hisia za msemaji na msikilizaji.
1.5.2 Mpokeaji sharti awe na muafaka
Katika utokeaji wa tendoneni hutokea pale ambapo msikilizaji au mpokeaji wa tamko hilo anaweza kulitenda
Kwa mfano , Mkuu wa chuo aliamuru mwanafunzi afukuzwe, hapa mwanafunzi sharti awe amekiuka taratibu na misingi ya chuo.
1.5.3 Hadhi na mamlaka ya msemaji
Katika sharti hili tutaangalia hadhi na mamlaka ya mtoa tamko dhidi ya msemaji
Kwamfano: Mkuu wa kituo cha Ostabey aliamuru Juma akamatwe.
Kutokana na tamko hilo polisi lazima watekeleze tamko kulingana na hadhi ya mtoa tamko.
1.5.4 Wakati muafaka wa tamko
Dhana ya tendouneni hutegemeana na wakati ambapo linatokea. Hivyo hadhira hutekeleza tamko kulingana na wakati.
Mwalimu alisema, kesho saa 5 kutakuwa na uwasilishaji , hapo inaonesha kukubalika kwa tamko hilo kulingana na wakati muafaka.
1.5.5 Kuwepo kwa Vifaa au Mavazi Maalumu ambayo huendana na Tukio Maalum au mahususi.
Ili tendoneni liweze kueleweka nilazima kuwepo na vifaa au mavazi yanayoendana na usemi husika. Kwa mfano: Jeshini lazima kuwe na vifaa vya kijeshi, na mavazi ya kijeshi
Vifaa na mavazi hayo huwezesha kutokea kwa tendouneni.
1.5.6 Kuwepo kwa lengo
Tendoneni huweza kukubalika iwapo lengo la tamko linadhihirika wazi kwa wasikilizaji na utekelezaji wake usiwe na ugumu ikiwa na maana kuwa tamko linapaswa kuwa na manufaa kwa wasikilizaji.
Kwa mfano: Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania aliwaamuru wananchi walime mazao ya chakula.
Utimizwaji wa masharti hayo ndiyo huwezesha utokeaji wa tendoneni.
2.0 Matumizi ya Nadharia ya Tandouneni katika Mazungumzo Yetu ya Kila siku
Nadharia hii ina umuhimu mkubwa katika mazungumzo ya watumiaji wa lugha kama ifuatavyo:
2.1 Kuongoza matendo ya mtu;
Baktr (2012) anasema the speech act control peoples behavior, on different occasions, this enabled when a tought of a listerner influenced by what he has heard from a speaker and take actions. ( Tendoneni huongoza matendo ya watu katika maeneo na matukio mbalimbali, hii hufanyika pale ambapo mawazo au ufahamu wa msikilizaji hupokea aliyo yasikia kutoka kwa mzungumzaji na kuyafanyia kazi. Kwa mfano: Wanafunzi nyamazeni, Wanafunzi baada ya kusikia usemi huo hukaa kimya.
2.2 Nadharia hii hubainisha nia ya msemaji.
Tendoneni huonesha lengo na nia ya msemaji na kuvifasili katika vitendo ambavyo msemaji au hadhira huvutenda kutokana na tamko. Kwa mfano Mwanangu leta sufuria, mwitiko wa mtoto kuleta sufuria hufasili nia ya mzazi wake kuwa alihitaji kuletewa sufuria.
2.3 Hutusaidia kuelewa maana ya ziada ya tamko.
Kutokana na nadharia hii tunapata maana za ziada za matamko na vilevile sehemu ya tamko haikusemwa bayana kwa Mfano katika tungo hii
Kula kula kichwa. Katika tungo hii msemaji huangalia mwitiko wa tamko kutoka kwa msikilizaji.
2.4 Husaidia kuimarisha mahusiano ya watu katika jamii.
Kwa mujibu wa Barktr (ameshatajwa) anasema kuwa, the role of speech act is to establish or rainforce social- relations to recognize the presence of each other since it's used to ask someone to do something, to get information and to express imotions (Tendouneni huleta na kuimarisha mahusiano mazuri miongoni mwa watu katika jamii kwa kuwa hutumika kuomba kitu au jambo, kutoa taarifa fulani, pamoja na kueleza hisia. Tafsiri yetu
2.5 Hudhihirisha maana ya tamko katika muktadha mahususi.
Maana ya tamko hutegemea zaidi muktadha mahususi ambao tamko limetokea.
Kwa mfano:
Niletee zege, tamko. Jibu kuleta zege, muktadha wake huweza kuwa sehemu ya ujenzi.
2.6 Huonesha uamilifu wa tamko na sheria za uafikishaji wake.
Hali hii hutusaidia kuelewa ruwaza za mawasiliano.
Kwa mfano:
Kufunga mlango yapo mawasiliano baina ya msemaji na msikilizaji.