Pia ratiba hiyo itazikutanisha KMC na Tanzania Prisons ambao utakuwa mchezo pekee kuwakutanisha wapinzani wa Ligi kuu katika atua hiyo.
Azam FC watakuwa wenyeji wa ama Madini FC ya Arusha, au Stand ya Babati, Yanga SC wataikaribisha amaIhefu FC au Tukuyu Stars, zote za Mbeya na Simba SC watawaalika Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.
Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wao wataanza na Mtibwa Sugar na Kiluvya United ya Pwani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, wakati washindi wa pili Singida United wataanzia nyumbani pia Uwanja wa Namfua mkoani Singida dhidi ya Arusha FC.
Mechi zitachezwa wikiendi ijayo kuanzia Desemba 21 hadi 24 na hii moja kwa moja inamaanisha mechi itachezwa kabla au baada ya mchezo wa marudiano wa Simba na Nkana Desemba 23 Dar es Salaam, lakini mabingwa wa Tanzania Bara wanajivunia kikosi kipana.
Ratiba kamili hii hapa: