
Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 31, atajiunga na Chelsea wiki ijayo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu katika mkataba wenye mshahara wa pauni 270,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji watano wanaolipwa zaidi katika EPL. (Star)
Chelsea wamemuulizia Philippe Coutinho, 26, ambaye bei yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 100. (Express)
Real Madrid wana matumaini ya kumsajili Eden Hazard, 28, kwa chini ya Euro milioni 100 ambazo Chelsea wanataka, kwa sababu mkataba wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji unaisha Juni 2020. (Marca)
Everton wanapanga kupanda dau la pauni milioni 40 kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Mitchy Batshuayi, 25. (Sun)
Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 20, amesema huenda akashawishiwa kwenda Real Madrid siku zijazo. (AS)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema klabu hiyo huenda ikatafuta mchezaji wa kuziba pengo la Harry Kane, 25, ambaye ni majeruhi kwa sasa kutoka katika akademi yake badala ya kusajili mchezaji mpya. (London Evening Standard)
Meneja wa Arsenal Unay Emery ana matumaini ya kupata wachezaji wapya wiki hii huku taarifa zikimhusisha kiungo wa Barcelona Dennis Suarez, 25, kwenda Emirates. (Star)
Meneja wa Everton Marco Silva amesema tena kuwa ana imani klabu hiyo haitosajili mchezaji yoyote mwezi huu. (Liverpool Echo)
Napoli wamekataa dau kutoka AC Milan la kumtaka kiungo Amadou Diawara, 21, ambaye amehusishwa na kuhamia Tottenham na Wolves. (Inside Futbol)
Mkurugenzi mkuu wa Inter Milan Giuseppe Marotta anadai kuwa nahodha wa Atletico Madrid Diego Godin, 32, ambaye awali alihusishwa na kuhamia Manchester United, sasa anataka kwenda Italia. (Calciomercato)
Uhamisho wa Marko Arnautovic kwena China umefutwa kwa sasa baada ya Guangzhou Evergrande kujitoa kwenye mkataba wa kutaka kumsajili. (Daily Mail)
Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho amesema alifahamu tangu mwanzo wa msimu kuwa klabu hiyo haiko kwenye mbio za kuwania kushinda Ligi Kuu ya England EPL. (Manchester Evening News)
Jose Mourinho amesema amekataa kazi tatu tangu alipoondoka Manchester United. (Telegraph)