Tuesday

Breaking: Wabunge Watimua Mbio Bungeni....Ni Baada ya Alarm Kuanza Kulia Ikiashiria Kuna Tatizo

0 comments

Taharuki imeibuka Bungeni huku Kikao cha Bunge kikivunjika kwa muda na wabunge wakilazimika kukimbia kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Jumanne, Februari 5, 2019  asububi baada ya alamu ya Bunge kulia ikiashiria kuna tatizo.

Alamu hiyo imelia wakati Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba alipokuwa akijibu maswali bungeni hali iliyomfanya kukatisha majibu yake.

Alamu hiyo ya tahadhari  ilianza kupiga saa 5:02 hadi saa 5:08 asubuhi na kuanza kulia tena baada ya dakika kama 10.

No comments:

Post a Comment