Picha ya mtandao
Japo serikali inapinga vitendo vya ukeketaji kwa watoto wakike lakini kwa baadhi ya wazazi wilayani hapa wamekuwa wakifanya jambo hilo ni furaha kwao kwani mtoto akisha kekektwa kwao tayari ni fursa ya kujipatia kipato.
Diwani wakata ya Binagi wilayani hapa Marwa Chacha amesema matokeo katika ya sekondari Nyamwigura si ya kuridhisha kutokana na wazazi kutoa kipaumbele kuwaozesha mabinti wao hasa waliokeketwa.
Shule ya sekondari ya Nyamwigura ni mmoja ya shule zilizojengwa kwa nguvu za wananchi lakini kumekuwepo na changamoto ya wanafunzi wakike kutohitimu masomo yao jambo ambalo wazazi wanaliona ni kero kubwa kwao.
Magabe Tai na Helena Mnanka ambalo ni wakazi wa Kijiji cha Nyamwigura walisema wao kama wazazi wamekuwa kikwazo kikubwa cha wasichana wao kushindwa kufikia malengo yao ya masomo na kuishia kuolewa.
"Baadhi yetu tunapenda sana Mali kuliko mafanikio ya watoto wetu, watoto wanafaulu vizuri kwenda sekondari lakini si nyingi anaolewa na baba yake anachukua Mali kutokana na kupenda Mali kuliko Elimu," alisema Tai.
Helena Mnanka anatumia fursa hiyo kuimbo serikali kufuatilia wanafunzi wanaoacha masomo ili kubaini sababu za wako kufanya hivyo.
"Serikali ingekuwa inafanya sensa kwa wanafunzi wanaoacha shule kabla ya kuingia kidato cha tatu wangebaini huku kwetu kuwa wanafunzi wengi wanasimamishiwa masomo na kuolewa, jambo ambalo hukatisha ndoto zao," alisema Mnanka.
Naye Anthony Charles ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Nyamwigura alisema changamoto kubwa inayozikabili shule za seokndari nchini ni shule hizo kukosa hamasa ya kitaluma inayosababishwa na wazazi.
"Wazazi wamekuwa kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya wananfunzi wetu, wao wamekuwa wakiwatumia wanafunzi has a nyakati za shule na wakati mwingi kushindwa kufuatilia maendeleo yao pale wanapobaki nyumbani hawawaulizi sababu ya kufanya hivyo," alisema Charles.
Katika kuhakikisha wanaboresha utendaji na ufundishaji katika shule ya sekondari Nyamwigura wazazi walifanya harambee ya kununua vifaa kitaaluma katika shule hiyo kwa kuchangia zaidi ya sh, 3 milioni.
Maoni ya mhariri
Wazazi badilikeni wateteeni wanenu( E.mashele)