Thursday

MHARIRI HANA NAFASI KATIKA KARNE YA 21 ?

0 comments




Mhariri amekuwa nguzo muhimu KATIKA kampuni za uchapishaji tangu shughuli za uchapishaji zilipoanza kufanya na makampuni mbalimbali.

Wahariri pamoja na kuwa kiungo muhimu kati ya kampuni, mwandishi na mchapaji bado wahariri wamekuwa wakifanya shughuli nyingine KATIKA kampuni za uchapishaji kama vile kutafuta msawada, kuhariri, matini, kutafiti masoko kabla mswada haujachapishwa, kunyoosha lugha, kuandaa mikataba, pamoja na kumshauri mwandishi.


Hali ipoje katika karne ya 21?

Katika karne hii ambayo inamapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia dhamani ya mhariri katika kampuni ya uchapishaji imeshuka sana. Hii nikutokana na uwepo wa nyezo za kidigitali zinazo weza kufanya majukumu ya mhariri.

Aidha uvumbuzi Wa kompyuta na kuzidi kupaa kwa matumizi yake kumepelekea waandishi wengi kujichpishia kazi zao wenyewe bila kuhusisha makampuni ya uchapishaji. Pamoja na hayo uchapishaji Wa mkondoni pia huenda umeathiri matumizi ya mhariri.

Pamoja na hayo shughuli zilizokuwa zinafanywa na mhariri  kama kunyoosha lugha huweza kufanywa na program za kompyuta.

Vilevile nyenzo za tehama zimepunguza matumizi ya mhariri mfano. Kampuni inaweza kutafuta mswada kupitia mitandao! Kutafuta soko kupitia mitandao na hata kuandaa mikataba.


Itaendelea
Info.masshele@gmail.com

No comments:

Post a Comment