Na. John Walter-MANYARA
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limekubaliana kuwaelimisha na kuwahamasisha wazazi wa wanafunzi katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari kuchangia kwa hiari chakula kwa ajili kuwajengea mazingira rafiki ya kujifunza na kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.
Awali wakitoa michango yao walimtaka Mkuu wa Wilaya na Mwanasheria wa Wilaya ya Babati kuruhusu itungwe sheria itakayowalazimisha michango iwe ya lazima.
Mkuu wa Wilaya, Elizabeth Kitundu alisema ni muhimu wanafunzi kupata chakula cha mchana ili kusaidia kuongeza ufaulu.