i)
Sinonimia za kimantiki /logica /
synomimes.
Ni sinonimia zinazotokea pale ambapo
leksimu mbili au zaidi huweza kubadilishana nafasi katika sentensi afifu zhote
pasipo kuathiri masharti ya ukweli ya sentinsi hizo.
Mfano -Lengo,
Kusudi, Nia, Dhumuni, Mama anatembea pole pole / Taratibu. Haraka haraka, Upesi upesi.
ii)
Sinonimia
Kuntu (Absolute Synomimes)
Ni Sinonimia ambazo hutokea pale ambapo
Leksimu mbili au zaidi huweza kubadilisha nafasi katika miktadha yote bila
athari yeyote ya maana. Watafiti wanakubaliana
kuwa hakuna lugha yeyote duniani yenye sinonimia kuntu.
Hivyo ni vigumu kupata maneno yenye maana
sawa kwa asilimia moja.
“Eneo moja wapo linaloaza kuwa na Sinonimia
kuntu ni eneo la Silabi”
Mfano Ving’ong’o
au Nazali wakati wote vinaweza kubadilishana
Sintaksia - Saruji
miundo
Fonolgia -
Mofolgia
Elimu viumbe - Baiologia
VYANZO VYA SINONIMIA / SABABU
Habwe ba jaranja
i)
Ukopaji
wa misamiati
Maneno yakiwa na asili tofauti huleta hali
ya Usinonimia.
Mfano Neno
Shule limetoholewa toka lugha ya kijerumani “Schule “ lakini kuna neno “Skuli “
hili limtokana na School la kiingereza.
Maneno haya yanatumika katika lugha ya
Kiswahili wengine wanatumia Skuli na wengine Shule/
ii)
Jinsia
Hutokana na maneno yanayolejelea ama
mwanmke au mwanaume.
Mfano Hali
ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa kwa m-ke ni Utasa na Ugumba kwa mwanaume. Msichana mrembo lakini Mvulana mtanashati
Mwanamke aliyefiwa na mume - Mjane
Mwanaume aliyefiwa na mke -
Mgaje
Mwitiko Abee na Naam
iii)
Tofauti
za kijiogorafia au Maeneo Wazungumzaji
wa lugha moja ambao wanaisi katika
maeneo tofauti ya kijiografia wanaweza kuwa na maneno tofauti yanayorejelea
dhana au kitu kile kile.
Mfano Zanzibar
- Markiti
Tanzania
bara - Soko
Tanzania
bara - Umeme
Kenya
- Stima
Tanzania - Bomba
Zanzibar
- Mfereji
Tanzania - Dala dala
Kenya - Matatu
iv)
Taaluma
au Uwanja
Taaluma mbili mbili huwa na maneno mbali
mbali yanayotumiwa kurejelea kitu au dhana ile ile.
Mfano katika
riwaya kuna Aya lakini ushairi kuna Ubeti, maneno hayo yote
hutejelea kitengo au mfululizo wa maandishi.
v)
Wakati
Baadhi ya Sinonimia huzuka kutokana na
wakati.
Mfano Habwe
na Karanja
Kuna neno kama soko kuna mahali liliitwa Utuku
Mfano Zamani
wanyonyaji - Mabepari kwa sasa Mafisadi
vi)
Urasimi
Tunarejelea neno lipi ni sanifu kuliko
lingine
Mfano Hela,
fedha, pesa – neno rasmi ni fedha
Mpumbavu, mjinga – yanaonekana
rasimi kuliko fara, bwege n.k.
vii)
Ujumla
na Umahususi yapo maneno ambayo hutumika
kwa jumla na wakati mwingine hutumika kwa umahususi
Mfano Hamu neno la jumla
kiu – kinywa, njaa.
viii)
Rika
au Umri
Tofauti za umri na rika, yapo maneno ambayo
yanaonekana ni ya kitoto zaidi mengine ni ya kiutu uzima.
Mfano Piga - mtu mzima / kutandika chapa – mtoto
ix)
Elimu
au Hadhi
Watu wenye elimu tofauti tofauti hutumia
maneno tofauti, wakati mwingine huwa ni kutofautisha.
Mfano neno Afya – kawaida na Siha – kitaaluma njema
x)
Dini
Dini tofauti huwa na maneno tofauti kwa
ajili ya kuelezea dhana zinazolingana hasa Waislamu na Wakristo
Mfano Dhana ya kujinyima chakula kwa
minajili ya kupata fadhila za kidini Waislam
- Saumu na Wakristo - Kwaresma
Mahali pa kuabudia Wakristo - Kanisa
Waislamu – Msikitini,
Sala - Swala
NAMNA YA KUBAINI
KAMA NI SINONIMIA KUNTU AU SIO KUNTU
Kuna mbinu kuu 2:-
i)
Kuangalia
miktadha mbalimbali ya matumizi husika ya Sinonimia
ii)
Katika
mazungumzo au katika maandishi
1. KUANGALIA MIKTADHA MBALIMBALI YA
MATUMIZI YA SINONIMIA HUSIKA KATIKA MAZUNGUMZO AU MAANDISHI
Mfano Fahamu, Jua, Elewa,
je maneno haya yanatumika kote
·
Nilielewa
atakuja, Nilifahamu atakuja
-
Muasherati, kahaba, mzinzi - utofauti kidogo kimaana
2. *
Kutunga sentensi kahaa tofauti kwa kutumia kila Sinonimia kwa sentensi
moja kishi kubadilisha nafasi ya kila Sinonimia katika sentensi hizo na kuweka
Sinonimia nyingine
Mfano -Shimo, Tobo, na Tundu
i)
Hamis
alichimba shimo.
ii)
Suruali
ya Festo ina tobo
iii)
Chandarua
change kima matundu mengi
iv)
Ni
rahisi ngamia kupenya kattika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika
ufalme wa Mungu.
Hizo ni Sinonimia lakini sio Sinonimia
Kuntu.
Shimo
- kubwa, Vifaa jembe n.k.
Tundu
- Dogo zaidi
UANTONIMIA / UNYUME
Ni uhusiano wa kimaana baina ya maneno
mawili ambayo maana zake ni vinyume yaani maana ya neno moja ni kinyume cha
maana ya neno jingine
Mfano Neno - Nenda - Rudi Cheka - Lia Kubwa - Dogo
Kuna aina kadhaa
AINA ZA UNYUME AU UANTONIMIA
i)
Unyume
kamilishani / complimentary or simple antonyms.
Ni Unyume ambao unampaka usiopitika ambapo ukanushi wa upande mmoja ni
unenetezi wa upande wa pili
Mfano Mwanamke
- Mwanaume
Hai - Mfu
Pata - Kosa
Kweli
- Si kweli
ii)
Unyume
kadilifu (Gradable)
Ni unyume ambao hamna mpaka usiopitika
hivyo huweza kuelezwa kwa makadirio yaliyopo baina ya pande mbili husika. Ukamohi wa upande mmoja si lazima uwe ni
unenko wa upande mwingine (wa pili) kubwa
- ndogo si lazima kinyume cha
kubwa iwe ndogo kwani inaweza kuwa ndogo wastani n.k.
Zito
- nyepesi inaweza kuwa nzito
wastani n.k..
iii)
Unyume
elekeana (Relational Antonyms)
Ni unyume unaokuwepo pale ambapo uhusiano
baina ya leksimu mbili katika jozi huwa ni wa kiuelekeano yaani Leksimu
nyingine kutegema na Uelekeo yaa upande ambako tendo linaelekewa.
Mfano Nenda - Rudi -
Uelekeo Fulani yaani tenda linaelekewa wapi
Panda - Shuka
Sukuma - Vuta
Kushoto - Kulia
Mbele - Nyuma
Juu - Chini
Chomeka
- Chomoa
iv)
Unyume
Rejezi au Tenduzi
Ni unyume ambao huhusisha Leksim ambayo
kwazo tendo la Keksim mojawapo kuweza kubadilishwa ili kurejelea kinyube chake.
Mfano Chomoa - Chomeka
Ezeka - Ezua
Ziba - Zibua
UHOMONIMIA
Ni hali au uhusiano ambao umbo moja la
kiisimu huwa na maana nyingi zisizohusiana.
Mfano Panda
·
Kusia
mbegu
·
Kwea
mlima au mti
·
Tawi
la mti
Kaku
·
Ugonjwa
wa vidole
·
Ganda
la yai
·
Ndugu
mkubwa wa kiume
UPOLISEMIA
Ni Sifa ya neno moja kuwa na maana nyingi
zinazohusiana, au ni hali ya neno kuwa na maana nyingi zinazo husiana yaani
maana inakuwa moja lakini inahusiana na vitu vingi
Mfano Mdomo
(N)
wingi wake midogo
i) Ni sehemu ya nje ya kinywa inayomwezesha
kiumbe kupitisha
kitu chakula.
ii) Uwazi wa kitu
kama chupa ya birika n.k.
iii) Kinywa
Kichwa
i) Ni sehemu ya mwili wa kiumbe hai
ii) Ni injini ya gari moshi inayokokota mabehewa
iii) Ni kiongozi wa
familia
iv) Mtu hodari sana katika masomo
UHIPONIMIA
Ni uhusiano wa kiwima baina ya Maneno ambapo fahiwa ya neno moja hujumuishwa
katika fahiwa ya neno jingine.Ina maana kwamba maana za neno Fulani ni sehemu ya
maana y neno jingine. Kuna neon moja jumuishi
na madogo madogo na ili uelewe maana ya neno kubwa lazima uhusishe maneno
madogo madogo.
Neno lenye maana pana huitwa neno jumuishi
nayale yenye maana finyu huita Haponimia
MATUNDA
Ndizi Chungwa Embe Parachichi
Fahiwa ya neno Ndizi ni sehemu ya fahiwa ya
matunda hivyo ukitaka kuifasili ndizi utasema ni aina ya matunda, ili uweze
kuelewa maana ya ndizi, chungwa, embe, parachichi ni sehemu ya fahiwa ya neno
jumuishi ambayo ni Matunda
UMERONIMIA
Ni uhusiano ulipo baina ya Leksimu
inayotaja sehemu na ile inayotaja kitu kizima.
Mfano Mwili
-
Shingo
-
Kichwa
-
Mabega
-
Miguu
-
Tumbo
Meronimia inahusu kitu na sehemu zake,
nikitaka kujua kichwa ni nini nitarejelea sehemu mbali mbali za kichwa
MAANA KATIKA NGAZI YA TUNGO AU SENTENSI
Kuna vipengele 5
i)
Usawe
ii)
UtataUkinzani
iii)
Ukinzani
iv)
Upotoo
v)
Uziadu
– dufu
USAWE
Ni uhusiano baina ya sentensi mbili au
zaidi zenye kudhihirisha maana moja ya msingi.
Mfano Sikujua
kwamba usingeongea naye abadani
Sikufahamu kuwa usingezungumza naye
katu
Katika sentensi hizimaneno yanaetofautiana
lakini maana ile ile
-
Maelezo
yako yalikuwa magumu kueleweka
-
Ilikuwa
vigumu kuelewa maelezo yake
Katikasentensi hizi kinachotofautisha ni
mpangilio.
AINA ZA USAWE
i)
Usawe
wa kilekisika
ii)
Usawe
wa kimuundo
1.
USAWE WA KILEKSIKA
Ni Usawe unaotokana na sentensi mbili au
zaidi kuwa na maneno yenye maana ile ile ya msingi katika nafasi ile ile.
Mfano Sikujua kwamba usingeongea naye abadani
Sikufahamu
kuwa usingezungumza naye katu
Maneno yaliyotumika katika nafasi ile ile
yanabeba maana ya msingi
2.
USAWE WA KIMUUNDO
Hutokana na maana ya msingi ya sentensi
mbili au zaidi hubaki ile ile japo sentensi zina mpangilio tofauti. Hapa kinachozingatiwa saidi na muundo wa ile
sentensi.
Mfano Maelezo
yake yalikuwa magumu kueleweka
·
Ilikuwa
vigumu kuelewa maelezo yake.
Kilichotofautisha hapa ni mpangilio tu.
Mfano Hakuna
aliyelewa maneno yake ya ajabu
·
Maneno
yake ya ajabu hakuna aliyeelewa.
UTATA
Ni hali ambayo sentensi moja huwa na maana
au tafasiri zaidi ya moja au huwezi kuelewaeka kwa namna zaidi ya moja.
AINA ZA UTATA
i)
Utata
wa Kileksia / Kileksika
ii)
Utata
wa Kimuundo
UTATA WA KILEKSIA
Ni Utata unaosababishwa na matumizi ya
Homonimia na Polisemia
Mfano Baada
ya shida nyingi alifannikiwa kumleta Papa nyumbani
Papa - Mnyama
- Mkuu wa kanisa.
Siku hizi bei ya kanga na sh 10,000
- Ndege
- Nguo.
UTATA WA KIMUUNDO
Hutokana na jinsi sentensi ilivyo pangiliwa
au umbo la neno au kirai kuwa katika nafasi malumu katika sentensi.
Mfano - Wanawake na wanaume waangalifu
walikaa kando.
1. - Wanawake walikaa kando
- Wanaume waangalifu nao walikuwa kando
2. - Wanaume waangalifu na Wanaume
waangalifu walikaa
Kando
* Mtoto alilalia maziwa
- Alikunywa maziwa akalala
-
Alilala juu ya maziwa.
* Ananipenda
zaidi kuliko wewe
- Nyinyi nyote wawili mnanipenda
- Wewe unanipenda lakini mwenzio
ananipenda zaidi yako
UKINZANI
Ni hali itokeayo pendi kiyambo cha lugha
kinapokuwa na sifa Fulani na wakati huo huo hakina sifa hiyo.
Kiambo cha namna hii hunena kwamba mtu au
kitu Fulani kina sifa Fulani na wakati huo huo hakina sifa hiyo.
Mfano Mwanamke
Yule ni mwanamke kweli kweli
+
Me
- Ke
Bibi yangu nikijana kabisa.
+
Uzee
- Uzee
Yule kijana ni mwizi mtakatiu
+ Mtakatifu
- Mtakatifu
Huyu mtoto ni mtu mzima
+
Uzima
- Uto Uzima au
+
Utoto
- Utoto
Nilikwenda mbele nikarudi nyuma
+
mbele
- mbele
UPOTOO
Ni Ukiushi wa kisemantiki utokeao pindi
vijenzi semantiki viwili singanifu vinapounganishwa kueleziea jambo au kitu.
Mfano Alichora
barua kwa guu wa kushoto
·
Viatu
vyake vinacheka
·
Kaptura
yake inwasha taa
·
Kuchora
– haliendani na neno “barua” kifaa kinachotumika kuchora hakiendani na mguu (wa
kushoto)
·
Barua
– haichorwi
Viatu vyake vinacheka
*Matumizi holela ya maneno katika lugha
na husababisha upotoshaji
UZIADA
– DUFU
Ni urudiaji wa maneno usio wa lazima au
usiohitajika ambao hauifany sentensi kueleweka zaidi au haufafanui zaidi maana.
Mfano - Mke wangu ni mke wangu
·
Mwizi
ni mwizi tu
·
Mwanafunzi
ni mwanafunzi tu
·
Mwalimu
ni mwalimu