Wednesday

MAANA/ DHANA YA ELIMU MITINDO

0 comments



Info.masshele@gmail.com
Dhana ya Elimu-mitindo inahistoria ndefu sana. Ipo mitazamo mbalimbali kjtokana na dhana ya mitindo na elimu-mitindo.

Mtazamo Wa wagiriki na warumi wa kale.
hawa walikuwa na mtazamo wao kuhusu mitindo kuwa ni kutumia maneno mengi lakini yasiyo na maudhui makubwa.
>mitindo ilitumika kama nyenzo ya kushawishi watu kufanya yafuatayo

1.kuwashawishi watu wavutiwe
2.Wasadiki
3.Kuyakubali yasemwayo.
> mtindo ulikuwa ni ufundi Wa kusema.
Mtazamo huu ulikuwa na mapungufu kwasababu mzungumzaji alikuwa anazungumza jinzi apendavyo na yeye ndiye aliye tawala mitindo.
>tunaweza kusema mtazamo huu ni finyu kwasababu ulijikita katika mazungumzo pekeyake.

∆Mtazamo wa pili
UHINDI YA KALE

>Mtindo ulichukuliwa kuwa mbinu ya kupamba mazungumzo, kuyafanya yapendeze na yawe matamu sana yafikiapo sikio

> kasoro
Tafsiri ya mtindo katika mtazamo huu unabanwa sana.

∆ MTAZAMO WA KARNE YA KATI
Katika karne ya kati mtindo uliambatanishwa na tanzu za fasihi andishi na katika kipindi hiki, kulifanyika majaribio mbalimbali katika tanzu mbalimbali.
>kwahivyo mitindo ya lugha ilihusishwa na tabia ya lugha zilizo jitokeza zaidi katika tanzu za fasihi.

Udhaifu wa mtazamo huu ni kuwa ulijikita katika  fasihi andishi tuu.

MTAZAMO WA MTINDO KAMA TABIA PEKEE YA KILA MTU.

>Idadi ya mitindo katika lugha ni saw a na idadi ya watu wanao tumia lugha hiyo. Mtazamo huu ulianzishwa na sana Isimu mambo Leo katika karne ya 20.

udhaifu
Idadi ya mitindo inakuwa kubwa mno.

MIKABALA KUHUSU MITINDO.
ni kazi ya mtunzi inayo mpambanu mtunzi mmoja na mwingine(Njogu & Chimerah)

aidha tunaweza kusema kuwa , ni upangaji wa fani na maudhui kwa namna ambayo inampambanua msanii mmoja na mwingine.

Vipengele vya mtindo ni
°Jazanda
°Motifu
°Taashira
°matumizi ya lugha
°Taharuki

UHUSIANO WA MTINDO NA MAUDHUI
tutaabiri mikabala minne
∆mkabala tenganishi
∆mkabala fungamani
∆mkabala wa uamilifu
∆mkabala jumuishi.

Elimu-mitindo maana na historian

Nidhana ambayo imepokea maana kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
° nitaaluma inayo chunguza mtindo.
Clucus (1955)
ni taaluma inayochunguza mitindo mbalimbali iliyopo katika usemi, matini andishi na nyaraka.

°Elimu mitindo inachunguza lugha ya kifasihi au uchunguzi wa tabia za lugha ya mwandishi Fulani na ruwaza yake ya uandishi.

° ni sayansi inayo chunguza jinsi wasomaji wanavyo husiana na lugha hasa ya matini za kifasihi ili kufafanua na kueleza namna wanavyo elewa na kuathiriwa na matini pindi wazisomapo.
°Ni taaluma/uchunguzi wa kisayansi wa mtindo unao weza kutazamwa kwa namna mbalimbali.
° nitaaluma inayo chunguza nduni za kiisimu , kama vile , fonojia, mofolojia, semantiki, sintaksia na pragmatiki

Ambazo kwa pamoja huathiri maana ya matini.

∆ Mtu muhimu aliye changia katika maendeleo ya taaluma ya elimu-mitindo ni mrusi ROMAN JACKOBSON.

MIKABALA YA ELIMU MITINDO.

∆Mtindo kama uteuzi
∆Mtindo kama MTU
∆mtindo kama ukengeushi
∆mtindo kama desturi
∆mtindo kama wakati
∆mtindo kama Hali

Itaendelea

Angalizo sehemu kubwa ya maudhui haya yamenukuliwa katika mihadhara ya kozi ya elimu-mitindo ya Dkt J. Bulaya
Hivyo makosa yeyote ya kiuandishi au upotoshaji nihusike Mimi.

No comments:

Post a Comment