Monday

Salamba, Kagere waiua APR

0 comments


Timu ya simba imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya KAGAME baada ya kuwafunga APR ya Rwanda kwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao.

Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza.

Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.

Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2 na APR kutoka Rwanda wakiwa na 1

No comments:

Post a Comment