Saturday

UHAKIKI WA RIWAYA ZA NAGONA NA MZINGILE PDF

0 comments
UCHAMBUZI WA RIWAYA ZA NAGONA NA MZINGILE

1.0 Utangulizi
Katika makala haya tutachambua riwaya za Nagona na Mzingile. Katika kuchambua riwaya hizi tutajikita katika kuangalia baadhi ya vipengele kama dhamira, falsafa, lugha, mtindo wa usimulizi, wahusika, motifu na suala la ontolojia.
2.0 Maelezo kuhusu mwandishi na riwaya zake
2.1 Maelezo kuhusu mwandishi
Euphrase Kezilahabi alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Namagondo kilichoko kisiwani Ukerewe katika ziwa Victoria nchini Tanzania. Alipata elimu ya msingi huko kijijini Ukerewe na baadaye alijiunga na seminari ndogo ya Nyegezi kwa ajili ya masomo ya upili. Baada ya kumaliza alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 1967. Katika masomo yake alijishughulisha na nadharia mbalimbali zihusuzo falsafa (Wamitila 1991:64). Mnamo mwaka 1976 alitunukiwa shahada ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kabla ya kutunukiwa shahada nyingine ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1982. Mwaka 1985, Kezilahabi alitunukiwa shahada ya uzamivu katika fasihi na Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison huko Marekani baada ya kukamilisha tasnifu yake ambayo ilihusu African philosophy and the problem of literature interpretation. Baada ya masomo yake huko Marekani alirudi kufundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kabla ya kuhamia Chuo Kikuu cha Botswana ambako anafundisha Lugha za Kiafrika na Fasihi.
Kezilahabi ameandika riwaya kadhaa kama vile Nagona, Mzingile, Dunia Uwanja wa Fujo, Kichwa Maji, Gamba la Nyoka. Kezilahabi ameandika vitabu kadhaa vya ushairi ambavyo ni pamoja na Karibu Ndani, Kichomi na Dhifa. Katika medani ya tamthilia, msanii huyu amentunga kazi tamthilia ya  Kaptula la Marx na hadithi fupi kama vile Mayai Waziri wa Maradhi, Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani nakadhalika.
Katika maisha yake Kezilahabi ametunukiwa tuzo kadhaa kutokana na uandishi wake. Miongoni mwa tuzo hizo ni ile ya kumbukumbu ya Edoardo Sanguinetti (1990) na ile ya kumbukumbu ya Shaaban Robert (1995) (Mezger 2002: 76).
2.2 Maelezo kuhusu riwaya zenyewe na muktadha wa utunzi
2.2.1 Riwaya ya Nagona
Riwaya hii ilichapishwa mwaka 1990. Riwaya hii inahusu motifu ya safari ya nguli wa kiume amabaye jina lake halikubainishwa na mwandishi. Nguli huyu anatumia muda mrefu kusafiri katika nyika na amechorwa kwa kupatilizwa tajiriba na uwezo usio wa kawaida. Katika safari yake anakutana na wanafalsafa mashuhuri. Miongoni mwao ni Marx, Nietzche na Freud ambao wamekaa katika duara wakizungumza na roho zao ambazo wamezitema katika viganja vyao. Kisha nguli huyu anagundua kuhusu kuwepo kwa paa wa ajabu na anaamua kumfuatilia kwa kuangalia nyayo zake. Ili kumkamata anapaswa kuhimili mafumbo mazito ya kimaisha ambayo yanaonekana kutokuwa na suluhu.
Ingawa majukumu hayo yanaonekana kuwa magumu, nguli huyo anafanikiwa kumpata paa kwa kusaidiwa na wazee wanne ambao wana uwezo wa ajabu. Baada ya kumpata paa ambaye anaonekana kuwa ni mwanamke mzuri, nguli anashindwa kutimiza masharti ya kummilika paa na hatimaye anamtoroka.
Katika sura ya nane kuna maungamo yanaonekana kufanyika ambayo kwa hakika ni vigumu kueleweka kama yanafanywa na nguli au vinginevyo. Mhusika anaonekana kuungama dhambi za karne mbili zilizopita ambazo wanadamu wamezitenda, anaungama dhambi hizo kwa padiri. Kisha katika riwaya hii mnaonekana kuna ngoma ya ungamo kuu inasubiriwa. Ngoma inapowadia, makundi mbalimbali kama vile ya wanafalsafa, wanasaikolojia, wanamapinduzi na vichaa yanajitokeza kushindana. Nguli wa riwaya hii anashiriki ngoma hii akiwa na kundi la vichaa. Mwisho wa riwaya hii msichana aitwaye Nagona anazaliwa na nguli anamfuata.
2.2.2 Riwaya ya Mzingile
Riwaya hii inaanza na kisasili cha kuzaliwa mtoto-kizee ambaye wanamwita Kakulu. Riwaya hii ni muendelezo wa riwaya ya Nagona. Kama ilivyo Nagona, riwaya hii nayo inahusu motifu ya safari ya shujaa asiye na jina. Shujaa huyu anajiita Mimi na ndiye msimulizi wa riwaya hii. Huyu Mimi anatumwa kupeleka ujumbe wa kifo cha Mkombozi wa pili kwa babaye anayeitwa Mzee. Lakini safari yake ya kumtamfuta Mzee inampeleka pia katika kutafuta kiini na maana ya maisha. Mimi anafanikiwa kumpata Mzee katika kijumba chake juu ya mlimani na kufanya naye mazungumzo. Hata hivyo Mimi anashindwa kumshawishi Mzee kuhudhuria mazishi ya mwanaye. Kutokana na hali hii Mimi anaamua kurudi na safari yake inampeleka katika kutafuta majibu ya maswali ambayo hajaulizwa. Inamchukua Mimi karne nyingi kufika kijijini kwake. Anapofika anagundua kuwa kijiji kimeharibiwa na mabomu ya nyuklia na kubaki magofu.
Anapoingia katika nyumba yake iliyoharibiwa, Mimi anamkuta Mzee na mazungumzo yanaendelea. Baada ya kitambo kirefu mvua inaanza kunyesha na uoto unarudi katika hali yake. Katika kipindi hiki mwanamke anajitokeza kimaajabu na kumuongoza Mimi kuelekea ulimwengu mpya na kumuacha Mzee ambaye baadaye anatoweka. Mimi na Mwanamke wanaishi pamoja na kuanzisha ulimwengu mpya. Wote wanaonekana kujua makosa yaliyofanyika zamani. Ili kuepukana na makosa hayo hapo baadaye, wanaamua kujenga ulimwengu mpya bila kutumia maarifa yaliyopo.
2.2.3 Kuhusu utunzi wa Kezilahabi

Soma zaidi hapa katika PDF >>>>>
     Bofya maandishi ya blue
                  HAPA

Inahifadhiwa na passwords
Nitumie gmail info.masshele@gmail.com
Au massheleemanuel@gmail.com
Au simu +255766605392 ili nikutumie passwords 

No comments:

Post a Comment