
- Kwa sasa anafanya utafiti wa kina wa viumbe vidogo vidogo kwenye udongo utakaosaidia kuongeza tija katika sekta ya kilimo nchini.
- Ni mmoja ya wanawake ambao wanahitajika katika kuhakikisha wanakuwa mifano kwa kizazi cha sasa juu ya dhana ya ugumu wa masomo ya sayansi.
Dar es Salaam. Imekuwa ikiaminika kuwa watoto wa kike wengi wanaogopa masomo ya sayansi na kukukimbilia kuchagua masomo ya biashara au sanaa kwa kuwa ndiyo rahisi kuyasoma na hata baadaye kutoka kimaisha.
Hata
hivyo, ukweli ni kwamba kuna wanawake wamefanya mengi katika ugunduzi
wa vitu mbalimbali duniani baada ya kusoma vema na kuipenda sayansi. Wao
na sayansi, sayansi na wao tangu wakiwa wadogo na wanafanya vizuri
hadi sasa kuliko hata wanaume.
Miongoni mwao ni binti wa Kitanzania, Aneth David (29), Mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mwanafunzi Shahada ya Uzamivu (PhD) aliyejikita kufanya utafiti wa namna viumbe vidogo vidogo vilivyo kwenye udongo (soil microorganisms vinavyoweza kuongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo nchini.
Utafiti
wake unajaribu kuelewa uhusiano kati ya viumbe hivyo na mfumo wa kilimo
wa sukuma-vuta. Mfumo huu unatumiwa na wakulima wa mashariki na kusini
mwa Afrika kupambana na visumbufu vya 'stem borers' na magugu aina ya
kiduha ambayo husumbua mazao ya nafaka hasa mahindi na mtama.
"Matokeo
ya utafiti huu yanaweza kutumiwa kuboresha mfumo wa sukuma-vuta kuupa
tija zaidi na kuongeza uzalishaji wa mazao husika," amesema Aneth.
Kwa
mfumo wa elimu nchini na umri wake huenda ukapata maswali mengi
likiwemo kama alisoma nje kutokana na mafanikio yake ya haraka ya
kitaaluma.
Imekuaje
binti wa miaka 29 akafika ngazi hiyo kubwa ya kitaaluma hususan katika
masuala ya sayansi ambayo yametawaliwa na wanaume tu?
“Nimesoma elimu yangu ya msingi na sekondari mkoani Kilimanjaro na shahada yangu ya kwanza na umahiri nimesomea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,” Aneth ameiambia Masshele katika mahojiano ya hivi karibuni.
Binti
huyo alisoma Shule ya Sekondari ya Mawenzi kwa kidato cha kwanza hadi
cha nne na Shule ya Sekondari ya Majengo katika elimu ya kidato cha tano
hadi sita.
Ile
dhana ya kuwa tatizo ni ubora hafifu wa shule nchini ndiyo sababu ya
wasichana hawasomi sayansi kwa haifanyi kazi. Sayansi kwake ni wito wa
ndani wa mtu unaoweza kumpeleka mbali kama akiamua kuamini katika ndoto
zake.
Aneth anasema kuwa kwa sasa mambo yanabadilika na anaona wanawake wanaingia katika sekta mbalimbali za sayansi lakini bado ni wachache kutokana na tatizo linaloanzia mbali tangu mashuleni ambapo wanafunzi wa kike kwenye baadhi ya kozi za sayansi sio wengi.
“Bado nguvu inahitajika sana kwenye kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi na kuendelea na ajira kwenye sayansi,” amesema.
Mbali
na kuendelea na utafiti wake unaolenga kuchagiza uzalishaji wa mazao
nchini, Aneth ni mdau mkubwa wa masuala ya usawa wa kijinsia na amekuwa
akitumia muda wake wa ziada kuandaa na kushiriki katika makongamano
mbalimbali yenye lengo ya kumwinua mtoto wa kike hasa katika sekta ya
elimu kwenye mambo ya sayansi na teknolojia.
Sayansi
na teknolojia ni chachu ya maendeleo kwa sasa ulimwenguni na kampuni
kubwa zaidi duniani ni zile zinajihusisha katika sekta hizo kama
Microsoft, Facebook, Amazon, Novartis na Pfizer.
Anaamini katika kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta matokeo chanya katika jamii, na mara nyingi hutumia muda wake kushirikiana na wadau kama Buni Innovation Hub ili waweze kufikia malengo ya kuwainua watoto wa kike katika sayansi.
Anaamini katika kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta matokeo chanya katika jamii, na mara nyingi hutumia muda wake kushirikiana na wadau kama Buni Innovation Hub ili waweze kufikia malengo ya kuwainua watoto wa kike katika sayansi.

Aneth
ni mmoja wa mabinti wa mfano katika wanasayansi wachanga ambao
wanapenda watoto wa kike wasome masomo ya sayansi. Picha| Kwa hisani ya
Aneth David.
Licha
ya kuwa hasikiki kama walivyo baadhi ya wanawake nchini, Aneth amewahi
kupata tuzo ya balozi wa sayansi ambayo hutolewa na Jukwaa la Next
Einsteins Forum (NEF). Jukwaa hilo linakuwakutanisha Wanasayansi na
wadau mbalimbali duniani ili kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili
Afrika na maeneo mengine ulimwenguni.
Ushindi
huo ulimfungulia milango mingi zaidi ndani na kumpa uwanja mpana wa
kuchangia katika kuleta mabadiliko kwenye sayansi na teknolojia Tanzania
na Afrika kwa ujumla.
“Sio
lazima wote tuwe wahandisi au wahadhiri au watafiti, wanasayansi
wanahitajika kwenye kila eneo kwa sasa nchini na duniani kote,” amesema
David.
Amewazaje kumudu vyote hivyo kwa pamoja?
Hata
hivyo, kutokana na umri wake na vitu anavyofanya Aneth amesema kuwa
kitu kikubwa anachofanya ni kupanga ratiba yake ili usiingiliane na muda
wa kufanya utafiti ambao ameanza tangu mwaka 2016.
“Najipangia
malengo ya kila wiki, mwezi, robo mwaka na mwaka, supervisors
(wasimamizi) wangu wa PhD wanasaidia sana kuhakikisha ratiba ya shule
inaenda na muda wangu haumezwi na mambo mengine ya nje,” amesema David.
Kwenye
masomo ya sayansi, kwa mujibu wa Aneth, kuna fursa nyingi na maeneo
mengi ya kushiriki ambayo kila mtu anaweza kupata nafasi kama kwenye
mambo ya tiba, lishe, viwanda ,Tehama na mengineyo ni swala la
kuchagua nini kinakufaa na kukifanyia kazi.
Ujumbe
wake kwa watoto wa kike waliopo mashuleni ni kuwa watafute mifano hai
ya wanasayansi wanawake ili wapate kuwa chachu kwa maendeleo yao na
kujifunza kutoka kwao.