KWA kawaida tunazifahamu dawa za meno na tunatumia majumbani lakini pia zimezoeleka kuitwa kama dawa ya mswaki. Njia kuu moja wanayoifahamu watu wengi kuhusiana na dawa hizi ni kusafishia kinywa lakini imetambulika kwamba hakuna kiboko ya uchafu kama dawa ya meno.
Leo utapata kujua dawa hizo za meno zinaweza zikakusaidiaje nyumbani kwako tofauti na kusafisha kinywa tu.
TUMIA DAWA YA MENO KWA MATUMIZI YAFUATAYO
1: Tumia dawa ya meno kusafishia sinki nyumbani kwako kwa kutumia sponji au kitambaa laini.
2: Tumia kusafishia lensi ya kamera kwa kitambaa laini au tishu.
3: Wengi wetu tumekuwa tukipata shida kwenye camera zetu za simu kuwa chafu. Tumia dawa ya meno kufanya hivyo kwa kitambaa laini.
4: Kusafisha kioo cha simu kwa kutumia kitambaa laini au tishu
5: Usafi wa bomba za sinki kwa kutumia sponji.
6: Tumia kusafishia taa za gari lako kwa kitambaa laini au sponji
7: Tumia kusafishia pasi chafu kwa kitambaa laini au dodoki gumu la kuoshea vyombo.
8: Tumia kusafisha miwani kwa kitambaa laini
9: Tumia mswaki wenye dawa ya meno kusafishia Cheni Ya Silver
10: Tumia Kitambaa laini au tishu kusafishia CD
11: Tumia kusafishia kwenye njia za vigae vya ndani hata nje pia.
12: Tumia kupaka mkononi na kusafisha harufu mbaya ya chochote ulichoshika.
13: Tumia kusafishia kioo cha kujiangalia kwa kutumia kitambaa laini.
14: Tumia kusafisha viatu vyeupe kwa kupaka dawa kwenye mswaki.
15: Tumia kusafishia kucha za mikono kwa muda wa siku Tano utaona matokeo
16: Tumia kusafishia iliyogandia uchafu kwapani(njano)kwa kupaka dawa na sabuni ya unga kidogo.