Hivi ni vifaa au ala zinazotumika kutoa sauti zilizo na uwezo wa kuwasilisha ujumbe fulani kutoka kwa mpigaji na mpigiwa.
Ala hizi ni za kisasa hasa nazo ni kama zifuatazo;
1.Filimbi , hutumika kwa askari , kutaarifiana vilevile kuonesha hali ya hatari au kukaa chonjo vilevile wakati Wa kufanya matukio muhimu kama vile kupandisha bendera filimbi hupigwa. Katika michezo ya mipira hasa kandanda mwamuzi hutumia filimbi katika kuamua matukio uwanjani.
2.Vuvuzela, hutumika katika matukio ya sherehe, pia kwa miaka ya karibuni yamekuwa yakitumiwa viwanjani, wakati Wa kushangilia Mpira.
3.Kengele, mwito Wa kuwakusanya watu
4.King'ora, hali ya hatari au msafara ya viongozi Wa afrika kingora huweza kupigwa
5.Toni ya simu
6. Milio ya ambulensi
Hizo no baadhi ya ngomezi za kisasa
Itaendelea.
Sifa za ngomezi
• Ujumbe huwa umefichika ile hali ya midundo na mapigo ya ngoma.
• Mapigo na midundo hii hufuata toni na wizani (ridhumu) kwa mujibu wa lugha ya wahusika au jamii husika.
• Ujumbe huweza kueleweka na kutafsiriwa na wanajamii au hadhira iliyonuiwa. Hulenga hadhira teule.
• Kila utaratibu wa ngoma hubainisha suala tofauti na ula mwingine
Kutegemea mapigo huweza kutofautisha baina ya habari za kutangaza hatari ya vita, harusi, au kifo cha kiongozi.
• Huweza kuwasilisha ujmbe wa dharura kwa njia ya haraka na ambayo si ghali ikilinganishwa na njia zingine.
• Ngomezi huongozwa na watu teule katika jamii ili kuhakikisha kuwa hakuna kutuma ujumbe unapotosha au kuwasilishwa visivyo.
• Ngomezi vilevile hutolewa wakati maalum mfano vita au vifo kitokeapo
Info.masshele@gmail.com