Kikosi cha Simba SC kimeanza mazoezi leo jioni kwenye viwanja vya Boko Veteran tayari kwa maandalizi ya pambano la Klabu bingwa Afrika (CAfchampionsLeague) dhidi ya AS Vita Club litakalopigwa Jumamosi saa 1:00 usiku katika dimba la Taifa jijini Dar es salam'
Wachezaji Emmanuel Okwi , Erasto nyoni Juuko Murshid na wachezaji wengine wote waliokuwa majeruhi wamefanya mazoezi leo hii , ingawa kikosi hicho cha Simba kitaendelea kuwakosa beki Shomari Kapombe na Salum Mbonde wanaoendelea na matibabu.